Kisiasa na kimaendeleo: Nini hulka ya Mtanzania

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Uvivu? Woga? Unafiki? Undumilakuwili? Nidhamu ya woga? Kujipendekeza kwa wakubwa? Kujifanya ni mahodari wa kusahau shida kuigiza tunaipenda amani sana kuliko maisha yetu na vizazi vyetu? Kufanya vitu kwa kuogopa flani atakasirika au kufurahi sana hivyo kuhujumu rasilimali za nchi ili kumridhisha?

Au ni kweli tunaipenda nchi yetu na amani tuliyonayo bila kujali maisha yetuna mustakabali wa nchi na vizazi vyetu hivyo tuko tayari kuifia amani bilakujali maisha tunayoishi hata kama niyadhiki kiasigani.

Nini hulka yetu watanzania maana hatueleweki tunataka nini na kwa wakati gani?

Maana tukotuko tu bora liende.
 
Unawasema Madaktari walio jipendekeza kwa kikwete kumba msamaa ile hali madai yao ya msingi hayajatekelezwa hata moja. Na wala huduma mahospitalini hazijaboreshwa.
 
MR. ABLE;4659810]Unawasema Madaktari walio jipendekeza kwa kikwete kumba msamaa ile hali madai yao ya msingi hayajatekelezwa hata moja. Na wala huduma mahospitalini hazijaboreshwa.

PAMOJA NA WENGINE
 
We need to build a "Positive National Attitude". Otherwise, we are undefined and easily divided!!!
 
kamawewe si ntanzania klichokusukuma ukafungua huu uzi ni nini,hilo swali la pili sikujibu maana si hadhi yangu

Hujajibu swali.

JF kuna watu wa mataifa mbalimbali wanakuja, kuna mpaka forums za Wakenya. Hakuna sehemu inayoshurutisha mtu kuwa Mtanzania ili ufungue thread.

Unajionyesha unaenda kwa assumptions zaidi bila uhakika.

Bado hujanijibu swali langu, umejuaje kama mimi Mtanzania?

Na kabla ya kuanza kujadili hulka ya Mtanzania, kwanza lazima ujue mipaka ya unachokiongelea iko wapi, na Mtanzania ni mtu gani.

Wewe hujaweza kum define Mtanzania, utawezaje kuongelea hulka yake?
 
Hujajibu swali.

Bado hujanijibu swali langu, umejuaje kama mimi Mtanzania?

Na kabla ya kuanza kujadili hulka ya Mtanzania, kwanza lazima ujue mipaka ya unachokiongelea iko wapi, na Mtanzania ni mtu gani.

Kiranga, wewe unaonekana ni mtanzania halisi. Longo longo yako ni kubwa. Maneno mengi.

Hii ni hulka ya watanzania na hata dugu zetu za Kenya zinaelewa hili. Huwezi shinda mtanzania kwa maneno.

Hii ni maana ya mtanzania ya mtaani, maana ya kisheria au kiuhamiaji wengine watadadavua.
 
Kiranga, wewe unaonekana ni mtanzania halisi. Longo longo yako ni kubwa. Maneno mengi.

Hii ni hulka ya watanzania na hata dugu zetu za Kenya zinaelewa hili. Huwezi shinda mtanzania kwa maneno.

Hii ni maana ya mtanzania ya mtaani, maana ya kisheria au kiuhamiaji wengine watadadavua.

Hujajibu maswali, Mtanzania ni mtu gani? Definition please.

Bill Clinton ana longolongo kushinda watanzania kibao, mpaka anatwist what is the definition of is.Kapigwa BJ White House watu tukafikiri atakuwa impeached na kujifungia maisha yake yote yaliyobaki.

Na mtu sio tu kabounce back kwa sababu mdomo mali yake, ila mpaka kesho anapata standing ovations.

Na yeye Mtanzania?

Sio mnataka kujiingiza katika maswala makubwa eti hulka ya Mtanzania wakati simple defnitions tu kazi.
 
kwanza nianze kwa kusema kuwa kujifunza ni jambo lisilo na mipaka na wanasema kujifunza kunaanza na kufikiri maana usipo fikiri unanuka..... maana ya neno hulka hubebwa dhana ya tabia ama mazoea ya mtu kuelekea jambo Fulani sasa kwa msingi huo muuliza swali amejikita kutaka kufahamu upi utamaduni wa watanzania kuelekea mambo hayo aliyo yataja kama , kulinda amani , kuwasujudu wakubwa, kuficha matatizo mbele ya mgeni n.k kaka hii si hulka hii ni tabia ya makundi ya watu duniani kote na makundi hayo yapo manne sasa ukijifunza aina ya makundi manne ya tabia za mwanadamu utafahamu hulka zao ama mazoea yao kwa kina. niishie hapa kwanza
 
Back
Top Bottom