Kipindi kigumu jimboni Kawe

Kuna mengi ambayo ameyafanya huyu mbunge:
1. Barabara toka Millenium Tower, kupitia Chekechea ya Hindu Mandal hadi Shoppers Plaza inawekwa lami.

2. Daraja la njia fupi toka Rose Garden kwenda School of Journalism Mikocheni limejengwa.

3. Amesaidia kuhamisha soko la Tegeta na Stendi ya Daladala Tegeta toka barabarani kwenda sehemu nzuri zaidi.

4. Amesimamia vema ujenzi wa barabara toka Tegeta Nyuki hadi Bahari Beach kiwango cha lami. Ujenzi umekamilika.

5. Amesimamia vema ujenzi wa New Bagamoyo road na upgrade ya Old Bagamoyo Road.

6. Amepambana sana na uvamizi na ubadilishaji holela wa matumizi ya ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya kijamii (KUNDUCHI, WAZO, MADALE n.k.) na kubatilishwa na kupewa watu wenye pesa. Katika hili kikwazo ni madiwani (wa CCM), ambao ndio wawakilishi wa maeneo husika kwenye vikao vya halmashauri pamoja na maafisa wa Halmashauri (inaongozwa na CCM) ambao ndio watekelezaji na ambao hawampi ushirikiano. Hapa ushirikiano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ulihitajika sana.

7. Amekusanya data za viwanda na mahoteli yote ya jimboni kwake ili kuhakikisha wanalipa kod inayoongeza pato kwa shughuli za maendeleo ya jimbo la Kawe.

8. Amekuwa anakutana na wananchi na kusikiliza kero zao na kupata maoni yao. Angalia video hii

9.Amepigania chuo cha IMTU Kilikuwa kinatoza ada kwa dola za marekani sasa kinatoza kwa fedha za TZ, pia ada ya imeshuka na kuwa fixed.

10. Eneo la Tegeta amesimamia ujenzi wa Shopping mall ya kisasa. Imekamilika.

11.
Amehamasisha na kuamsha ari ya vijana na kina mama katika kushiriki kwenye siasa na ameonyesha umahiri na kujiamini kwa hali ya juu jambo ambalo lemesaidia sana kubadili mtazamo wa wamama na wasichana walio wengi kwamba wakina dada nao wanaweza.

12. Ameshiriki
unanzishaji na uendelezaji wa vikundi vya kina mama Kawe.

13. Amekuwa na mchango mzuri sana katika kujadili miswada bungeni, na katika kuibua hoja za kitaifa.

Na mengine mengi sana mnisaidie kuongeza.

Ameyafanya yote haya licha ya juhudi za makusudi za Halmashauri (ambao ndio wanapokea fedha za maendeleo za jimbo) na madiwani (ambao ndio wawakilishi wa wananchi wa kata zao kwenye halmashauri) kumkwamisha.

Nahisi nyuzi nyingi zinaletwa hapa kwa sababu wanataka kuona juhudi za makusudi za kumkwamisha zimefanikiwaje.

By the way, kati ya wabunge wote wa Dar hakuna ambaye amezorota kama Abas Mtemvu. Mbona haanzishiwi threads nyingi kama Mdee? Na kuna thread ipo nimejaribu kwa makusudi kupost ili iwe juu tuone kama kweli watu wako objective lakini hakuna anayepost kitu kule.

Fikiria vema!

hivi Dr. Ndungulile nae ana cha kujivunia?
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu wana special interest na Halima Mdee hata kama angefanya nini. Kuna huyu Mafilili

Tarehe 06.03.2012 alianzisha thread hii: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-mdee-njoo-utuokoe-kunduchi-machimboni-2.html Nanukuu sentensi ya mwisho: " tulifikiri wewe utakuwa Mbunge bora kumbe AFADHALI wakati wa RITA MLAKI alikuwa karibu na wapiga kura."
Mbunge wetu Halima Mdee, kumbuka maneno yako matamu kama asali uliyotoa kipindi cha uchaguzi hatimaye wana Kawe wakakupa UBUNGE. Umepita mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu umekabidhiwa dhamana ya kutuwakilisha MJENGONI Dodoma.

Twakushangaa sana unakuwa mkimya kipindi ambacho wananchi twahitaji utetezi wako. Nachukua fursa hii kukukumbusha wapiga kura wako wa Kunduchi Machimboni twapata shida, kuanzia wachimba kokoto, mama nitilie, wauza kokoto na wenye nyumba katika eneo husika twanyanyaswa na uongozi wa wilaya na mkoa. WEWE UPO KIMYA tukuelewaje??

