Kisa cha Waziri Ngeleja na Mlinzi kwenye ATM

ngeleja ni tatizo hapo wala wasimwogope yeye nani nchi hii ni mwizi tu nae

urafiki wao na JK ndo watanzania tutaumia sana
 
Hya ndiyo matatizo ya tunchi tulitokuwa korapti, yaani mtu akishakuwa kwenye public office tayari anakuwa ni Mungu mtu..........

Cha kushangaza hata hao mabosi wa Ngeleja they may neva ask him anything about this! Hii haiwezi kutokea nchi zilizoendelea na zilizokomaa kidemokrasia. Kwanza waziri kujibizana kimipasho na mwananchi tena sehemu yake ya kazi regardless nani mchokozi ni ukosefu wa busara
 
hi kali - ila nachojua mimi ukiwa waziri unakuwa exempted kwenye public services kwamba hutatakiwa kupanga foleni na unatakiwa kupata huduma muda uleule na kuondoka ili uwahi majukumu ya kiserikali ya kufanya.

Kwa hiyo hata kama Ngereja angekaa mule saa nzima anaongea na simu hakuna ubaya, may be alikuwa anaongea na Bosi wake (Rais) kwa hiyo hawezi kum hold bosi wake na lazima akae sehemu kuna privacy. (Hii inafanya kazi kama simu ilikuwa muhimu sana na asingeweza kui hold)

Fast track kwa mawaziri hainipi shida kuielewa. Lakini hili la Ngeleja ni ukosefu wa busara. Hata kama ni waziri (au mtu yeyote mwenye dharura) ukikuta watu wapo kwenye foleni ni busura ukajitambulisha na 'kuomba' hiyo fast track.

Hili la waziri kukaa kwenye ATM saa nzima nashindwa kuelewa, na linanipa shida zaidi kama kukaa kwake huko si kwamba anatumia ATM bali anaongea na simu! No way! Yule bawabu was right whether or not alijua kwamba ni waziri.
 
Humu jamvini kuna waandishi wengi,kwa nini wasifuatilie tukio hili na likatoka magazetini ili wananchi wa kawaida ambao hawana muda wa kusoma mtandaoni wakawajua viongozi wao waliowachagua wakoje? Kisa cha Meya wa Moshi kumpiga mlinzi makofi kama kisingetoka magazetini kingeisha kimya kimya lakini kusambaa kwa habari ile kumefanya haki itendeke. Wajibikeni waandishi.

ipo kwenye mwananchi ya leo mkuu
 
Kama ni kweli inabidi waziri aombe radhi hadharani. Kwenye hizo ATM si kunatakiwa kuwa na camera? Obama anajipanga foleni kupata huduma, hawa mawaziri wetu wanaona nini tatizo? Huyu mlinzi akifukuzwa kwa sababu hii basi itakuwa vyema kama wale mawakili wetu wapenda haki watalivalia njuga.

Amandla......
 
poor ngeleja..tulikuwa tunamfikiria kama anaweza kuwa kati ya kundi la mawaziri vijana ambao mwaka 2015 tutawafikiria kuwaunga mkono......lakini kumbe HAFAI ameshalewa ulevi wa ukubwa ....anatukana wanyonge matusi ya nguoni...,anavunja utaratibu..na kudharau watu ...na zaidi ya yote anangangania MNYONGE afukuzwe kazi.tena bila kosa ..kama adhabu....bila kuhesabu yeye amewatendea watanzania milioni 40 makosa mara ngapi yanayotugharimu kila siku....

kijana ngeleja ya have done a mistake which has just cost you your political future ....tunakuarifu kuwa tumefuta jina lako katika list ya potential runners wa 2015 na milele amina!!!!! forget that post!!!

Ngeleja Huna adabu!!!
 
bahasha kaka bahasha waandishi wa tanzania ni matapeli 20per wakipewa bahasha wananyamaza kimya
 
Inaonekana ndivyo alivyo hata "Vasco" akisikia unadhani atamfanya kitu?
Namuonea huruma mshikaji kibarua kinawezaota nyasi..
Lakini alikosea akimbebabeba pale afu mengine baadaye...
Ni viongozi wote wa kibongo full ujivuni....Wanaboa balaa!!!!
 
Habari zaidi zinadai kwamba, katika kikao na waajiri wa Mnaku, Ngeleja alisema: "Siwezi kumsamehe (Mnaku) mpaka atakapopewe adhabu kali."

Ndugu waziri unapaswa usamehe kama unavyosamehewa na watanzania mil 40 unaowakosea
Hiyo familia ya Mnaku inayomtegemea naamini sasa hivi inalia machozi ya damu kwa sentensi yako hii

hima ngeleja msamehe na utoe taarifa kwenye press
 
poor ngeleja..tulikuwa tunamfikiria kama anaweza kuwa kati ya kundi la mawaziri vijana ambao mwaka 2015 tutawafikiria kuwaunga mkono......lakini kumbe HAFAI ameshalewa ulevi wa ukubwa ....anatukana wanyonge matusi ya nguoni...,anavunja utaratibu..na kudharau watu ...na zaidi ya yote anangangania MNYONGE afukuzwe kazi.tena bila kosa ..kama adhabu....bila kuhesabu yeye amewatendea watanzania milioni 40 makosa mara ngapi yanayotugharimu kila siku....

kijana ngeleja ya have done a mistake which has just cost you your political future ....tunakuarifu kuwa tumefuta jina lako katika list ya potential runners wa 2015 na milele amina!!!!! forget that post!!!

Ngeleja Huna adabu!!!

