Kiswahili kimeficha mengi

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,897
4,620
Kuna rafiki yangu mtu wa nchi jirani niliyekuwa nazungumza nae juu ya mambo fulani fulani yanayohusu utawala wetu. Mtu huyu hajui kiswahili na kwa kweli alisema anaona watanzania wakiwa na malalamishi dhidi ya serikali yao lakini hajui wanachokilalamikia kimejengwa juu ya msingi wa nini.

Nimejaribu kumweleza wanacholalamikia ni wizi unaofanywa na serikali kupitia kwa wale wenye dhamana ya uongozi na kilichofunua zaidi huu wizi ni report ya CAG. Alipoona kinacholalamikiwa ameshangaa ni kwa nini sheria haichukui mkondo wake? Maana aliendelea kudai kama ingelikuwa ni kwao wala usingelisikia malalamishi bali ungeliona vitendo.

Wazo lilinijia pale pale ikiwa mabalozi wanowakilisha nchi zao nchini na wanchi fadhili wana ufahamu na kile kilicho katika taarifa ya CAG na report za kamati za bunge.

Rai yangu kwa makamanda wapambanaji hasa Chadema tunaomba mfanye mpango wa kuzichapisha ripoti za CAG na za kamati za bunge zinazoonyesha jinsi nchi inavyoliwa, kwa lugha ya kiingereza na nakala ziwafikie mabalozi wate wa nje na nchi wahisani. Sii ajabu nao hawana ufahamu wa kile watanzania wanacholalamikia kwa sababu tu ya lugha yetu kiswahili. Nawakilisha.
 
Back
Top Bottom