Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
Bongo siku hizi hakuna popobawa tumuonyeshe huyu msukuma kazi.
poor ngeleja..tulikuwa tunamfikiria kama anaweza kuwa kati ya kundi la mawaziri vijana ambao mwaka 2015 tutawafikiria kuwaunga mkono......lakini kumbe HAFAI ameshalewa ulevi wa ukubwa ....anatukana wanyonge matusi ya nguoni...,anavunja utaratibu..na kudharau watu ...na zaidi ya yote anangangania MNYONGE afukuzwe kazi.tena bila kosa ..kama adhabu....bila kuhesabu yeye amewatendea watanzania milioni 40 makosa mara ngapi yanayotugharimu kila siku....
kijana ngeleja ya have done a mistake which has just cost you your political future ....tunakuarifu kuwa tumefuta jina lako katika list ya potential runners wa 2015 na milele amina!!!!! forget that post!!!
Ngeleja Huna adabu!!!
Laligeni labda kama wewe ni learned sister/brother ujitoe kumsaidia!! vinginevyo usimuingize matatizoni mtanzania mwenzetu kwa kweli!!!
afu Ngeleja eti 'unanijua mimi ni nani'....who cares bana kwani hapo ulipo umanisaidia nini bana!! kwa taarifa yenu akija kwenye mgahawa wangu anapanga foleni kama mteja wangu yeyote(FIFO)!!! kwani zake ni za dhahabu!!!
Bahati yake mbaya sikuwa wa pili kwenye hiyo foleni, maana nisingesubiri mlinzi amtoe, ningemwambia mwenyewe i want to use this service so you can continue to talk in your car.
Mkuu Umenena. I really hate a person who starts an mkwara wa 'Unanijua mimi ni nani?' Nikujue ili iweje bana? nakuona una mikono miwili, miguu miwili, macho mawili, sili kwako na kadhalika so definitely you are a fellow Human Being and not a Martian from a far, far away galaxy!SO WHAT?
ha ha ha bibie umeiandika kiuchungu sana kama angekua mbele yako ungempa makofi teh teh!! Ndio bongo ilivyo ye anajua wote tunaangalia TV so tht utakua unamjua tuu!! Heri ya mwaka mpya!aaah si ndo hapo sasa babadesi!!! hata nikujue inanisaidia nini mtanzania ninayeteseka na wewe unabonyoa tu PAYE inayoniumiza kila mwezi dispite ya kijisalary ambacho hainikidhi hata basic needs!!
ha ha ha bibie umeiandika kiuchungu sana kama angekua mbele yako ungempa makofi teh teh!! Ndio bongo ilivyo ye anajua wote tunaangalia TV so tht utakua unamjua tuu!! Heri ya mwaka mpya!
Hapo kwenye nyekundu hapo umepiga penyewe!! teh teh tehumenisoma kiundani wewe chaaaaaaaaaaa!! heri ya mwaka mpya wa uchaguzi Kimey!!! ila sijui kweli kama ntapoteza mda wangu kwenye foleni ya kupiga kura in the name of 'eksesaizing my voting right'
unanijua mimi....jamaa tv yenyewe anachabo kwa jirani tena michezo ya kuigiza sasa Ngeleja atamjuaje???
hata akimjua bana sasa ndo uwapotezee watanzania wengine wenye haraka ya kupata huduma na kwenda kuhanja huko, kisa unaongea na simu!!!
nyamabafu kwanza PAYE kubwa kuliko PPF na NSSF. ahhhhh mi naumia kweli
Huyu the so called Ngereja anaonekana ni Mshamba sana na mambo ya ATM... Tangu lini aliona kwamba vibanda vya ATM ndio vya kufanyia maongezi ya simu... au alikuwa na mpango wa kufanya kama Wale Wa-bulgaria...
Halafu hii ya kumtishia mtu eti hivi hunijui... kwani yeye ni kiumbe adimu? Anajulikana kwamba yeye ni binadamuwa busara, na kilichokuwa kinafanyika ni kumkumbusha kwamba kulikuwa na msururu wa watu unangojea kutumia facility hiyo na sio peke yake...
Pia ya nini Ngereja kufanya yote hayo mpaka mlinzi wa watu kuitwa ofisini kwake? Haya ni matumizi mabaya sana ya ofisi ya Ngereja... Ofisi ni mali ya umma na inabidi iheshimiwe na si mahala pa kuingia kila kitu hata walinzi wa ATM. Inafaa ngereja aitwe NGEDELE maana ni huyu mnyama pekee anayerushiwa jiwe na kukurushia tena jiwe hilo...
Pia inafanaa awajibike kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma kwa kujiuzuru haraka sana... kama angekuwa na kasi ya kushughulikia matatizo yetu basi Umeme ungewaka TANZANIA masaa 24 siku 365 za mwaka...
Amenikera sana na namlaani kwa kitendo chake cha kutaka mwenzake aoteshe kibarua chake majani...
afu si unaona eeeh Ngeleja eti analeta jeuri usikute na yule askari aliyetukanwa tuhela twake tunakwatwa PAYE...aaah jamani nyieHapo kwenye nyekundu hapo umepiga penyewe!! teh teh teh
What a guess...........!!
