Kishindo CCM ; Nape hatarini kung’olewa uenezi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Tuesday, November 22, 2011, 5:44




*Nape hatarini kung'olewa uenezi

*JK ajipanga kuvunja makundi, mahasimu
*Wasiwasi watanda, kila mmoja na utabiri yake

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAKATI joto la kisiasa likizidi kupanda miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi kwa ujumla, Rais Jakaya Kikwete, anatarajiwa kutumia uwiano wa kisiasa (political balancing act), ili kujaribu kurejesha amani ndani ya chama hicho.

Chanzo cha habari ndani ya vikao vya juu vya CCM vinavyoendelea, kimeliambia MTANZANIA kuwa lengo kuu la mkakati huo ni kuhakikisha makundi hasimu yanavunjwa na viongozi wanaotajwa kuwa katika mapambano wanashughulikiwa mmoja mmoja.

Mahasimu wakuu wanaotajwa ndani ya chama hicho ni kundi linalojiita wanachama ‘waadilifu' na kundi jingine ni ambalo wale ‘waadilifu' wanaliita la mafisadi.

"Ninachoweza kukwambia ni kuwa, Mwenyekiti wetu ni lazima avunje makundi yenye uhasama ndani ya chama, kwa sababu bila kuyavunja, basi chama kiwe tayari kuvunjika vipande vipande na hili hatuwezi kukubali litokee.

"Na ili aweze kuvunja makundi hayo hasimu, hana budi kushughulika na wale wanaotajwa kuwa viongozi wa makundi. Sasa hawa watajieleza na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.

"Si sahihi kusema wafukuzwe na katika hili, tunaweza kuamua kutumia busara ya madaktari pale wanapomshauri mgonjwa wa kansa kutokata sehemu yenye mwili iliyoathirika na ugonjwa huo, kwa sababu kwa kuikata mgonjwa baada ya muda mfupi anaweza kupoteza maisha.

"Haya mambo ya kutimuana nadhani wote tunakumbuka yalivyoigharimu Zanzibar, ambapo kwa miaka wakasahau mambo ya msingi ya maendeleo, badala yake wakapoteza muda mwingi kwenye malumbano. Nadhani ni vema kujifunza kutokana na makosa tuliyofanya siku za nyuma," alisema.

MAHASIMU KUSHUGHULIKIWA
Mahasimu wanaotajwa zaidi katika mgogoro ambao kwa kiasi kikubwa unakiyumbisha chama ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa, chama kinakusudia kuchukua hatua dhidi ya wote wanaotajwa, ambapo miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kumuondoa Nape katika nafasi yake ya sasa.

Katika hatua hiyo, bila kutaja muda halisi wa utekelezaji wake, zimesema kada huyo kijana ambaye anatuhumiwa kuchochea moto wa uhasama, atapangiwa kazi nyingine katika moja ya balozi zetu nje, na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, ambaye pia kwa nyakati tofauti amekuwa akitoa kauli tata katika mikutano ya hadhara.
"Kumpangia kazi nyingine Nape ni sawa, kwa sababu hata hii dhana ya kujivua gamba ni yeye ambaye awali kabisa aliipotosha, ingawaje sasa anajaribu kufukia mashimo, lakini kumweka Lusinde badala yake itakuwa ni hatua kubwa kuelekea kukiua kabisa chama," alisema mmoja wa wajumbe wa NEC.

NAPE ALAMBA MATAPISHI YAKE
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Nape alisema kuwa, dhana ya kujivua gamba kamwe hailengi mtu, lakini lengo lake ni kuleta mageuzi ndani ya chama hicho katika nyanja mbalimbali.

Katika mkutano huo, alivilaumu vyombo vya habari kwa kile alichokiita kutomuelewa na kupotosha ukweli, na kuahidi kuwa, kuanzia sasa chama hicho hakitavumilia tena upotoshwaji unaofanywa na vyombo vya habari.

