Kiruka njia??

Babu DC sidhani kama itakua sahihi kwasababu huyo sio kama ni hulka yake kuhamahama bali anakua analazimika kutokana na hao anaokutana nao.
 
Lizzy,

Naona unalenga kwenye kitufe chenyewe. Nimekuwa nikishangazwa na kauli za akina mama (zaidi kuliko wanaume) kwamba wako tayari kunyanyaswa ili mradi wasijeitwa viruka njia.

Imeniuma sana kwani nashindwa kuelewa kwa nini mtu ajali zaidi mambo ya watu kuliko mateso anayopata kwenye ndoa au mahusiano!!
 
BAbu yangu Kiruka njia nadhani ni mtu ambaye hajatulia, hashikiki, .............sijui kama mcharuko au mapepe vinawezatumika kwa mtu wa aina hii

Tofauti kidogo, mcharuko na mapepe wanaweza kuwa sio viruka njia
Kiruka njia ni zaidi ya hao
 
Lizzy,

Naona unalenga kwenye kitufe chenyewe. Nimekuwa nikishangazwa na kauli za akina mama (zaidi kuliko wanaume) kwamba wako tayari kunyanyaswa ili mradi wasijeitwa viruka njia.

Imeniuma sana kwani nashindwa kuelewa kwa nini mtu ajali zaidi mambo ya watu kuliko mateso anayopata kwenye ndoa au mahusiano!!

Babu DC lawama zote ziiendee jamii yetu kwa kupenda kuhukumu bila kujua undani wa mambo!!!

Kuna wale watu ambao maisha yao yote yanaendeshwa na “nitaonekanaje“..“nitafikiriwaje“..“watasemaje“ na hawa ndio victim wa hukumu zitolewazo hovyo na jamii.Mtu yuko radhi kua na manundu kila siku alimradi familia/majirani/marafiki na jamii kwa ujumla wasimhukumu ndivyo sivyo!!!
 
Babu DC lawama zote ziiendee jamii yetu kwa kupenda kuhukumu bila kujua undani wa mambo!!!

Kuna wale watu ambao maisha yao yote yanaendeshwa na "nitaonekanaje".."nitafikiriwaje".."watasemaje" na hawa ndio victim wa hukumu zitolewazo hovyo na jamii.Mtu yuko radhi kua na manundu kila siku alimradi familia/majirani/marafiki na jamii kwa ujumla wasimhukumu ndivyo sivyo!!!

Sawa Lizzy,

Nadhani tatizo langu ni kwamba nabeba maisha yangu na kusonga mbele bila kujali watu wengine wananisema nini ili mradi naamini sina makosa. Sasa mtu anaburuzwa na kutwangwa mateke kila siku kama tuku tuku...Lakini utamkuta kesho anakanda maji na kujiapiza kuwa atafia kwenye hiyo nyumba ili asionekane kiruka njia....Hii ni sawa kweli?????????

Kuna wengine ndio maana wanakaribia kunywa sumu wakiachwa...!!!!
 
Lakini mkuu DC, bila kuruka njia utafikaje upande wa pili wa njia?

Sometimes nadhani tumeabuse maana ya hili neno...Kiruka njia manake ni kitu kinachoruka njia....
Hivi ingekuwa ni 'mruka njia' bado tungekuwa na maana hii tuliyonayo?

ngoja nirudi kuruka njia....
 
Ngoja tusubiri wenye ma ujuzi yao watufafanulie,

Ila ukumbuke kwamba hata ukifanywa Bushoke fulani utulie tu...Vinginevyo utaruka njia!!
 
Sawa Lizzy,

Nadhani tatizo langu ni kwamba nabeba maisha yangu na kusonga mbele bila kujali watu wengine wananisema nini ili mradi naamini sina makosa. Sasa mtu anaburuzwa na kutwangwa mateke kila siku kama tuku tuku...Lakini utamkuta kesho anakanda maji na kujiapiza kuwa atafia kwenye hiyo nyumba ili asionekane kiruka njia....Hii ni sawa kweli?????????

Kuna wengine ndio maana wanakaribia kunywa sumu wakiachwa...!!!!

Babu DC hilo sio tatizo lako bali ni uzuri wako.Au labda naona hivyo kwasababu na mimi ndivyo nilivyo....mtu asiye yaishi maisha yangu hana haki ya kuniamulia kwamba nikienda kulia ndio sahihi na nikienda kushoto mimi sifai!

Tatizo ni kwamba hua hatufikirii kama ni sisi ambao tungekuwepo kwenye situation ya huyo mhukumiwa je tungefanyaje?!Ni rahisi sana kutoa maamuzi ukiwa nje kuliko ukiwa ndani.Na hao wanaruhusu walimwengu wawaamulie maisha kwakweli sina cha kuwasaidia zaidi ya kuwaonea huruma.
 
