Kishindo cha BAVICHA mkoani Rukwa

Wakuu, Kwanza naomba radhi kwa kushindwa kupachika pix za BAVICHA hapa jamvini pindi walipokuwa Mpanda. Kwa walitembelea uzi wa Mtoto wa Mbale (M4C Sumbawanga Picha) watakua wameona makamuzi ya vijana hawa ambao wako kazini mkoani Rukwa na Katavi. Wakiunguruma katika viwanja vya shule ya Msakila mjini Sumbawanga John Heche na Deo Munishi leo wamezidi kusasambua serikali ya chama cha mapinduzi na safari hii wameivua nguo na kuiacha uchi wa mnyama. Wakati Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deo Munishi akiwaambia maelfu ya wananchi wa Sumbawanga kuwa raisi Kikwete na CCM yake ni waongo waliokubuhu kwa kuwadanganya watanzania kutengeneza ajira milioni moja ambazo mpaka sasa watu wameishia kuokota makopo barabarani, John Heche alimfananisha na matonya ambaye ana kazi ya kuomba omba na tofauti yao ni kwamba rais Kikwete anapanda ndege akiwa amevaa suti kuomba wakati matonya wa mtaani anaomba akiwa dhoofu bin taaban. Wakati Munishi akibainisha ni jinsi gani ilani ya Chadema ya 2010 ilivyobainisha jinsi ya kutatua tatizo la ajira kwa mamilioni ya vijana wa kitanzania na wananchi wote kwa ujumla kwa kujikita katika kutengeneza uchumi wa viwanda vikubwa (Heavy), vya kati na vidogo sambamba na kufanya mapinduzi ya kweli ya kilimo na hivyo kuunganisha uchumi wa vijijini na mijini, John Heche alibainisha jinsi serikali ya CCM inavyoidhoofisha nchi kwa kulea wezi huku ikiuza rasilimali za Tanzania ikiwaacha wananchi wakielemewa na umasikini wa kutupwa. Munishi aliwataka wananchi kuona umuhimu wa kufuta vyeo vya ukuu wa wilaya na mkoa kwani uwepo wake hauna maana yeyeote ile kwa watanzania zaidi ya kuwa kichaka cha kutoa ulaji kwa maswaiba wa rais na akaongeza kuwa kama vina umuhimu basi sharti watu hawa wachaguliwe na wawajibike kwa wananchi moja kwa moja. Alitumia fursa hiyo kumponda Mkuu wa Mkoa wa Rukwa bibi Stela Manyanya kwa kushindwa kuhimili kishindo cha BAVICHA na hivyo kuamua kupita kule walikopita ili kufuta nyayo zao. Wakati John Heche akimponda Mwigulu anayejifanya mchumi wa benki kuu kuwa sio mchumi bali ni kilaza wa benki kuu na kwamba walipaswa kufika Rukwa kuwaeleza wananchi wa Rukwa kwa nini wao ni masikini wakati wanazalisha chakula cha kuilisha Tanzania na pia wanakalia madini mbalimbali kama dhaabu kwenye mbuga ya Katavi na mbuga yenyewe ya Katavi, Munishi alimchana Mwigulu huyo huyo na Nape kwa kusema kuwa kama kushirikiana na chama cha CDU kinachounda serikali ya Ujerumani kunafanya CHADEMA kiunge mkono USHOGA basi na CCM nacho ni chama cha MASHOGA kwa kuwa nacho kinashirikiana na SDP ambacho nacho kinaunda serikali ya ushirika ya Ujerumani. Pia aliendelea kusema kuwa kama kushirikiana na Conservative ya Uingereza kunaifanya CHADEMA kuunga mkono USHOGA basi CCM na Serikali yake ni ya MASHOGA kwa kuwa inapokea misaada kutoka serikali ya Uingereza inayoongozwa na Conservative wakishirikiana na LIBDEM. Wakati John Heche akiwataka wananchi kupunguza mamlaka ya rais kupitia mchakato wa kuandika katiba mpya kwa kutoa maoni yao, Munishi alihamasisha vijana kudai Baraza la Taifa la Vijana ili liwe chombo maalumu cha kuwaunganisha na kutetea maslahi ya vijana wote Tanzania bila kujali itikadi za kisiasa, kabila rangi wala dini. Kwa taarifa ni kwamba leo Viongozi hawa wa BAVICHA wataendeleza moto wao mjini Tunduma na Mbeya Mjini.
Mziki wa CHADEMA ni mnene. Yaani vijana wanawatesa mawaziri na CCM kiasi hiki. Hii ni udhiirisho wa jinsi BAVICHA ilivyosheeni vijana wa ukweli wenye tija ambao wanakisaidia chama kwa mapana. Mzee Dr Slaa endelea kutulia vijana wafanye kazi kama hizi. Upanguzi wa hoja mfu za CCM umenikuna kweli kweli. Hongera HECHE, heongera MUNISHI
 
Watu wanaimarisha chama wengine wanawaza urais, upuuzi mtupu,komaeni makamanda
Yaani inakera saana. Hivi wanataka urais kwa kutumia chama gani wasichotaka kukijenga. Vijana wa CHADEMA msikubali chama chenu kiyumbishwe na walevi wa madaraka.
 
Wapi UVMASABURI? WAPI NAPE MPAKA CAROLINE NA PODA? WAPI KILAZA WA BOT MWIGULU? CHEZEA BAVICHA WEWE? MTAJUTA KUIFAHAMU.
 
Vijana sauti zina kauka kwakusambaza sera za CDM mengine yamekalia kuchukua rushwa Tanesco na kutanganza kuwania urais Huku yakiungana na ccm kufisadi hii nchi
Ni jukumu lenu makamanda HECHE na MUNISHI kuwaunganisha vijana nchini. Msikatishwe tamaa na wehu wasiokitakia chama kheri.
 
Back
Top Bottom