Kwa wale wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa, watakumbuka kuwa baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kutangaza dhana ya kujivua gamba mjini hapa Februari 5, 2011, Nape na Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Chiligati, walizungumza na vyombo vya habari
.
Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, waliwataja watuhumiwa watatu wa ufisadi ambao ni aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Lowassa na Chenge na kuwataka ndani ya siku 90 wawe wamejiondoa wenyewe, vinginevyo chama kitawaondoa.

Pia siku ambapo Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, alipokutana kwa mara ya kwanza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Nape alirudia kauli ya siku 90 na kusababisha kupingana hadharani na bosi wake, ambaye alisema hilo halikuwapo katika ajenda za vikao vya CCM.

Lakini jana katika hali ya kushangaza, Nape hakuzungumzia siku 90 na badala yake alisema mpango au dhana ya kujivua gamba ni suala la muda mrefu.
Alipobanwa zaidi aliseme; "Jamani mtu anapoamua kuoga, ni lazima awe na pa kuanzia, iwe miguuni au kichwani, kujivua gamba ni mageuzi ndani ya chama yatakayochukua muda mrefu.

"Dhana haijaeleweka vizuri, kusimamia uadilifu si kuleta mpasuko ndani ya chama na kutenganisha wabadhirifu na waadilifu si kubomoa chama."

Nape, aliwalaumu wanaomuhusisha na makundi ndani ya chama, na kudai yeye hana kundi, ila wanaomuhusisha wanatafuta njia ya kukwepa majukumu.

Alikiri kuwapo kwa hali kubwa ya wasiwasi miongoni mwa wana-CCM na wananchi, na kuvituhumu vyombo vya habari kwa kusababisha hali hiyo, ambapo alisema hali ndani ya vikao vinavyoendelea ni shwari na tulivu.

Lakini taarifa zilizozagaa mjini hapa zinadai kuwa, kauli hizo za Nape zina lengo la kupoteza lengo, ilhali akijua kuwapo kwa mipango na mikakati ya kuwaumiza kisiasa mahasimu wake na wa kundi lake, kabla ya kumalizika kwa vikao mwishoni mwa wiki hii.

Mwisho.



 
Basi na Rostam Aziz arudi maana haikuwa dhana ya kauli hiyo kwa yeye ujitoa ccm na ubunge,wamrudishe waendelee kukirekebisha chama kwa staili ambayo ndio wanayoisema sasa wahuni tuu hawa...Nilijua tuu hakuna kitu kwenye kujivua wala nini ilikuwa danganya toto...CRAAAP..!!
 
Wishful thinking. Unasema Mwenyekiti anataka kuvunja makundi na huku wanachochea wengine waondolewe kwenye nafasi zao. Hiyo ni contrdiction ya nguvu.
 
......LL, Lusinde Livingstone, huyu ninayemfahamu, basi nakubaliana na mwandishi kwamba hii ni hatua nyingine kubwa zaidi ya kukiua kabisaaa chama, yaani hiki cha magamba, well done jk, kazi yako ya kuisambaratisha ccm itakuwa imetimia.
 
BAADHI YA WAZEE WALIOWAHI KUVUMAA HUKO CCM WADAIWA KUKACHA VIKAO VYA NEC DODOMA BAADA YA KUNUSA HARUFU ZA FEDHA HEWANI NA POTEZESHA DIRA MKUTANO MZIMA NA VILE VILE 'MUSWADA WA MAKINDA' KUONEKANA SUBILI



Eti mkutano wa CCM Dodoma; hakuna kitu pale na ni bure kabisa!!! Swala lote la gamba kuvuka limegoma mara baada ya kuloweshwa na utitiri wa vijisenti na kuwa ngumu na kunata zaidi mwilini. Hiyo ndio maana baadhi ya wazee wa chama hicho wakaamua kujitunzia heshma zao mbali yale yanayoendelea huko.

Kuna ugomvi mkali mno wa makundiunaoendelea ndani CCM hadi dakika hii lakini yote yanaendelea hivi sasa nyuma ya pazia.

Nasema ugomvi hatari ya kuwahi kutokea CCM unaendelea kupamba moto hadi kakika hii tunavyoendelea kuandika humu.

