Kisingizio: Daftari la Wapiga Kura, vyombo vya dola. Sababu?

Mwanakijiji tukiangalia kwa jicho tafauti unaonaje kama tukijumlisha kura zote kata zote halafu tuone nani alipata kura nyingi??inaweza kuwa tathmini nzuri ya 2015?
 
MMK!! Uongozi wa juu wa chama ulikufanyia nini!!!?

Nalazimika kuuliza hivi maana walalama hata pale ambapo sababu ziko wazi na unazielewa!! Namshukuru Mungu plan yako yako ya Arumelu ilikosa mafanikio, kama ingefaulu na ikaja hii ya jana, bila shaka leo ungehamasisha maandamano!!

Niliwahi kukwambia humu kwamba wewe na mgombea wako aliejitenga naM4C mna mbinu chafu dhidi ya ukombozi, nadhani wakumbuka!! Leo umepata pa kuanzia ba umedhihirisha niliyoyasema!

MMK, nategemea mtu kama wewe uje na "tufanye hivi" kusongesha ukombozi(mtazamo chanya, na ujengaji chama). Lakini mwenzangu unaleta "tufanye hivi" (mtazamo hasi) ili chama kibomoke!!

Nakuuliza tena MMK, mtafaidika vipi CDM ikifa na sisi walala hoi tukaendelea kukandamizwa!!? Jisikieni aibu jamani aaah!!
 
Ina maana hawa waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu huwa hawa shawishiki kupigia kura upinzani?Mpaka wapatikane wapika kura wapya?
Kwa maaana hiyo Chadema katika movement zake imeshindwa kushawishi wapiga kura waliopo sasa kukipa kura?Wameweza kata 3?Harakati na operaion kibao za miaka miwili wamefanikiwa kata 3 mpya?Je miaka 3 ijayo mpaka kufikia uchaguzi ujao kata ngapi zitaongezeka?Ubunge je?Urais?
Ikumbukwe walizungusha makamanda wao wote kwenye maeneo yote yaliofanyika uchaguzi!Dr.Slaa na viongozi wote !
Chadema watulie wajipange,wajitulize kusonga mbele!

labda ungeeleza "wajipange" ndio nini, wameongeza hizo kata 3 kutoka kwa wapigakura wale wale walioichagua ccm uchaguzi kabla ya huu. margin ya ushindi wa ccm imezidi kupungua sana (naongelea idadi ya wapiga kura waliowaunga mkono) ina maana mabalozi wa chadema wanaongezeka day come day go,
lazima, nasema tena lazima tuwapongeze wananchi kwa kutekeleza demokrasia katika mazingira magumu sana na kuonyesha kuwa ni kweli wao ndio wenye nguvu.
hushangai ccm inatumia mpaka majambazi sugu ku-terrorise voters na polisi wamebung'aa tu.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ngonini mbona Bawacha ilishakufa siku nyingi tu? Chadema wana Bavicha tu.

Na kwa kina mama ndipo ccm inapojipatia ushindi wa kutakata. Mahali ambapo wapiga kura wengi ni akina mama hasa maeneo ya vijijini ndipo ccm wamekuwa wakifanikiwa sana kuwarubuni kwa chumvi, sukari, khanga na scarf.

Bawacha wana deni kubwa sana kwa watanzania juu ya wajibu wao wa kuwakomboa akina mama wa kitanzania toka katika minyororo ya utumwa wa ccm.
 
Ina maana hawa waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu huwa hawa shawishiki kupigia kura upinzani?Mpaka wapatikane wapika kura wapya?
Kwa maaana hiyo Chadema katika movement zake imeshindwa kushawishi wapiga kura waliopo sasa kukipa kura?Wameweza kata 3?Harakati na operaion kibao za miaka miwili wamefanikiwa kata 3 mpya?Je miaka 3 ijayo mpaka kufikia uchaguzi ujao kata ngapi zitaongezeka?Ubunge je?Urais?
Ikumbukwe walizungusha makamanda wao wote kwenye maeneo yote yaliofanyika uchaguzi!Dr.Slaa na viongozi wote !
Chadema watulie wajipange,wajitulize kusonga mbele!
I see!!..... wewe ni bonge la Analyst na ni kweli ni Tanzanite Member, nilikuwa sijui kwamba Joshua Nasari ni mbunge wa CUF na Jeremia Sumari alikuwa Mbunge wa Chadema baada ya kifo chake Chadema ikanyanganywa jimbo. Good Analyst.
 
