Kisa halisi: Nani mlinzi na mtekelezaji wa sheria za mazibgira?

Sophist

Platinum Member
Mar 26, 2009
4,484
3,400
Ndugu zangu.
Bado sisi watanzania hatujafahamu wajibu wa utekelezaji wa sheria (law enforcement) zilizopo hapa nchini, hata kama tukiona sheria hizo zinavunjwa.
Kisa halisi: Siku moja mama mmoja (Mzungu) alikuwa akisafiri, akaona vijana wanachoma moto msitu, akasimamisha gari lake na kuwaita vijana hao na kuanza kuwahoji kwa nini wanafanya hivyo. Vijana hao walianza kumzomea sana na kumtolea matusi ya ajabu. Mama huyo aliwaacha vijana na kundelea mbele. Baada ya kilometa kama mbili aliona Kituo cha Polisi, akasimamisha gari na kuwaendea askari wawili waliokuwa wamekaa kwenye benchi nje ya kituo wakicheza karata na kuwaambia "ona kule nyuma moto unachoma msitu, nimeona watu wanachoma, bado wako pale pale, twende tusaidiane kuuzima". Bila kushtuka, Askari mmoja alijibu "tumeuona moto huo tangu muda mrefu, nenda ukamwambie Mwenyekiti wa kijiji achukue hatua." Yule mama alifadhaika sana kuona "watekelezaji wa sheria" hawajali hata kidogo.
Alipofika kwa Mwenyekiti wa kijiji, alitoa maelezo yale yale. Mwenyekiti alijibu; "kwanza wewe kwenda Polisi ulifanya makosa, Polisi hawahusiki na mambo ya moto; hii ni kazi ya Afisa Misitu. Pili hata mimi sina la kufanya sasa hivi maana Afisa Misitu wetu yuko likizo" Mzungu alisikitika sana.
Kwa kuwa alikuwa na namba ya simu ya Mkuu wa Wilaya, aliamua kumpigia siku na kumsimlia kisa chote. Mkuu wa Wilaya alijibu "pole mama; lakini kwa sasa sina la kukusaidia maana Afisa Maliasili wetu ameishatoka kazini.... tusubiri kesho asubuhi nitalishughulikia"
Mama huyu ambaye alijulikana kwa jina la Sista Lamert Kortimum alianza kutoa machozi mbele ya Mwenyekiti wa Kijiji ambaye alianza kumdhihaki na kusema "Sista. mbona una uchungu wa mwana kuliko mzazi...?"
Kisa hiki ni cha kweli ambacho kilitokea si siku nyingi zilizopita.
Ndugu zangu, nani mtakelezaji wa sheria za nchi hii? Naomba jibu na mchango wenu.

Mwanamazingira mwenzenu,

Yusto P. Muchuruza
EXECUTIVE DIRECTOR-KADETFU
+255754740267
kadetfu@gmail.com
Kagera Development and Credit Revolving Fund (KADETFU) - HOME.

Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
 
Back
Top Bottom