Kiswahili kitamu kutoka congo

Uchunguzi mwingi uliofanyika wa lugha ya kiswahili ulishaonesha kuwa wa Kongo ndiyo wanazungumza kiswahili asilia, kwani huko kwao ndipo kilipoanzia. Tofauti iliyotokea ni kuwa kiswahili cha pwani baadaye kiliingiza maneno mengi ya kigeni- hususan Kiarabu, Kireno, na Kijerumani na ndiyo kikazaliwa hiki kiswahili ambacho wengi wetu wanahisi ndiyo fasaha.

Hata mimi naamini hivyo kwani Kiswahili cha Kongo kina maneno karibu yote ya Kibantu wakati hiki tunachotumia viraka ni vingi tu (maneno mengi ni ya kuazima). Kitu cha muhimu ni kuwa Kongo wanazungumza kiswahili chenye lafudhi ya bara na siso wengine tunazungumza kiswahili cha lafudhi ya mwambao, ambacho kiliendelezwa zaidi na wafanyabiashara miaka iliyopita.

Ahsanteni.


Unamaanisha jimbo la Katanga?
 
Hii aliitoa rafiki yangu mmoja machachari sana pale ssc anaitwa BUTEMBO21
butembo.jpg
 
Nitakuja nyuma - Nitakuja baadae...
Nitakuya mbele - Nitakuja kabla.

Fasi gani - Wapi uko
Kutomboka - Kugombeza/kubwabwaja kwa hasira kutweta.
 
Wadau nimekuwa nawafuatilia sana watangazaji wanaoripoti kutoka Kinshasa na kwa hakika kiswahili chao ni cha kukufanya ucheke! Ebu angalia mifano hii kisha na wewe utupie ulichosikia:
1.Askari thelathini waliuwawa - Masoje makumi matatu walikufishwa
2. Wanasiasa - Wafanya siasa
3.Upande wa upinzani - Ng'ambo ya upinzani
4.Mara kwa mara - Maya kwa maya

hicho ni kilingala
 
Ukuye fasi ya huku - njoo huku
weye - wewe
usipime - acha kabisa
PDG - Pedeje
makuta - fedha
kabuchungu - dagaa wa Mwanza
nakuzidi kumasomo - nakuzidi elimu
 
Mbele ukule magharibi ukanawe vile kutakuwa kifukutu sana apres.......

Kabla hujala jioni uoge maana kutakuwa na joto sana baadae!
 
Back
Top Bottom