Tatizo nimoja tu,Kuwa ccm awataki kuandikishwa wapiga kura wapya au kuboresha daftari la wapiga kura kila uchaguzi uanapofika.Hii imekuwa njia potofu ya ccm wanayotumia kushinda.
AMINI USIAMINI SIKU DAFTARI LA WAPIGA KULA LIKIBOLESHWA NA UCHANGUZI KUFANYIKA WATU AWATAAMINI MATOKEO.
Vijana wengi wanaojitokeza kwenye mikutano ya vyama vya siasa awajajiandikisha.
 
MMK, wakati unaandaa mwendelezo naomba haya:-

(a) CDM 2010 walipata kiasi gani cha kura ktk kata zote(29) za jana na pia uchaguzi huu wamepata kiasi gani.

(b) Idadi ya wapiga kula(ktk kata husika) 2010 na 2012, kwanini wameongezeka ama wamepungua.

(c) Tupe maoni yako binafsi kwamba, ikiwa daftari la wapiga kura lingeboreshwa matokeo yangekuwaje na sababu pia.

Let say tuwawajibishe viongozi wa juu kwa kuwatimua(napendekeza hivo), tupe mapendekezo yako ni nani awe nani.
 
Hivi watu humu ndani tumeshawahi kufanya tathimini kuona wabunge wengi wa CHADEMA wametoka mijini au vijijini!? Kwa taarifa yenu CHADEMA inashinda sana vijijini kuliko mijini, tatizo kubwa ambalo watu wengine wameliongelea na hapa namnukuu Matola kwamba wananchi hasa wa vijijini huchagua mtu anayewafaaa na wanayemjua mambo ya chama huja baadaye!!
 
Last edited by a moderator:
MMK, wakati unaandaa mwendelezo naomba haya:-

(a) CDM 2010 walipata kiasi gani cha kura ktk kata zote(29) za jana na pia uchaguzi huu wamepata kiasi gani.

(b) Idadi ya wapiga kula(ktk kata husika) 2010 na 2012, kwanini wameongezeka ama wamepungua.

(c) Tupe maoni yako binafsi kwamba, ikiwa daftari la wapiga kura lingeboreshwa matokeo yangekuwaje na sababu pia.

Let say tuwawajibishe viongozi wa juu kwa kuwatimua(napendekeza hivo), tupe mapendekezo yako ni nani awe nani.


Mkuu wa hesabu zako bado ujaonyesha ukweli.
KABLA ya uchaguzi
CCM ilikuwa inatetea kata 27 ni sawa na 93%
CDM ilikuwa inatetea kata 2 ni sawa na 7%
BAADA YA UCHAGUZI
CCM wamepata kata 23 ni sawa 79%
CDM wamepata kata 5 ni sawa 17%
TLP wamepata kata 1 ni sawa 3%


Je ni nani kapanda na kushuka?
 
Nguvu ya Umma ya Chadema ipo wapi.

KABLA ya uchaguzi
CCM ilikuwa inatetea kata 27 ni sawa na 93%
CDM ilikuwa inatetea kata 2 ni sawa na 7%
BAADA YA UCHAGUZI
CCM wamepata kata 23 ni sawa 79%
CDM wamepata kata 5 ni sawa 17%
TLP wamepata kata 1 ni sawa 3%


Je ni nani kapanda na kushuka?
 
Wakati watu walipotoa ushauri na kuhoji usafi wa Mgombea wa CHADEMA kata ya Mawanza na jinsi baba yake alivyomnadi hadharani kwamba ni Mwizi, kuna wanazi wa CHADEMA humu ndani walituona hamnazo. Lakini hebu tuwe wakweli kama baba mzazi wa mtu anasema hadharani kwamba mwanawe ni mwizi wewe mtu baki unaweza kweli kumsafisha!?

Mimi tatizo ninaloliona ni kwa CHADEMA kudhani kwamba viongozi wa kitaifa wanaouwezo wa kubadili upepo kila mahali. Hoja hapa ni kuanza kufuatilia kwa karibu aina ya wagombea na sifa zao na kusimamia mchakato mzima wa upatikanaji wa wagombea hao!!
 
Mzee Mwanakijiji

Mkuu,

Tathimini yako na wengine kwa haraka haraka ni rahisi kukurupuka kuwa Chadema kimeshindwa...

Hatuna sababu ya kuwa wakali wala kutafuta sababu, uzuri wanachadema tunazijua sababu,


Kwa hili ungewashauri CCM, wajitadhimini na waje na sababu kwa nini wanazidi kuporomoka...uchaguzi huu wamepoteza viti 3 vya udiwani...Chadema tumeongeza, sasa sijui nani aje na hizo sababu...