Hujaelewa nini sasa? usilete ukilaza wako...
- Hivi hebu tuwe Great Thinkers japo kidogo tu, katika hii article ni wapi hasa panapoashiria kwamba Waziri alitaka kuzichapa? Mbona kama kichwa cha habari na habari hazifanani?Waziri Ngeleja nusura azichape kwa adha ya ATM Dar OchuToday, 05:52 AM
NI BAADA YA KUTAKIWA AWAPISHE WATEJA
Sadick Mtulya
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, juzi alizua tafrani kwenye mashine ya kuchukulia fedha (ATM) ya benki ya Standard Chartered, jijini Dar es Salaam baada ya kutaka kumchapa makonde mlinzi wa mashine hiyo, Pascal Mnaku. Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na mlinzi huyo wa kampuni ya Ultimate Security, zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 asubuhi kwenye jengo la Habour View, maarufu kama JMall.
Mnaku aliliambia gazeti hili kuwa alinusurika kupigwa na waziri huyo kijana aliyekuwa akizungumza na simu ndani ya kibanda hicho, baada ya kumtaka atoke kuwapisha wateja wengine kupata huduma hiyo. Mnaku alisema waziri huyo alikuwa anatumia muda mwingi kuzungumza na simu ndani ya mashine hiyo badala ya kuchukua fedha wakati msururu mrefu wa watu ukiwa unamsubiri atoke.
"Kwanza mimi sikujua kwamba mtu niliyemwambia awapishe wateja wengine ni waziri. Ni kweli nilimfuata na kumwambia awapishe kwa sababu alikuwa anatumia muda mwingi kuzungumza na simu, wala sikuwa na nia nyingine yoyote mbaya dhidi yake," alisema Mnaku na kuongeza:
"Lakini, waziri huyo ghafla aligeuka na kuanza kunifokea akiniambia wewe unanijua mimi nani?... hunijui mimi! na kunitusi, (matusi yasiyoweza kuandikika)."
Mnaku aliendelea kueleza kuwa; "Kutokana na hali hiyo nilipomjibu kwamba, mimi sikuwa na nia mbaya na nilifanya vile ili wateja wengine wapate huduma". Aliongeza: "Baada ya kumwambia hivyo akazidisha ukali, lakini watu walipoanza kukusanyika, huku wengine wakimwomba radhi kwa kumtaja jina, alianza kupunguza hasira na kuondoka".
Kwa mujibu wa mlinzi huyo, baada ya tafrani hiyo iliyodumu kwa takribani dakika nane, Waziri Ngeleja aliondoka na baadaye kunako majira ya saa 7:00 mchana uongozi wa kampuni yake ya ulinzi ulimwondoa katika kituo hicho cha kazi na kurudishwa makao makuu. Alisema saa 9:30 jioni, alichukuliwa na uongozi wa kampuni hiyo na kupelekwa ofisini kwa Ngeleja kwa ajili ya mazungumzo zaidi.
"Baada ya kutokea kwa tukio saa 9:30 jioni wakuu wangu walinipeleka ofisini kwa Ngeleja na kisha akazungumza mengi ambayo siwezi kukuambia na baada ya hapo wakuu wangu wakamuomba msamaha kwa niaba ya kampuni," alisema Mnaku. "Na kwa sasa maelekezo niliyopata kutoka kwa waajiri wangu ni kwamba, wanalifanyia upelelezi suala hili hivyo hatima ya kibarua changu kinategemeana na majibu ya upelelezi huo," alisema Mnaku
Mashuhuda wa tukio hilo walilieleza gazeti hili kuwa hali hiyo ilijitokeza baada ya Mnaku kuwahamishia wateja kutoka katika mashine ya ATM ya Barclays iliyoko katika jengo hilo ambayo wakati huo ilikuwa imeishiwa fedha.
"Baada ya Mnaku kuona mashine ya ATM ya Barclays kuwa haina fedha, ndipo akalazimika kuwaambia wateja wakatumie ATM ya Standard Chartered ambayo wakati huo Waziri Ngeleja alikuwa anaitumia na huku akizungumza na simu,†alisema shuhuda mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe.
Shuhuda huyo alisema baada ya Mnaku kumtaka waziri kuwapisha wengine, ghafla na huku akiwa na hasira, Waziri Ngeleja alisema: "Ina maana hunijui mimi, hujui nafasi yangu, halafu...tusi," alisema shuhuda huyo.
Shuhuda huyo aliongeza: "Kutokana na maneno hayo, Mnaku akamjibu kwa kujitetea kwamba, mimi nimekuomba uwapishe wateja wengine, sikuwa na lingine".
Habari zaidi zinadai kwamba, katika kikao na waajiri wa Mnaku, Ngeleja alisema: "Siwezi kumsamehe (Mnaku) mpaka atakapopewe adhabu kali."