Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Nusura nipost sehemu ya mwisho ya "Kumbatio" ndipo nimekutana na email ndefu yenye kunilalamikia na kunidokeza kuwa kisa hiki kimetokana na kisa cha kweli na kuwa yawezekana nimesimuliwa na mtu wa karibu wa wahusika. Na kwamba licha ya kujaribu kugeuza mambo mbalimbali kisa hicho ni kweli kimemkuta bosi fulani ambaye ni mwanasiasa maarufu.
Baada ya kuandika kwa kirefu, mwandishi (ambaye anajina la huyo bosi na nikitaja tu wote mtamjua) anamalizia kwa kunipa wito, kunitaka, kuniamuru or whatever have you...
Baada ya kurudia rudia kijibarua hicho nimejikuta nina utata na kuanza kujiuliza maswali kwani ni kweli kisa hicho kimevuviwa na tukio la kweli japo simulizi lake ni la kutunga na manjonjo yamo humo humo lakini kwa asilimia 100 jina la huyo bwana halihusiani na kisa labda matukio yamefanana tu. Lakini hata hivyo kama anaamini ndiyo yeye basi ninajikuta kwenye utata. KUendelea na kumalizia au kujaribu kukibadilisha zaidi na kuruka simulizi la Jumamosi au kulibadilisha kabisa?
Naomba mpige kura kwa kuzingatia kiwango cha ukweli kilichomo ndani. Nataka nifikir uamuzi ifikapo J'pili ili kama kisa kitakuwa kimeisha niwaambia au kama ndio nikiposti kiishe niwapostie maana Jambo limezua Jambo!
Baada ya kuandika kwa kirefu, mwandishi (ambaye anajina la huyo bosi na nikitaja tu wote mtamjua) anamalizia kwa kunipa wito, kunitaka, kuniamuru or whatever have you...
....Ninakusihi usiendelee kubandika simulizi lako hilo kwani linanikumbusha machungu ambayo nimeyapitia na limeshazua mtafafuru kati yangu na baadhi ya marafiki ambao walikuwa wanajua undani wa kilichotokea kati yangu na mke wangu. Kilichotokea "Jumamosi" hakifai kusimuliwa wala kujulikana kwani ni ndiyo nimefanya makosa na nimeyalipia mara mia moja na pamoja na hayo tuliamua kuendelea kuwa pamoja.
Kukisoma kisa chako hadi kilipofikia kimeshatonesha madonda mengi na kurudisha kumbukumbu ya matukio ambayo tulishaamua kuyaacha yapite. Chonde, tafadhali mwanakijiji pamoja na kutumia mbinu zote za kiuandishi kuwaficha wasomaji wako watu wanaofahamu kisa chetu watagundua mapema kabisa kuwa ni nani anazungumziwa.
Naomba usimalizie hicho kisa na niko tayari kuzungumza nawe kwa herufi kubwa ili tuweze kuyamaliza kiutuzima. Tayari nimeshaabika siko tayari kuabika tena hasa kama magazeti ya udaku yatakipata kisa chako. ....