Tulitegemea mara baada ya Mkuu wa Mkoa kutoa tamko la kufunga machimbo, wewe ungetoa msimamo wa kuunga wapiga kura. Mbaya zaidi ofisini haupatikani KULIKONI Mheshimiwa, ama kweli sikio la kufa halisikii dawa, tulifikiri wewe utakuwa Mbunge bora kumbe AFADHALI wakati wa RITA MLAKI alikuwa karibu na wapiga kura.

Tafadhali njoo utusikilize na kutuunga mkono ili tusihamishwe kwa nguvu na FFU.

Tarehe 18.05.2012 alianzisha thread hii: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/266207-mheshimiwa-halima-mdee-kulikoni.html
Ni masikitiko kwa wana Kawe, Mbunge Halima Mdee umekuwa huonekani jimboni mwako hasa majira ya mchana. Umekuwa ni mtu wa kutoka alfajiri ili ukimbie kuonana na wapiga kura, unarudi usiku wa manane.
Kwa kweli waliokushauri uchukue ubunge wa jimbo walifanya makosa makubwa, uwezo wako ni kuwa MBUNGE wa Viti Maalum. Tunakushangaa zimebaki siku chache kwenda kikao cha BAJETI, Dodoma, HAUJATHUBUTU kupita kwa wapiga kura kukusanya maoni ili uyawakilishe BUNGENI. Kwa taarifa yako TUMEKUCHOKA SANA pamoja na chama chako!!

Tarehe 14.06.2012 alichangia post hii: Note red coloured text
Halima Mdee + John Mnyika = Hodari wa kupiga maneno, UFUATILIAJI ni ZERO. Wabunge hawa wameshajijua 2015 hawarudi mjengoni hivyo wanashughulika na mambo yao binafsi kuliko kusikiliza na kufanyia kazi kero za wananchi.

Wananachi wa ubungo wanajuta kumpa kura Mnyika, wa Kawe wanasema afadhali enzi za Rita Mlaki alikuwa msikivu na mfuatiliaji

Tarehe 1.7.2012 alianzisha thread: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/286150-mheshimiwa-halima-mdee-karibu-tegeta-namanga.html
Pole kwa majukumu ya mjengoni Dodoma, mie mpiga kura wako nachukua fursa hii adimu kukuomba uje sehemu husika, Tegeta Namanga utukisikilize namna tunavyoteseka kuishi nje katika kipindi hiki cha baridi baada ya nyumba zetu kubomolewa na Big Bon, tafadhali njoo haraka!
Leo tarehe 15.09.2012 ameanzisha tena thread hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/323991-kipindi-kigumu-jimboni-kawe-4.html
Na ninanukuu maneno ya mwisho ya Mafilili: "Kwa kweli wakazi wa jimbo la Kawe tupo katika kipindi tete tunamkumbuka RITA Mlaki ambaye alikuwa karibu na wapiga kura."

Naona MAFILILI inawezekana ni campaign manager wa Rita Mlaki na anaanza mapema sana kumpigia kampeni.

Lakini pia swali kwako Mafilili: Kwa nini usiendeleze nyuzi zako za zamani za Halima Mdee na karibu kila mwezi unatuanzishia threads mpya.

Wananchi wengine wa Kawe tunaona anayoyafanya. Chungulia kidogo hapa chini. Na kwa taarifa yako unampromote kwa kumuandama.

Kuna mengi ambayo ameyafanya huyu mbunge:
1. Barabara toka Millenium Tower, kupitia Chekechea ya Hindu Mandal hadi Shoppers Plaza inawekwa lami.

2. Daraja la njia fupi toka Rose Garden kwenda School of Journalism Mikocheni limejengwa.

3. Amesaidia kuhamisha soko la Tegeta na Stendi ya Daladala Tegeta toka barabarani kwenda sehemu nzuri zaidi.

4. Amesimamia vema ujenzi wa barabara toka Tegeta Nyuki hadi Bahari Beach kiwango cha lami. Ujenzi umekamilika.

5. Amesimamia vema ujenzi wa New Bagamoyo road na upgrade ya Old Bagamoyo Road.

6. Amepambana sana na uvamizi na ubadilishaji holela wa matumizi ya ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya kijamii (KUNDUCHI, WAZO, MADALE n.k.) na kubatilishwa na kupewa watu wenye pesa. Katika hili kikwazo ni madiwani (wa CCM), ambao ndio wawakilishi wa maeneo husika kwenye vikao vya halmashauri pamoja na maafisa wa Halmashauri (inaongozwa na CCM) ambao ndio watekelezaji na ambao hawampi ushirikiano. Hapa ushirikiano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ulihitajika sana.

7. Amekusanya data za viwanda na mahoteli yote ya jimboni kwake ili kuhakikisha wanalipa kod inayoongeza pato kwa shughuli za maendeleo ya jimbo la Kawe.