Mkuu,
Ngeleja ni zao la malezi mabaya tu siajabu toka utotoni!!! na ulimbukeni wa ukubwani...
 
Nyie watu vipi?

Kwa nini Waziri amsamehe Mlinzi na si Mlinzi amsamehe Waziri kwa matusi yake?

Wale Mawakili wa haki za binadamu naomba waliingilie kati hili swala. Huyu Waziri ndiyo inatakiwa apandishwe kizimbani kwa kutowa matusi.

Halafu wee unayesema anaweza kukaa hata saa nzima akiongea, kwa nini asingelitoka na apewe chumba pale Bank na aongee hilo saa lake zima. Kwani akirudi si watampisha achukue pesa zake?

Kwa nini mnawafanya hawa watu Miungu watu? Nategemea mwaka huu watu wa Sengerema watafanya kweli na jamaa ATOSWE. Labda Kikwete ashinde tena na amchukue jamaa kama Mbunge wa kuteuliwa. Sasa naamini, matunda ya nchi corrupt ni mabaya saana. Tumeyanunua wenyewe kwa kanga na Tshirt za njano/kijani.
 
Kama ni kweli inabidi waziri aombe radhi hadharani. Kwenye hizo ATM si kunatakiwa kuwa na camera? Obama anajipanga foleni kupata huduma, hawa mawaziri wetu wanaona nini tatizo? Huyu mlinzi akifukuzwa kwa sababu hii basi itakuwa vyema kama wale mawakili wetu wapenda haki watalivalia njuga.

Amandla......

Ofisi kuu isikae kimya na impatie ushauri nasaha.
 
poor ngeleja..tulikuwa tunamfikiria kama anaweza kuwa kati ya kundi la mawaziri vijana ambao mwaka 2015 tutawafikiria kuwaunga mkono......lakini kumbe HAFAI ameshalewa ulevi wa ukubwa ....anatukana wanyonge matusi ya nguoni...,anavunja utaratibu..na kudharau watu ...na zaidi ya yote anangangania MNYONGE afukuzwe kazi.tena bila kosa ..kama adhabu....bila kuhesabu yeye amewatendea watanzania milioni 40 makosa mara ngapi yanayotugharimu kila siku....

kijana ngeleja ya have done a mistake which has just cost you your political future ....tunakuarifu kuwa tumefuta jina lako katika list ya potential runners wa 2015 na milele amina!!!!! forget that post!!!

Ngeleja Huna adabu!!!

You've said it! Kweli hana adabu!! Hata kama yeye ni Waziri kumtukana mtu ambaye alikuwa anatimiza wajibu wake si uungwana hata kidogo.

Ngeleja anadhani kwa kuwa yeye ni waziri basi kila mtu anaweza akamtambua akipita barabarani? Basi bora yeye na wote wanaotaka kutambuliwa mitaani kwa nyadhifa walizonazo waweke 'lables' nyusoni tujue moja ili kila tukiwaona tuwasujudie! Wanasahau kwamba hao ndio wapiga kura wakati wa kampeni akina Ngeleja watageuka na kuwasujudia ili wapate kura za wanaowatukana sasa!
 
Nyie watu vipi?

Kwa nini Waziri amsamehe Mlinzi na si Mlinzi amsamehe Waziri kwa matusi yake?

Wale Mawakili wa haki za binadamu naomba waliingilie kati hili swala. Huyu Waziri ndiyo inatakiwa apandishwe kizimbani kwa kutowa matusi.

Halafu wee unayesema anaweza kukaa hata saa nzima akiongea, kwa nini asingelitoka na apewe chumba pale Bank na aongee hilo saa lake zima. Kwani akirudi si watampisha achukue pesa zake?

Kwa nini mnawafanya hawa watu Miungu watu? Nategemea mwaka huu watu wa Sengerema watafanya kweli na jamaa ATOSWE. Labda Kikwete ashinde tena na amchukue jamaa kama Mbunge wa kuteuliwa. Sasa naamini, matunda ya nchi corrupt ni mabaya saana. Tumeyanunua wenyewe kwa kanga na Tshirt za njano/kijani.

NImeambiwa kuna idara ya ethics pale kwa mkulu, i hope watamwita wamweke sawa... ila sintashangaa akirudi, tena anaweza kupokewa kwa maandamano kama ngudu yenu Chenge... Kuna wakati huwa siwaelewi wasukuma kabisaaaa, huyu jamaa wanasengerema wanatakiwa wampe kubwa tu aishie
 
ipo kwenye mwananchi ya leo mkuu
Asante mkuu,ila nilikuwa namaanisha wasishie hapo leo, waandike na kuandika kwa jinsi sakata hilo linavyoendelea ili kumnusuru huyo mlinzi na wengine wanaokumbwa na majanga ya kijinga kama hayo
 
Papa Benedict XVI alianguka na kuumia miezi michache iliyopita akavunjika kiwiko (wrist) cha mkono.

Alipofika Hospitali yaani MOI ya kule alikuta foleni ya watu. Kwenye foleni wanamjua Papa alivyo muhimu duniani na wote walimpisha.

Yeye mwenyewe akasema waendelee kukaa kwenye foleni hadi ilipofika zamu yake akaingia kutibiwa.

Ni mara ngapi Nyerere amepiga picha anasubiri foleni ya kupiga kura au hata kuandikisha kupiga kura.

Huyu mtoto wa juzi Ngeleja ana umuhimu gani kuliko hao niliowahorodhesha.

Kwanza lafudhi yake bado ya kisukuma pamoja na kukaa kote mjini na kutembelea nchi mbalimbali.
 
Back
Top Bottom