andalwisye
New Member
- Apr 11, 2012
- 1
- 0
Hodi wana jamvi! Nina tatizo nahitaji msaada wa maoni na ushauri wa kitaalamu au uzoefu, mzee wangu ana tatizo la kisukari kwa muda sasa lakini hivi karibuni limejitokeza tatizo lingine la mtoto wa jicho ambapo hawezi kuona kabisa. Baada ya kutafiti matibabu yake inaonekana anahitajika kufanyiwa upasuaji mdogo ili kuondoa mtoto wa jicho. Napenda kufahamu ni Hospitali gani nzuri kwa matibabu hayo kwa Dar es Salaam na je upasuaji mdogo hauwezi kuwa na madhara zaidi kwa mgojwa wa kisukari?