8. Amekuwa anakutana na wananchi na kusikiliza kero zao na kupata maoni yao. Angalia video hii

9.Amepigania chuo cha IMTU Kilikuwa kinatoza ada kwa dola za marekani sasa kinatoza kwa fedha za TZ, pia ada ya imeshuka na kuwa fixed.

10. Eneo la Tegeta amesimamia ujenzi wa Shopping mall ya kisasa. Imekamilika.

11.
Amehamasisha na kuamsha ari ya vijana na kina mama katika kushiriki kwenye siasa na ameonyesha umahiri na kujiamini kwa hali ya juu jambo ambalo lemesaidia sana kubadili mtazamo wa wamama na wasichana walio wengi kwamba wakina dada nao wanaweza.

12. Ameshiriki
unanzishaji na uendelezaji wa vikundi vya kina mama Kawe.

13. Amekuwa na mchango mzuri sana katika kujadili miswada bungeni, na katika kuibua hoja za kitaifa.

Na mengine mengi sana mnisaidie kuongeza.

Ameyafanya yote haya licha ya juhudi za makusudi za Halmashauri (ambao ndio wanapokea fedha za maendeleo za jimbo) na madiwani (ambao ndio wawakilishi wa wananchi wa kata zao kwenye halmashauri) kumkwamisha.

Nahisi nyuzi nyingi zinaletwa hapa kwa sababu wanataka kuona juhudi za makusudi za kumkwamisha zimefanikiwaje.

By the way, kati ya wabunge wote wa Dar hakuna ambaye amezorota kama Abas Mtemvu. Mbona haanzishiwi threads nyingi kama Mdee? Na kuna thread ipo nimejaribu kwa makusudi kupost ili iwe juu tuone kama kweli watu wako objective lakini hakuna anayepost kitu kule.

Fikiria vema!
 
Last edited by a moderator:
sasa kwanini tunapenda kujustfy udhaifu wa mtu kwa kulinganisha na udhaifu wa Jk? Nafikiri mleta mada kaeleweka,tatizo hapa baadhi tunapenda au kuchukia mada bila kuwa na sababu.
"sikiliza shauri na kupokea mafundisho upate hekima ya kukufaa siku zijazo" (Meth 19:20)

Yeye ndo dhaifu namba moja,one,moko au wahed katika nchi hii
 
Mkuu mafilili wewe unakaa wapi? Kunduchi Machimboni kama unavyoonesha hapa,
Mbunge wetu Halima Mdee, kumbuka maneno yako matamu kama asali uliyotoa kipindi cha uchaguzi hatimaye wana Kawe wakakupa UBUNGE. Umepita mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu umekabidhiwa dhamana ya kutuwakilisha MJENGONI Dodoma.

Twakushangaa sana unakuwa mkimya kipindi ambacho wananchi twahitaji utetezi wako. Nachukua fursa hii kukukumbusha wapiga kura wako wa Kunduchi Machimboni twapata shida, kuanzia wachimba kokoto, mama nitilie, wauza kokoto na wenye nyumba katika eneo husika twanyanyaswa na uongozi wa wilaya na mkoa. WEWE UPO KIMYA tukuelewaje??

Tulitegemea mara baada ya Mkuu wa Mkoa kutoa tamko la kufunga machimbo, wewe ungetoa msimamo wa kuunga wapiga kura. Mbaya zaidi ofisini haupatikani KULIKONI Mheshimiwa, ama kweli sikio la kufa halisikii dawa, tulifikiri wewe utakuwa Mbunge bora kumbe AFADHALI wakati wa RITA MLAKI alikuwa karibu na wapiga kura.

Tafadhali njoo utusikilize na kutuunga mkono ili tusihamishwe kwa nguvu na FFU.

Au Tegeta Namanga kama unavyosema hapa
Pole kwa majukumu ya mjengoni Dodoma, mie mpiga kura wako nachukua fursa hii adimu kukuomba uje sehemu husika, Tegeta Namanga utukisikilize namna tunavyoteseka kuishi nje katika kipindi hiki cha baridi baada ya nyumba zetu kubomolewa na Big Bon, tafadhali njoo haraka!

Au unapopiga propaganda za CCM unaruhusiwa kutumia uongo kwa kuwa unadhani wananchi ni wajinga?
 
Ivi wapiga kura kujadili utendaj usioridhisha wa wabunge wao, ni dhambi?,au kwa sabab anaeonekana kusemwa ni-m4c basi hapo hamna mada????mh!!!!,kaz ipo!
 
Ivi wapiga kura kujadili utendaj usioridhisha wa wabunge wao, ni dhambi?,au kwa sabab anaeonekana kusemwa ni-m4c basi hapo hamna mada????mh!!!!,kaz ipo!

Wameoneshwa kuwa kuna vitu vinafanyika:

Kuna mengi ambayo ameyafanya huyu mbunge:
1. Barabara toka Millenium Tower, kupitia Chekechea ya Hindu Mandal hadi Shoppers Plaza inawekwa lami.

2. Daraja la njia fupi toka Rose Garden kwenda School of Journalism Mikocheni limejengwa.

3. Amesaidia kuhamisha soko la Tegeta na Stendi ya Daladala Tegeta toka barabarani kwenda sehemu nzuri zaidi.

4. Amesimamia vema ujenzi wa barabara toka Tegeta Nyuki hadi Bahari Beach kiwango cha lami. Ujenzi umekamilika.

5. Amesimamia vema ujenzi wa New Bagamoyo road na upgrade ya Old Bagamoyo Road.

6. Amepambana sana na uvamizi na ubadilishaji holela wa matumizi ya ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya kijamii (KUNDUCHI, WAZO, MADALE n.k.) na kubatilishwa na kupewa watu wenye pesa. Katika hili kikwazo ni madiwani (wa CCM), ambao ndio wawakilishi wa maeneo husika kwenye vikao vya halmashauri pamoja na maafisa wa Halmashauri (inaongozwa na CCM) ambao ndio watekelezaji na ambao hawampi ushirikiano. Hapa ushirikiano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ulihitajika sana.

Mchango kwenye Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Tarehe 16/08/2011

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nukushukuru kwa dhati kwa kunipa fursa hii. Lakini vile vile siungi mkono hoja si kwa sababu sina imani na Waziri wala Naibu Waziri, hapana. Ni kwa sababu licha ya wao kuwa na nia njema ya kufanya kazi mbali ya kuwa na fedha finyu. Lakini nadhani hapati ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mzungumzaji mmoja nadhani ni mama Kikwembe if I am not mistaken wakati nimetoka akapiga mawe kidogo. Lakini nimhakikishie kwamba siwezi kuzungumza kitu ambacho sina ushahidi nacho. Aliniambia nimtajie majina ya Madiwani waliokwenda Marekani siku nne. Nitamtajia Kata, majina itakuwa kazi yake yeye kutafuta. Kuna Diwani wa Kata ya Magamba, kuna Diwani wa Kata ya Sitalike, kuna Diwani Viti Maalum Karema na kuna Diwani Viti Maalum Uruwira. Sasa majina akayatafute yeye.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini inasikitisha. Unapoona Mbunge mnajaribu kutetea eneo lake yeye, anakuja ana-crash down pasipo hoja za msingi na kwa sababu ya uvivu wa kusoma. Juzi kwenye SADC Forum iliyokwisha tu majuzi. Moja ya ajenda ilikuwa ni Land Crabbing Africa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wazungu huko walishamaliza kwao, wanakuja kurudisha ukoloni. Kibaya zaidi mtaalam wa Canada, mzungu huyo huyo akaenda na mikataba mizito hivi na mkataba uliotolewa mfano, kama West Case Scenario ni mkataba wa Agrisoil Tanzania. Nasikitika jana namsikia Mbunge mmoja kutoka Kigoma, anasema eti wenzake wa Kigoma wameshindwa kutumia ardhi, wakati kuna hekta 80,000 wameshindwa kutumia ardhi, kwa hiyo walete wawekezaji. Tena msomi mzuri, inasikitisha. Kwa hiyo, niseme hili la suala la Agrisoil mbali na
upungufu wake wote na upuuzi wake wote umekiuka Sheria ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria zetu ziko wazi kabisa na hii namwambia Mheshimiwa Waziri Mkuu asipoli-handle vizuri anaweza akaanguka nalo. Ataanguka nalo kabisa. Kwa sababu kuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba Ofisi yake ilihusika. Kwa hiyo tutumie busara tuokoe nchi. Sheria ya Ardhi iko wazi. Muwasaidie Mawaziri, mumsaidie Naibu Waziri. Sheria ya Ardhi iko wazi kabisa. Mgeni ama mwekezaji anapotaka kuja kumiliki ardhi ya nchi imeeleza wazi, kifungu cha 19, Kifungu cha 20(i) hadi 20(iv) mabadiliko ya 2004. Very clear na imesema wazi kabisa kama kuna joint venture inamhusu raia na Sheria ya Uraia haijatambua kampuni, haijatambua Halmashauri, haijatambua kitu kingine chochote raia mmoja mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mtuambie huko Rukwa ni raia gani anamiliki hekta laki mbili na kitu. Huko Lugufu Kigoma kuna raia gani anamiliki hekta 80,000 ambaye anaingia ubia sasa ili ule mchakato wa kufuata TAC usifuatwe. Naomba tuache ushabiki. Hii ni crisis?
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza taarifa yake siitaki. Lakini pili, mimi mwenyewe hivi kiwanja changu sina Hati Miliki. Hati Miliki siyo issue.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tatu, kuna kitabu cha makubaliano waliyoingia baina ya Halmashauri na Agrisoil na mkitaka nitaleta kwenye Meza yako. Wao wenyewe hapa wamekiri, kuna hivyo vitu vinavyoendelea Bungeni. Kwa hiyo, kama nyinyi ambao ndiyo mnatakiwa mtekeleze Sheria mnakuja hapa mnatetea wahalifu, tunakoelekea kama nchi kunatisha. Hatutafuti umaarufu wa kisiasa, umaarufu upo tayari, tunataka kujenga nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nirudi Jimboni maana nilisimama kwa ajili ya Jimbo. Lakini alinivurugua system Mama Kikwembe ikabidi nirudi kule ambacho sikutaka kurudi.

Suala la kwanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunilinda. Katika Jimbo langu na nadhani katika Majimbo ya Dar es Salaam ndiyo yanaongoza katika migogoro ya ardhi. Naomba Mheshimiwa Naibu Waziri na Mheshimiwa Waziri suala la Mabwepande. Miaka minne iliyopita mlikwenda pale, mkawaambia wananchi wasiendeleze maeneo yao. Mkawalipa wengine kama 160. Mheshimiwa Naibu Spika, namwonea huruma sana kwa sababu 2015 sijui kama atarudi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la Mabwepande. Naomba na muda wangu huu pia uzingatiwe. Miaka minne iliyopita Serikali ilikwenda kufanya tathmini na ninavyozungumza hivi pia na katika mfumo huo huo nazungumzia eneo la Kwembe kwenye Jimbo la Mheshimiwa Mnyika. Nilikwenda kufanya tathmini, wananchi wakaambiwa wasiendeleze maeneo yao na kwamba Serikali ina mipango ya kuja kulichukua lile eneo kwa ajili ya matumizi mapya. Jimbo la Ubungo lilikuwa ni kwa ajili ya kujenga Chuo cha Muhimbili kwa mantiki ya Campus nyingine. Lakini vile vile Mabwepande kulikuwa kuna chuo cha IFM na miradi mingine 20,000 ya viwanja.

Mheshimiwa Naibu Spika, imepita zaidi ya miaka minne. Wananchi hawajui mustakabali wao. Waliolipwa ni wananchi 160 tu kwa kipindi hicho zaidi ya wananchi 600, hawajui mustakabali wao ukoje. Lakini vile vile kwa upande wa Kwembe Serikali iliwaahidi wananchi kuwalipa pamoja na thamani ya ardhi na siyo mimea, kwa sababu pia Sheria zinasema hivyo na wananchi wa Kwembe hawana tatizo la kuhama. Tatizo lao la msingi ni ile haki yao waliyokubaliana kimsingi walipwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Mabwepande tunavyozungumza leo hii na nakumbuka wakati wa Kamati, nilivyokuja kwenye Kamati yao, nilimwambia kuna uvamizi wa hali ya juu unaendelea. Wananchi ambao waliiamini Serikali yao hawakulima, hawakujenga kwa sababu waliambiwa kwamba kuna mipango ya maendeleo, wakaa pembeni leo wamegeuka wakimbizi kwenye ardhi yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa namwomba Mheshimiwa Waziri kwa sababu nimeshapiga kelele katika Halmashauri, nimekwenda kwake kwa njia ya barua. Lakini hali kule ni mbovu. Naomba Serikali ichukue hatua. Mimi kama Mbunge wa Kawe silindi mvamizi hata mmoja. Wasije watu wakawa huko kwa maslahi yao, wanasema Mheshimiwa Halima Mdee anatuunga mkono. Sijatuma mvamizi yoyote akavamie eneo,nataka haki itendeke. Kwa hiyo, naomba suala la Mabwepande na suala la Kwembe naomba myafanyie kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini suala lingine Mheshimiwa Waziri kuna hili suala la Boko Dovya katika Shamba la Bwana Somji. Kuna taarifa hapa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kipindi kile alipokuwepo Mheshimiwa Chiligati, alikiri kwamba hili tatizo limekwisha. Serikali itachukua lile eneo kwa ajili ya kugawiwa kwa wananchi. Mpaka leo hakuna kinachoeleweka Somji anaendelea kuwasumbua wananchi ambao wako kwenye maeneo hayo. Kwa hiyo, naomba tafadhali tafadhali niweze kupata ufafanuzi kwa haya masuala.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini lingine ni suala la Chasimba. Hili suala siyo dogo kama watu ambavyo wanataka walifikirie. Ni suala ambalo linahusisha wananchi zaidi ya 10,000. Ni suala ambalo ushahidi wake uko wazi na nimeeleza kwa kina sana kwenye hotuba yangu. Lakini nitalizungumza hapa. Inawezekana Serikali mkaja na scenario kwamba hili suala ni la zamani, lilienda Mahakamani na limeamualiwa Mahakamani. Kwa hiyo, wananchi waondoke, naomba mtumie busara. Nina hukumu ya Mahakama hapa. Nina documents hapa nitamletea Mheshimiwa Waziri zinazoonesha jinsi kijiji kilivyosajiliwa zinazoonesha kwamba mmiliki wa kiwanda hamiliki viwanja vyote vitatu kwa mantiki ya moja, nne na saba. Lakini nimesoma hukumu hapa, inasema naomba ninukuu kidogo: "It is the respondent case from a total twelve witnesses that the village officials of Boko".Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba muda wangu kidogo, kengele ya kwanza? It is the respondent case from a total of twelve witnesses that the village officials of Boko and Tegeta were contacted with the view of securing more land by organizing meetings with the villages. At the end of the day the respondent managed to buy a number of villages by wealth composition. Hukumu sababu katika hii kesi respondent alikuwa ni TUGHE. Kwa sababu ilikuwa ni Mahakama ya juu kabisa. Wanakiri kwamba walioweza ku-manage ni a number of villages sio all of the villages. Ndiyo maana nashukuru tu kwa maana ya Mheshimiwa Ole-Medeye. Nashukuru sana. Wananchi waliokuwepo pale ni watu wazima, tofauti na maeneo mengine ya uvamizi, unaona ni vijana vijana tu wamekuja juzi. Naomba Serikali iliangalie hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, Lakini kesi ambayo ilikuwa inahusu watu takriban 1,000 ikaamuliwa on technical grounds kwamba linapokuja suala la ardhi, hatuangalii suala la representative's suit hairuhusiwi. Ikiwa ni Mahakama ya Rufaa Court of Appeal, haki za maelfu za wananchi zikaminywa simply because kwa uelewa wao labda mdogo waliamua wenzao 13 wakawakilishe Mahakamani na kati ya wenzao 13 waliokwenda kuwakilisha Mahakamani still walishindwa kuthibitisha wanne kati yao kwamba walilipwa fidia. Kwa hiyo, naomba Waziri asiwe mkali, naomba mtumie busara. Nawaombea wapiga kura wangu. Najua kuna haki imeminywa sehemu. Najua kuna interest za watu zinataka kuwaumiza watu maskini.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasikia wanataka kuhamishiwa Mabwepande. Sisi hili hatuliafiki. Tunajua eneo la kiwanda ni kubwa. Wakitaka kujipanua wataacha chenji. Tunaomba muwasaidie wananchi na niwaambie kwa hili, maana Madiwani wa Kata hizo mbili ni wa CCM. Moja, tumesema iwe jua, iwe mvua, sisi tutakufa na wananchi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hatufanyi uchochezi. Lakini nadhani natumia lugha laini sana. Ukienda Chasimba mwenyewe, sijui! Ole Medeye, tulikwendanae na anajua zaidi, naomba tuwasaidie wananchi wetu. Kuna siasa hapa, kuna vyama vyote viko kule, tuweke utu kwanza; eneo lipo la kutosha, la msingi ni kwenda kufanya vikao na wananchi, kujua eneo la kiwanda liko wapi, wananchi wanaweza wakakaa wapi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mwisho, hivi viwanja 20,000. Kunakuwa kuna tatizo kwamba, Wizara kwa nia njema kabisa mnaandaa miradi mbalimbali. Lakini tatizo ni kwamba, miradi hiyo haimilikishwi kwa wananchi ili waweze kujua viwanja vya wazi ni vipi? Viwanja vya shule ni vipi? Viwanja vya huduma za jamii ni vipi? Matokeo yake viwanja hivi vimegeuka kuwa sehemu ya Wenyeviti wa Mitaa kupata kula yao! Kwa hiyo, naomba katika miradi yoyote ambayo mliifanya, mwende mkai-review, muangalie maeneo ya wazi, maeneo ya umma ni yapi? Myafanye yawe wazi, ili wananchi kwenye maeneo hayo wawe walinzi wa ile rasilimali. Bila kufanya hivyo!

Mheshimiwa Naibu Spika, leo sheria haitambui kama Mwenyekiti wa Mtaa, anaweza akagawa eneo, lakini nitakwambia huko Dar-es-Salaam, wanagawa kwa kwenda mbele! Wakati nyie mnatoa maagizo huku, Wenyeviti wa Mitaa na baadhi ya Madiwani ambao sio waaminifu wanaendelea kuuza maeneo kwa kushirikiana na watu wa Manispaa ambao sio waaminifu. Kwa hiyo, naomba haya myaangalie kwa makini.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho kabisa na ambalo pia sio la muhimu, ni viwanja vya wazi Mkoa wa Dar-es-Salaam. Tunajua mna changamoto kubwa kwa sababu, wengi ambao wamewahi kupewa hayo maeneo ya wazi, hususan katika maeneo strategic, ni wakubwa! Wengine wamejenga ma-bungalow yao! Sasa naomba leo mtuhakikishie wakati mnahitimisha, ile taarifa iliyotolewa na Kamati iliyoundwa na Mheshimiwa Lukuvi, mtaitekeleza kwa ukamilifu wake na ndani ya kipindi gani? Nakuhakikishia Mheshimiwa Tibaijuka, ukiniahidi hilo nitakuona kweli wewe ule moto wako unaendelea. Ukiwa unasitasita nitajua yale ambayo yanasemwa, ulianza kwa speed wenzio wakakuminya! Tunakuamini mama, namwamini Mheshimiwa Naibu Waziri sana kama ambavyo namwamini yeye sana, hii sekta ndio uhai wa nchi. Hii sekta tukiipuuza na naiambia Serikali, tukiipuuza watoto wetu, wajukuu zetu watakuja kuchinjana na hatutaki tutengeneze Tanzania ya kuchinjana!

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana.

7. Amekusanya data za viwanda na mahoteli yote ya jimboni kwake ili kuhakikisha wanalipa kod inayoongeza pato kwa shughuli za maendeleo ya jimbo la Kawe.

8. Amekuwa anakutana na wananchi na kusikiliza kero zao na kupata maoni yao. Angalia video hii

9.Amepigania chuo cha IMTU Kilikuwa kinatoza ada kwa dola za marekani sasa kinatoza kwa fedha za TZ, pia ada ya imeshuka na kuwa fixed.

10. Eneo la Tegeta amesimamia ujenzi wa Shopping mall ya kisasa. Imekamilika.

11.
Amehamasisha na kuamsha ari ya vijana na kina mama katika kushiriki kwenye siasa na ameonyesha umahiri na kujiamini kwa hali ya juu jambo ambalo lemesaidia sana kubadili mtazamo wa wamama na wasichana walio wengi kwamba wakina dada nao wanaweza.

12. Ameshiriki
unanzishaji na uendelezaji wa vikundi vya kina mama Kawe.

13. Amekuwa na mchango mzuri sana katika kujadili miswada bungeni, na katika kuibua hoja za kitaifa.

Na mengine mengi sana mnisaidie kuongeza.

Ameyafanya yote haya licha ya juhudi za makusudi za Halmashauri (ambao ndio wanapokea fedha za maendeleo za jimbo) na madiwani (ambao ndio wawakilishi wa wananchi wa kata zao kwenye halmashauri) kumkwamisha.

Nahisi nyuzi nyingi zinaletwa hapa kwa sababu wanataka kuona juhudi za makusudi za kumkwamisha zimefanikiwaje.

By the way, kati ya wabunge wote wa Dar hakuna ambaye amezorota kama Abas Mtemvu. Mbona haanzishiwi threads nyingi kama Mdee? Na kuna thread ipo nimejaribu kwa makusudi kupost ili iwe juu tuone kama kweli watu wako objective lakini hakuna anayepost kitu kule.

Si vibaya HM angeingia jamvini au kupitia FB page yake akajibu mwenyewe ili kuclear hizi doubt za wanaKawe coz wengi wanachangia kwa kuponda mada wkt hawaishi Kawe!
 
Si vibaya HM angeingia jamvini au kupitia FB page yake akajibu mwenyewe ili kuclear hizi doubt za wanaKawe coz wengi wanachangia kwa kuponda mada wkt hawaishi Kawe!

Hatumii facebook wala jamiiforum bali anakutana na kufanya mikutano na wananchi kama uonavyo kwenye video hii. Hapo huwaeleza anachofanya na kusikiliza kero zao. Wanaolalamika hawako Kawe na kama wako Kawe hawahudhurii vikao.

Last edited by a moderator:
Mheshimiwa Halima Mdee upo hapooo? Etonyi! Ethina ngolo mbibi, nimwa dengerua. Avache thana.
 
Nyie watu wa Kawe mnavamia viwanja vya watu,mnajenga kwenye mito,mnaziba mikondo ya Bahari mnataka halima atetee upuuzi huo?! please
 
Halima mdee yeye kazi yake ni kushinda saloon kama bunge hamna.Sisi ubungo huku tunajuta kumjua mnyika.Maji mwezi huu hatujui ni nini.
 
Keleleeee wee
Ww badala ufanye kazi kwa bidii na maarifa.... unafanya mapenzi all night asubuhi UNAAMKA KUMPIGIA HALIMA MDEE kelele zako, utabakia poor.....
acha uvivu.....

Wananchi wa jimbo la Kawe tupo katika kipindi kigumu cha kukosa mwakilishi aliye makini bungeni katika kipndi cha mwaka 2010 kuelekea 2015. Mbunge aliyeingia kwa mbwembwe nyingi Halima Mdee amekuwa ni zigo lisilosaidia wapiga kura badala yake anajisaidia mwenyewe.

Tangu amechaguliwa:
1. Hapendi kuitisha mikutano ili kupata mawazo ya wananchi
2. Wananchi wa Madale waliopatwa na mashambulizi ya polisi wamekosa pole na msaada wake
3. Wakazi wa Majipwande wanamlilia kwa kutopata msaada wa mali na faraja toka kwake
4. Mfuko wa Jimbo haujatolewa maelelezo kwa wananchi
5. Kushindwa kutekeleza ahadi zake za kuinua kiuchumi vikundi vya vijana na wanawake
6. Kushindwa kutatua matatizo wanayoyapata vijana wa bodaboda na bajaji

Hizo ni kero chache ambazo zilitakiwa zifanyiwe kazi na mbunge wetu.

Kwa kweli wakazi wa jimbo la Kawe tupo katika kipindi tete tunamkumbuka RITA Mlaki ambaye alikuwa karibu na wapiga kura.
 
Jamani kinachoelezwa kama ni kweli HM ashauriwe na waliokaribu naye, mambo mengine ni madomadogo, ni vema kama mfalme amekaa vibaya akaambiwa.
 
Wananchi wa jimbo
la Kawe tupo katika kipindi kigumu cha kukosa mwakilishi aliye makini
bungeni katika kipndi cha mwaka 2010 kuelekea 2015. Mbunge aliyeingia
kwa mbwembwe nyingi Halima Mdee amekuwa ni zigo
lisilosaidia wapiga kura badala yake anajisaidia mwenyewe.

Tangu amechaguliwa:
1. Hapendi kuitisha mikutano ili kupata mawazo ya wananchi
2. Wananchi wa Madale waliopatwa na mashambulizi ya polisi wamekosa pole
na msaada wake
3. Wakazi wa Majipwande wanamlilia kwa kutopata msaada wa mali na faraja
toka kwake
4. Mfuko wa Jimbo haujatolewa maelelezo kwa wananchi
5. Kushindwa kutekeleza ahadi zake za kuinua kiuchumi vikundi vya vijana
na wanawake
6. Kushindwa kutatua matatizo wanayoyapata vijana wa bodaboda na bajaji

Hizo ni kero chache ambazo zilitakiwa zifanyiwe kazi na mbunge wetu.

Kwa kweli wakazi wa jimbo la Kawe tupo katika kipindi tete tunamkumbuka
RITA Mlaki ambaye alikuwa karibu na wapiga kura.
Mbona mbunge huyohuyo amekuwa akifanya vikao na sisi wa huku Boko NHC almost kila mwezi kujadili namna ya kutatua matatizo kadhaa kama vile barabara na maji! Tafadhali usitukumbushe huyo Ritha Mlaki...
 
kuna watu hutumwa na dhaifu na vijidhaifu kuchafua hali ya hewa na kupima upepo au kutikisa kibiriti.Leo takwimu zimepatikana za kujaza kibiriti na sasa magamba leteni za mkyeku Ritaa Mulyakii
 
mbona mr.ii anaendelea kuimba??????....y iwe nongwa kwa mh:ngonyani????

Kichwa cha panzi.. Kuimba ni tofauti na uchawi.. Unacikia kila ciku serikali inaahidi kuwawekea mazingira bora wasanii wa kuimba ila wafaidi matunda ya kazi zao na serikali kuweza kukusanya kodi.. Uchawi kila ciku serikali inapiga vita.. Hao akina maji marefu ndo wanaosababisha wenye ulemavu wa ngozi kuuawa.. Halafu ati ni mbunge..!
 
mwakilishi aliye makini bungeni
Tangu amechaguliwa:

2. Wananchi wa Madale waliopatwa na mashambulizi ya polisi wamekosa pole na msaada wake
3. Wakazi wa Majipwande wanamlilia kwa kutopata msaada wa mali na faraja toka kwake
6. Kushindwa kutatua matatizo wanayoyapata vijana wa bodaboda na bajaj

.

Hayo ya kwenye red ndiyo yanaondoa umakini wa mbunge? Really!
 
Back
Top Bottom