Ingekuwa ndo harusi naona ningefirisika kwa kuwachangia...Inasikitisha sana!!
 
Hivi watu wanaoruhusiwa na dini au sheria (za mila au nyingienezo) kuwa na multiple relationships nao ni viruka njia??
 
Its not true, unajua hayo majina yanapachikwa kwa watu kimakosa. Mimi sipendi kuyatumia kwa sababu mtu kushuka daladala na kupanda nyingine ana sababu may be alikosea baada ya kwenda mwenge akapanda ya ubungo.

Hata hawa wanaohama kwenye uhusiano wowote wana sababu siyo lazima wakutangazie wewe kwa nini wameachana. Nafikiri tunapoteza muda kumuita mtu kiruka njia wakati hutakaa ujue sababu za yeye kufanya hivyo, hata ungeijua its non of your business.

Baaba ya kukaa chini tubuni miradi ya kufanya tunabuni majina ya kudhalilisha watu. Sorry kama nimemuudhi mtu ndiyo hali halisi.

Usiiku mwema.
 
May be..

Ila nimekutana na jambo ambalo limenifanya nipate msinyao wa ubongo..

Hivi mwanamume akio mke wa kwanza ila akakuta mama mwenyewe ni Tyson..kila siku baba hakosi vinundu usoni. Akaamua kubwaga manyanga na kumpata namba 2..huko nako akukana na moto wa aina nyingine...huyoooo akang'atuka kiaina na kupata namba 3....Labda bahati pia ikawa mbaya na huyo akawa si riziki!!

Au mdada wa watu ambaye ailiuvaa mkenge na kuolewa na jamaa mwenye wake 2 (yeye wa 3) kwa sababu hakumueleza ukweli...Baada ya vitimbi kibao naye akaamua kupanda dala dala ya 2...Hivyo hivyo hadi anafikia chuo cha 4 au 5 (married to 4 or 5 different men)!!!

Hawa watu wana-qualify kuitwa viruka njia???

Njia ukiruka sababu ya obstacle mbeleni au kwa kujisikia mie naona yoote ni kuruka njia... Ila tu nimeshangaa, kweli kiswahili kigumu, siku zoote nilifikiri kiruka njia ni yule ambae ana toka from one person to another bila sababu za msingi, ila sikujua kama wa ndoani yupo katika hilo group...
 
Its not true, unajua hayo majina yanapachikwa kwa watu kimakosa. Mimi sipendi kuyatumia kwa sababu mtu kushuka daladala na kupanda nyingine ana sababu may be alikosea baada ya kwenda mwenge akapanda ya ubungo.

Hata hawa wanaohama kwenye uhusiano wowote wana sababu siyo lazima wakutangazie wewe kwa nini wameachana. Nafikiri tunapoteza muda kumuita mtu kiruka njia wakati hutakaa ujue sababu za yeye kufanya hivyo, hata ungeijua its non of your business.

Baaba ya kukaa chini tubuni miradi ya kufanya tunabuni majina ya kudhalilisha watu. Sorry kama nimemuudhi mtu ndiyo hali halisi.

Usiiku mwema.

Uko sahihi dada,

Shida yangu kubwa si kwa wale wanaotoa majina bali kwa wale wanaoogopa kuchukua maamuzi mazito eti wanayaogopa hayo majina!
 
Njia ukiruka sababu ya obstacle mbeleni au kwa kujisikia mie naona yoote ni kuruka njia... Ila tu nimeshangaa, kweli kiswahili kigumu, siku zoote nilifikiri kiruka njia ni yule ambae ana toka from one person to another bila sababu za msingi, ila sikujua kama wa ndoani yupo katika hilo group...

Kumbe hukujua??

Hao walio kwenye ndoa ndio waoga sana wa hilo jina...Ngoja nikapumzike.. Akili ikurudi nyumbani nitaandaa kisa chenyewe!!
 
DC katika mambo magumu ni kutaka kumuelewesha mtu mwenye hisia tofauti kwako. Mimi kama Carol siwezi ishi na mtu ambaye ni kero kwangu, sina hisia nae, amenidhalilisha kwa namna moja au nyingine. Kuishi ni kuchagua jinsi gani uendeshe maisha yako wewe kama wewe. Ukianza kuangalia nini community inavyokuchukulia nafikiri utakuwa unapoteza muda wako.

Binadamu ana kawaida ya kufanya kila wazo lake analofikiria kwa mtu au kwake mwenyewe kuwa sahihi. Ebu DC nenda pale mtaa wa OHIYO waulize kwa nini wanasimama pale. Kila mmoja akianza kukupa historia ya maisha yake utalia machozi. Ila tayari kabla ya kujua nini tatizo lao, mlishawapachika majina mengi tu (malaya, Changudoa, maharage ya mbeya etc).

Kila kitu kia sababu siyo wote wanafanya vitu fulani kwa utashi wao wenyewe ni hali tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom