Kiswahili kimezidi mno kuelemea kwenye Kiarabu zaidi ya Kibantu. Je, upendeleo wa Uarabu dhidi ya Ubantu?

Umesoma Tanzania? Kama umesoma Tanzania elimu ya msingi na ya upili huwezi kuacha kujua maneno haya. Labda uwe unaidharau lugha ya Kiswahili kiasi kwamba hutaki kuwa makini nayo.

Kwako wewe uliyesoma Tanzania msingi, upili na mwenyeuwezo wa kung'amua mapenzi na kiwango cha thawabu nilichonacho juu ya Kiswahili; naomba mchango wako kwenye hoja niliyoweka ya Kiswahili kuelemea kwenye Kiarabu zaidi ya Kibantu. Ahsante.
 
Kabla sijatoa mchango wangu, nini maana ya maneno mstakabali, nakili na kimfano.
 
Je, nikiyajibu na kutofautiana na kile unachotarajia kukisikia bado hakutakuwa ulimbukeni au saratani iliyoenea?!

Sasa badala ya kujibu swali unauliza swali.

Kama nia yako mada yako kujadiliwa, iweke sawa, huo ulimbukeni na saratani kama vimeenea ni wewe ndio unajibu; mimi sina haja ya kujua. Shida yangu ni kujua ulikuwa unamaanisha nini kwa maneno nakili, mstakabali, kimfano kabla sijaendelea kuchangia changu kidogo?
 
Si hivyo tu, bali shida yako yawezekana pia kutojua ulimbukeni ni nini na matumizi yake yanafaa wapi.
 
Si hivyo tu, bali shida yako yawezekana pia kutojua ulimbukeni ni nini na matumizi yake yanafaa wapi.

Sina shida na kujua maana ya ulimbukeni, matumizi yake na mahali hayo matumizi yanapofaa kama unavyotaka kushinikiza hapa.

Unaweza niambia nisichangie mada yako kwani huna haja na mchango wangu (ingawa huu umeainishwa hapa kama mjadala hai, 'live topic'.
 
Samahani, sina nguvu hiyo.
 
Kabla sijatoa mchango wangu, nini maana ya maneno mstakabali, nakili na kimfano.

Ameshasema kiswahili kinampiga chenga, atatumia kiingereza pale atakaposhindwa. Sasa wamlazimisha?

"Seriously, I think there is an over-arabization of Kiswahili from its conception to this day."

Hicho cha wazungu hapo juu amesema amejaribu kutumia kiswahili kashindwa!

Nadhani aweza kuwa ni mwenyeji wa sehemu za ndani ndani za Tanzania ambako wanaongea kiingereza!
 
...si hivyo tu Kuhani, bali pia yawezekana ametokea sehemu za ndani ndani za Tanzania ambako kuna nyoka wa aina hii wanaoshindana nafsi:
two_headed_snake_by_slug45.jpg
.... na amepata ujuzi wa kuwaua nyoka hao pale wanapoandamana kumng'ata. Siku akishindwa kabisa kabisa anaishia kuwakata mikia tu!!!
 
... na amepata ujuzi wa kuwaua nyoka hao pale wanapoandamana kumng'ata. Siku akishindwa kabisa kabisa anaishia kuwakata mikia tu!!!

Kingine, SteveD, inawezekana ana uwezo wa kukata mikia ya wachangiaji kwa vile, kama huyo nyoka wa nafsi mbili, yeye nae ni reptilia anaejibadilisha rangi kutokana na kazi anaoingia kuifanya jamvini siku hiyo.

mellers-chameleon.jpg
 
Pole sana Steve...naona jamaa anakuona wewe kibonde ndo maana anapenda sana kukuonea. Yaani chochote utakachoandika jamaa lazima atafute kasoro, hata iwe kwa kulazimisha.Aisee naona unahitaji ile kitu yetu aisee (substance).

But I like your style, though. You take adversity all in your stride and remain cool, calm, and collected.

Ingekuwa mimi tayari ningekuwa nshapewa server ban...

BTW, Ile kitu bado haijawasili.
 
Last edited:
Pole sana Steve...naona jamaa anakuona wewe kibonde ndo maana anapenda sana kukuonea. Yaani chochote utakachoandika jamaa lazima atafute kasoro, hata iwe kwa kulazimisha.Aisee naona unahitaji ile kitu yetu aisee (substance).

But I like your style, though. You take adversity all in your stride and remain cool, calm, collected.

Ingekuwa mimi tayari ningekuwa nshapewa server ban...Lol

BTW, Ile kitu bado haijawasili.

Dawg, you know what, yule atumiaye elimu na exposure yake kwa lengo la kunyanyasa ni worse than the one without hiyo elimu. And i think you remember my kind of resolve to this kind of issues... I'm the kind of guy who will never use ones' weakness to fight back my case, I'll only deal with their strengths and core values.
-------------------------

Ile kitu natumaini itawasili, kuwa na subira tu ng'wanangwa! cupcake ataipenda ikiwasili:)
 
Way to go hommie....
 
