Kiswahili chafa

tabibumtaratibu

JF-Expert Member
May 29, 2011
2,405
1,181
Jaman watumiaji wa kiswahili mmeliona hili?Ngoja niwaoneshe "kuna maneno kede wa kede ya kiswahili yamepoteza hadhi yake ya kawaida na kuvikwa hadhi ya matusi,mfano maneno kama;kuliwa,kupakuliwa,kupigwa,kugeuzwa,kubanduliwa na kadhalika"jaman mbona twakitia ukakasi wa maana kiswahili chetu?Tuacheni tabia hii sio nzuri katika kaumu.
 
Kama serikali yenyewe ilosema iwe lugha ya taifa imeshindwa kukiendeleza unadhani wananchi watakuwa je? Mfano katiba na sheria zetu zimeandikwa kwa lugha ya kingereza hapo utasema serikali inakithamini? Mashule mengine hapa tz ukiongea kiswahili ni adhabu kili utapewa pia mashuleni karibia masomo yote yanafundishwa kwa lugha ya kingereza je hapo kweli tunaithamini lugha yetu?
 
Mimi sidhani kama ni tatizo maana hayo maneno hutafasiriwa tofauti tofauti kutokana na mada na mahali husika!Still unaweza kutamka kubanduliwa kwa maana yake halisi mahala fulani isiwe shida!Mkuu usipate shida na maneno ya vijana mitaani!!
 
haya bwana yakhe me langu sikio 2 kusikiliza
 
Jaman watumiaji wa kiswahili mmeliona hili?Ngoja niwaoneshe "kuna maneno kede wa kede ya kiswahili yamepoteza hadhi yake ya kawaida na kuvikwa hadhi ya matusi,mfano maneno kama;kuliwa,kupakuliwa,kupigwa,kugeuzwa,kubanduliwa na kadhalika"jaman mbona twakitia ukakasi wa maana kiswahili chetu?Tuacheni tabia hii sio nzuri katika kaumu.

lugha ya kiswahili ni tata
 
Kiswahili lugha ya makabwela!tunaipa bendera ya taifa heshima inapopandishwa/kushushwa halafu shuleni utaambiwa kuna 'english speaking policy' ukiongea kiswahili unabebeshwa bango linakokudhalilisha!tuna nia ya kukiendeleza kiswahili?kama hatukiheshimu kiswahili(mf shule nyingi za sek) hakuna umuhimu wa kuiheshimu bendera ya taifa!TUUZE NCHI kila m2 apewe chake aangalie atafanya nn!"kingereza lugha ya sayansi" mwasemaje!
 
Kama tutatilia mkazo matumizi ya kiswahili fasaha hasa ktk shule na vyuo,hakutatoke uharibifu wa lugha 'english speaking policy' kwa anayetaka! Hapo kisw. Hakitaonekana kama lugha ya makabwela,na kitazungumzwa kwa ufasaha.
 
Back
Top Bottom