Kisiwa hatarini kutoweka Zanzibar-Habari Leo

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
[h=3]Kisiwa hatarini kutoweka Zanzibar-Habari Leo[/h]
KISIWA Panza kilichopo Mkanyageni mkoani Pemba chenye wakazi 600 kiko hatarini kutoweka kutokana na kumezwa na bahari.

Hali hiyo inatokana na mabadiliko makubwa ya tabia nchi yanayosababisha kina cha bahari kuongezeka na hivyo kasi ya mawimbi ya bahari kushambulia maeneo ya fukwe za kisiwa hicho.

Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Sheha Mjaja Juma, jana alithibitisha kuwapo kwa hali mbaya ya mazingira katika kisiwa hicho.

Akifafanua, alisema mabadiliko hayo ya tabia tayari yamesababisha athari katika jamii baada ya mawimbi hayo kufukua makaburi ya watu waliozikwa zaidi ya miaka 50 iliyopita.

“Kisiwa Panza kilichoko Pemba kimeanza kupata athari kubwa za mabadiliko ya tabia nchi kutokana na kasi ya mawimbi ya bahari kuvamia maeneo ya fukwe na kufukua makaburi,” alisema Mjaja.

Athari nyingine kwa mujibu wa Mjaja ni baadhi ya sehemu ya maji ya bahari kuingia kwenye makazi ya wananchi zaidi wakati bahari inapochafuka.

Mjaja alisema tayari Idara ya Mazingira imetoa taarifa kwa Serikali kuhusu kuwapo athari hizo ambapo tathmini zinaonesha kwamba kisiwa hicho ni miongoni mwa visiwa vilivyo hatarini kutoweka kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema juhudi na mikakati ya makusudi inahitajika kuokoa kisiwa hicho kutokana na tishio la kutoweka, kutokana na kasi ya mawimbi ya baharini kushambulia baadhi ya maeneo.

Wakazi wa kisiwa Panza ni wavuvi na kutokana na hofu ya bahari kuvamia kisiwa hicho baadhi ya wananchi wameanza kukihama.

Hivi karibuni wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanaoshughulikia mradi wa mabadiliko ya tabianchi wakati wakizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika semina kuhusu mabadiliko ya tabianchi, waliitaja Panza kuwa hatarini kutoweka kutokana na kasi ya bahari kuvamia nchi kavu.

Kisiwani Pemba kuna zaidi ya visiwa vidogo 15 ambavyo vinakaliwa na watu kikiwamo cha Kojani ambacho wananchi wake wengi ni wavuvi, huku visiwa vingine 10 vikiwa havikaliwi na watu na vinatumika kwa uvuvi na utalii kikiwamo cha Misali.
 
Watakoma!
Ngoja tuvunje Muungano wabaki hukohuko wakifunikwa na maji, hakuna kukimbilia huku.
 
Watakoma!
Ngoja tuvunje Muungano wabaki hukohuko wakifunikwa na maji, hakuna kukimbilia huku.
 
Na Zanzibar lilivyo chini ya Usawa wa Bahari kitamezwa pia unajua tena El-Nino... Watu naona watakimbilia Oman? Unajua Oman hawapendi rangi Nyeusi
 
Kwani dunia imejaa na watakakokimbilia patatita? wataenda kisiwa cha pemba au Oman, Iran, Syria, Mogadishu, Afghanistan, Pakistan au Nigeria Kaskazini
 
tutakimbilia egypt ama palestina

waarabu hawapendi ngozi nyeusi, walikuwa wanabaguliwa sana wakati wa utawala wa kiarabu, ndio maana karume mkubwa alivyochukua madaraka aliwafukuza waarabu, kutaifisha mali zao na kulazimisha kuoa waarabu kwa lazima.
 
ukitaka upate maoni ya JK kuhusu kisiwa hicho, yumkini utasikia akisema "huo ni Upepo tu utapita"

Bora mimi nina Aquaphobia. Ntakaa bara tu, huwezi nishawishi niishi ufukweni.
Tsunami zenyewe ndo hizo. Zina beep kila uchao!
 
Kumbe maombi yangu yamefika mbinguni, sasa nina-focus Unguja na Pemba. Naamini nikiendelea kufunga mpk mwezi wa kumi wa mwaka 2019 hakutakuwa na kitu kinaitwa Zanzibar kwenye uso wa dunia. Tunzeni picha na kumbukumbu mlizonazo
 
waarabu hawapendi ngozi nyeusi, walikuwa wanabaguliwa sana wakati wa utawala wa kiarabu, ndio maana karume mkubwa alivyochukua madaraka aliwafukuza waarabu, kutaifisha mali zao na kulazimisha kuoa waarabu kwa lazima.

Kama ni hivyo mkuu, mbona hawa wa sasa wanajipendekeza sana kwa waarabu kiasi wanataka muungano uvunjike ili wao wawe chini ya utawala wa waarabu ili wapate tende bure?
 
Back
Top Bottom