HAKUNA tena mwenye ubavu wa kufungia paka fisadi kengele baada wale wazee wenyewe kusikia ukigeugeu na unafiki kutoka Magogoni hdi wakaamu kujiweka kando na mkutano wa NEC CCM kule Daodoma ambao kwa maelezo yao ni kwamba hauna dira.

Vile vile kuna taarifa kwamba nako nyumbani kwa wana CUF nako si shwari kote Bara na Visiwani kutokana na uamuzi wao kuunga mkono muswada uliowaondolea kabisa matumaini wananchi wa pande zote mbili.

Kama mtu bado anasubiri zaidi moshi wa kijani na zambarau kuhusu BOMU linalowasubiri hadi hivi sasa basi kajikalie hapo. Mama Anna Makinda wabunge wa CUF huku Dodoma wamevimaliza kabisa hivi vyama viwili vya CCM na KAFU; hakuna tena kitu pale!!
 
CCM ni sawa na mbwa koko. Ingekuwa mimi ni dr ningewapeleka mirembe wote,hawaelewi lipi wanalolisimamia.
 
He he he! CCM kuna virojo! Kwa hiyo nafasi hiyo ya Uenezi ndivyo inavyo kwenda eeh! chini juu, juu chini.
Kulikuwa na Chiligati akampa pasi Nape. Naye ndio hivyo atampa Lusinde kisha kama sikosei basi Lusinde naye anaweza mpa pasi King'wendu (yule comedian) maana kumbe cheo hicho kinaenda kwa anayejua kuchekesha zaidi.
 
Ni hatari tupu kwa kuwa Magogoni Strategist hawakujiuliza vya kutosha MASWALI MAGUMU juu ya factor zote za kisiasa nchini badala yake wao walifunikwa akili na wingu tu la KULIKOMESHA CHADEMA na sasa ndio haya machungu yote ndani ya CCM na CUF kote nchini.

Hwezi kutumia kitu wanachokiita Waingereza IDEAL SITUATION kupanga mikakati kama haya na kupuuzilia mbali the REAL AND PRACTICAL SITUATION kwa uhalisia wake on the ground. Tathmini ya kina inabaini kwamba SHERIA YA KIKWETE kujitungia kujitungia katiba ni zao la CONVICTIONS BASED ON FEELING zaidi huku REASONING ikisamehewa na kupelekwa kulala mapema kabla ya maamuzi yote haya - A BOOMERUNG IS ON!!!

Nasema fukuto na ngoma zenyewe ndani ya vyama hivyo viwili machoni mwao umma wa Tanzania bado ni mbichi kabisa!!! Wenye kung'amua mambo haraka habari ndio hiyo.
 
CCM wamekwisha,hawana tena chao. Kiwete wao keshamaliza kazi ya KUIUA CCM na sasa wanasubiri mazishi.
CCM iliishia enzi za mwalimu kwa sasa hakuna kitu pale ni ufisadi,ubabaishaji,ujambazi,uhuni na uonevu kwa kila Mtanzania mpenda haki. Kama Chama kimeanza kutafunana wao kwa wao unategemea nini pale? Angalia Mwakyembe,angalia Mwandosya,angalia Rostam,angalia Lowassa,angalia Chenge,angalia Sitta, halafu upate picha ya nini KINACHOIMALIZA CCM!!!

CCM ni ya KUPIGA CHINI! Nasema piga chini huyo!Piga chini mafisadi na Magamba yao wameshatuchosha!
 
Ni kama vile karuma analzamishwa UCCM hautaki kabisa. Katika matukio yote muhimu ya CCM, sni mara chache sana amewahi kujivisha kijani. Siku zote yeye yuko tofauti na wengine. KJuna wakati CCM Dar ilipokuwa ikifanya kikao, na yeye anaita cha kwa Zanzibar ili asihudhurie kile cha Dar ilhali yeye ni Makamu mwenyekiti tu. CCM ni chama cha ajabu kweli
 
Back
Top Bottom