Kiswahili kitamu bwana

zegamba180

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
819
530
Unapoenda kumtembelea Zegamba kwake ukamuulizia ukaambiwa yupo ndani. Nawe uhitaji kuingia ndani. Je, utamwambia;
1.Toka nje ama
2.Toka ndani
lipi sahihi?
 
Je!nini unaelewa kwenye kiswahili ukiwasika watu wawili wanajibizana, mtu A anamuuliza B,,,,,"UPO,UPO?",na mtu B anamjibu mtu A,,,"UPO"
 
A: UPO UPO? upo kwa muda kidogo (muda si mrefu utaondoka)
B: UPO? Je upo kwa muda usiokadiriwa( kikomo cha uwepo hakipo bayana) yaweza kuwa siku, mwezi, Mwaka, miaka n.k
 
Je!nini unaelewa kwenye kiswahili ukiwasika watu wawili wanajibizana, mtu A anamuuliza B,,,,,"UPO,UPO?",na mtu B anamjibu mtu A,,,"UPO"
Naelewa kuwa A. Aliposema upo' upo? Upo ya kwanza ni kifaa fulani ambacho anakiulizia kwa neno lake la pili pale aliposema Upo?
Na B alikua anajibu kuwepa kwa kifaa hicho pale aliposema kuwa Upo''
 
Naelewa kuwa A. Aliposema upo' upo? Upo ya kwanza ni kifaa fulani ambacho anakiulizia kwa neno lake la pili pale aliposema Upo?
Na B alikua anajibu kuwepa kwa kifaa hicho pale aliposema kuwa Upo''
uko sawa mkuu,"UPO"ni kitu chochote ambacho hutumiwa na vyombo vya baharini ukiachilia mbali meli na boti za kisasa,ambacho hutumika kutolea maji yaliyo ndani ya ama mtumbwi,dau au ngalawa na kuyamwaga nje.
 
Back
Top Bottom