Kiswahili chaharibiwa

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Mie najivunia sana lugha ya kiswahili. Ni lugha yenye sarufi ya uhakika (ingawa ngumu) na ndo lugha iliyosaidia kujenga umoja wa watanzania.

Lakini kwa bahati mbaya sana hivi karibuni umeibuka mtindo wa utumiaji mbaya wa lugha hii. Na kibaya zaidi wanaoongoza katika utumiaji mbaya ni watangazaji kwenye vyombo vya habari tv na radio. Lipo tatizo la matumizi mabovu ya neno "kuweza" Hili neno lina maana yake maalumu lakini linatumiwa ovyoovyo tu. Kwa mfano utamsikia mtangazaji wa kipindi cha michezo kwenye radio akisema: Timu A iliweza kufungwa mabao mawili na timu B. Au kwenye habari za mafuriko ya Dar nilisikia: Watu wanane waliweza kufariki. Yote haya ni matumizi mabaya sana ya neno "kuweza" Matumizi haya yameenea sana kiasi kwamba utafikiri watu wanaogopa kupata ugonjwa fulani wasipotumia neno kuweza kwenye mazungumzo yao. Rais aliweza kuhutubia wananchi kupitia wazee wa daressalamu, Mto Msimbazi uliweza kufurika na kumwaga maji eneo la Jangwani. Kaa tayari ili uweze kusikia taarifa ya habari.Waungwana wa Jf mwaonaje? Kuna ukweli kwenye hili?
 
Back
Top Bottom