Mkuu MMK, kama Tanzania tungekuwa na Democrasia ya Kweli...Nami ningeungana nawe, kuwakosoa na kuwaponda viongozi wetu, lakini kwa jinsi uwanja wa demokrasia ulivyo, CDM wamejitahidi sana,, nikuulize kidogo tu...
1. Unafahamu kuna kesi ngapi zinazowakabili viongozi wakuu wa CDM mpaka sasa?
2. Kesi ngapi kwa mashabiki na wapenz wa Cdm mpaka sasa?
3.Kuna mashabiki wangapi wa CDM wamekufa mpaka sasa?
4.Kuna walemavu, wagonjwa, walioteswa wa CDM mpaka sasa?

MzeeMwanakijiji, Tanzania ni zaidi ya ujiavyoo..., Chadema tunawapongeza sana tena sana, endeleeni viongozi wetu tupo nyuma yenu.

Usitazame kuongezeka viti 3, ila tazama input ya rasilimali iliyowekwa kwenye hizi chaguzi hailingani na output yake, out put ya 5 ni ndogo sana ukilinganisha na msuli ulio wekezwa
 
Mzee Mwanakijiji, naingana na wewe kwa asilimia 100%, naleta kuni za kuchochea moto, hawa Chadema tuwapitishe kwenye tanuru la moto mkali kabisa ili wakitoka ni chuma cha pua na wale watakaoshindwa, yatatoka majivu!. Hakuna tena kuwaonea huruma Chadema ni kuwatembezea bakora kwa kwenda mbele, vingenevyo 2015 itakuwa ni kilio tena!.

Kwa wengine wetu humu Chadema ni chama kitukufu na mambo yake yote kwao ni utukufu na utakatifu!, kwao kukikosoa Chadema ni dhambi!. Hawa kazi yao ni kukiimbia nyimbo za sifa na utukufu na mapambio!.

Kuna wengine wetu humu, Chadema kinaheshimiwa sana kama Mzazi, kama Baba, hata kikikosea, hakiambiwi, kukikosoa itaonekana ni utovu wa nidhamu!. Hawa wanayaona mapungufu ya Chadema ila kufuatia kukiheshimu, wanajinyamazia tuu!.

Na kuna sisi wengine wetu wa Mwanakijiji type, kwetu Chadema ni chama tuu, tunakiona kiko kama mtoto, kinazaliwa, kinalelewa, kinakuwa, hivyo ni kama mtoto tuu, akibioronga, anabalazwa!, tena kadri ya ukubwa wa kosa ndio wingi wa bakora. We don't "spare the rod and spoil the child!", ni kutembeza tuu bakora za nguvu mpaka mtoto huyu anyooke na kuenenda katika mstari wa kuelekea ikulu 2015!.

Mimi nimewaambia mengi na kila siku huwa ninabezwa, kubwa kuliko yote nimewaambia Chadema hawajipanga!, ili wajipange ni lazima wakubali kubadilika!. Lazima watambue target yao ni nani?, lazima wawape wananchi solid reasons za kuichagua Chadema 2015!, mtaji wa Chadema kuwategemea wanaionga mkono kwa matumaini kufuatia kuichoka CCM, haitaipeleka Chadema Ikulu 2015 na hata CCM ikiwasimamisha "pace makers" wangu EL au Membe, Chadema itapigwa mwereka wa nguvu na Ikulu itabakia kuisikia tuu kwenye bomba!.

Siku zote nasema humu, 2015 its do or die for both CCM & Chadema!.

Pasco.
 
M4C ndio imezaa kata 3 kweli kazi mnayo.
Go extra mile, ulize, hizo kata zingine ambazo CCM wameshinda, Je! ni kwa Tofauti ya Ngapi? pia Linganisha na 2010, ndio uje na Tathimini ya M4C...Siyo kubwabwaja bwabaja tu bila figure!
 

KABLA ya uchaguzi
CCM ilikuwa inatetea kata 27 ni sawa na 93%
CDM ilikuwa inatetea kata 2 ni sawa na 7%
BAADA YA UCHAGUZI
CCM wamepata kata 23 ni sawa 79%
CDM wamepata kata 5 ni sawa 17%
TLP wamepata kata 1 ni sawa 3%


Je ni nani kapanda na kushuka?

Mkuu naona unafunguka kama Dr Benson Bana.
 

KABLA ya uchaguzi
CCM ilikuwa inatetea kata 27 ni sawa na 93%
CDM ilikuwa inatetea kata 2 ni sawa na 7%
BAADA YA UCHAGUZI
CCM wamepata kata 23 ni sawa 79%
CDM wamepata kata 5 ni sawa 17%
TLP wamepata kata 1 ni sawa 3%


Je ni nani kapanda na kushuka?

Kwa jinsi cdm inavyo pambwa humu jamvini ilionekana ingechukua viti zaidi ya nusu, ila vi5 tu kweli cdm na input mliyoweka mmepata hivyo tu? cdm bado kukubalika kwa wananchi huo ndio ukweli
 
Back
Top Bottom