Husikonde Mkuu tupo pamoja...! Maisha hayana raha bila kuwa na vikwazo vya hapa na pale.

Mkuu XP hiyo herufi H si pahala pake hapo kwani neno usikonde ile si tayari imeshabeba ukanushi wa ukonde.

Ama kuhusu kiarabu kuchukuwa nafasi kubwa katika kiswahili ni hali halisi ya mazingira na wakati, katika kipindi cha kukua kwa kiswahili ukanda wa pwani ya Afrika mashariki ni kipindi cha wafanya biashara wengi toka bara Arabu na bara Hindi na katika kipindi hicho maandishi yaliyokuwa maarufu kwa wafanyabiashara hao ni kiarabu, hivyo wajuzi wa kiarabu ndio waliokuwa wakiandika mambo yote ya biashara na mikataba yake kwa maandishi ya kiarabu.

Na ni kawaida kwa mwandishi kutumia lugha yake kuelezea jambo pale anapokosa neno la lugha husika hivyo maneno mengi ya kiarabu yalitumbukia katika kiswahili na kujijenga, na hata mfumo wenyewe wa lugha ukawa na athari za kumfumo toka kiarabu.

Jingine ambalo watu wengi hawapendi kulikubali ni kuwa Waarabu walijiingiza zaidi kwa wenyeji kuliko wageni wengine waliokuja Afrika Mashariki nasema hili wengine hawalipendi kwa sababu wamelishwa kasumba mbaya kwamba waarabu waliwatesa babu zetu na kuwapeleka utumwani. nakubali kuna ukweli kiasi ndani ya propaganda hiyo ila imetiwa chumvi ili kuleta ladha.

Mwarabu hakujibagua na mwenyeji bali alijichanganya na kuowana na kuzaliana na wenyeji zaidi kuliko wageni wengine hivyo ilkuwa rahisi kwake kutumia lugha yake sambamba na lugha ya wenyeji.
 
Kama ni hivyo, basi kuna favourism vilevile ya Ubantu dhidi ya sisi wengine ambao ni Non-Bantus. .. Na hii ni mabaya zaidi. Kiswahili hakina maneno yanayotoka ktk Non-Bantu languages kama Kimasai, Kimang'ati, Kijaluo, Kisandawi, n.k.

Wachawi wajichanganye nw wanaotumia Kiswahili na baadae kuleta kitu au dhana MPYA isiyokuwepo ndani ya Kiswahili. Sifa ya Kiswahili ni kupokea dhana mpya kwa lugha ya mtowa dhana mpya na kuitia ndani ya Kiswahili. Upo mpango maalum unaokubalika kusarifu lugha ya kigeni na kuingizwa kwenye Kiswahili.

Hii sababu ya dhana mpya ndiyo iliyosababisha Kiswahili kiwe na maneno mengi ya Kiarabu. Kama tulivyokwisha juulishwa na wengi kuwa Waarabu walikuwa na wakati mwingi kuleta dhana zao kuliko lugha nyengine ,na hapo zilipoingia lugha nyengine katika jamii inayotumia lugha ya Kiswahilitayari mambo na dhana nyingi za kidunia.

zilikwishatiwa kwenye Kiswahili kupitia Kiarabu. Lugha kama Kiingereza kilpokuja kilpingana na taathira za Kiarabu lakini tayari lugha ya Kiswahili ilishajenga maneno yake kwa kupitia Kiarabu hivyo haikuwa rahisi kuondowa taathira hiyo bila ya kuondowa Kiswahili chenyewe.

Lugha za Kihaya, Kisukuma, Kimasai na nyengine za Tanzania zilikutana na Kiswahili hivi karibuni tu na tayari Kiswahili kiko mbali kwa tabia yake ya kuiba maneno ya lugha nyengine. Kuingizwa kwa maneno mapya huja pale tu panapokuwa na sababu yaani pana dhana mpya na Wamasai, Wasukuma, Wahaya na makabila mengine si wazuri katika kuvumbua vitu vipya vitakavypleta maneno mapya ya kukifanya kiswahili kiyatie ndani ya lugha yao.

Tukubali kuwa Hayo maneno ya Kiarabu yaliyomo yamepitia mfumo wa kawaida wa KIswahili katika kumeza maneno kiasi kwamba hat Waarabu wenyewe wapata tabu kuelewa maneno hayo kuwa ni maneno ya Kiarabu kiasili. Pia tukubali kuwa athari ya maneno ya Kiarabu imekwisha sasa kwa vile wanaoleta dhana mpya sasa ni Wzungu na Wachina hivyo kwa tabia yake Kiswahili kitabeba maneno hayo na tone mifano ya maneno friji, televisheni, kompyuta na mengineyo,ambayo juu ya kuyalazimisha kuitwa jokfu, Runinga, na mengineyo wengi wa waswahili wataendelea kuviita kwa dhana ya muundaji kwani ni tabia ya Kiswahili kupokea dhana mpya kwa nama aliyeileta alivyofanya. Kiswahili si lugha ya kulazimishwa bali ni lugha inayokuwa yenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom