Kipindi kigumu jimboni Kawe

au ulitaka afanye haya ya magamba?mbunge aweka kando ubunge, afanya kazi ya kutoa `uchawi`mbunge wa jimbo la korogwe vijijini (ccm) , stephen ngonyani maarufu profesa majimarefu, juzi aliweka ubunge wake kando na kurejea kazi yake ya uganga kwa kutoa ‘wachawi’ katika kijiji cha kwemazandu.mbunge huyo alifanya kazi hiyo baada ya kuhudhuria mkutano wa kijiji uliopitisha maamuzi ya kumtimua mmoja wa wanakijiji wao kwa tuhuma za kishirikina.akizungumza na nipashe kwa simu kutoka korogwe, alisema alilazimika kufanya kazi hiyo wakati wa mkutano wa halmashauri ya kijiji ambao pamoja na mambo mengine, ulijadili suala la kijiji hicho kukosa mvua kwa kipindi kirefu.kufuatia kutonyesha kwa mvua hiyo, wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakimtuhumu mkazi mwenzao, (jina limehifadhiwa) kwamba amekuwa akijigamba mitaani kuwa mvua kijijini hapo haitanyesha.baada ya wajumbe wa kijiji kuchangia kuhusu suala hilo, ndipo mbunge alipoondoka huku akiongozana na wajumbe hao pamoja na wananchi waliofurika kumwangalia, wakielekea katika nyumba ya mtuhumiwa huyo kwenye kitongoji cha kimunyu.“jamani mnakumbuka kwenye kampeni nilivyosema, napenda niwakumbushe, nilisema kazi ya ubunge ni ya miaka mitano lakini kazi yangu ya uganga siwezi kuiacha nitaifanya hadi nitakapokufa," alisema profesa majimarefu.mbunge huyo baada ya kueleza hivyo aliongozana na mwenyekiti wa kijiji hicho, mtendaji wa kijiji na mwenye nyumba hizo kuingia nao ndani ya nyumba ya mtuhumiwa.baada ya kuingia katika nyumba hiyo, profesa maji marefu alitoka akiwa na tunguri mbalimbali zilizodaiwa kumilikiwa na mtuhumiwa huyo.chanzo: Nipashe
mbona mr.ii anaendelea kuimba??????....y iwe nongwa kwa mh:ngonyani????
 
Ninakubaliana kabisa na wewe mkuu, lakini kuwanyamazia ndiko kunakowapa kidomodomo na kueneza propaganda zao. Kama nilivyosema, hapa pametolewa madi sita tu, pata muda au mwengine yeyote kutoka kawe, wamwagieni hapa data na matukio tuone kama akina MAFILILI na mwanakawe watakuwa na la kusema.

Mkuu MAMMAMIA nadhani Halima mwenyewe anaweza kuja kujibu haya madai hata kama ni ya kipuuzi ili kuwaweka sawa wale waliopotoshwa na taarifa hizi, ama msaidizi wake anaweza kuja kutolea ufafanuzi, vinginevyo wakaazi wa jimbo la kawe najua tunao wengi hapa JF wanaweza kushuhdia ni mambo gani mbunge wao aliahiodi na ameyatejkeleza kwa kiwango gani.

Natarajia kukutana na Halima kesho kutakuwa na mkutano Kigamboni na yeye ndiye anatarajiwa kuwa msemaji mkuu, niatamfikishia salamu hizi ili atoe taarifa ya kazi alizofanya so far ili kukomesha huu upotoshaji unaofanyika hapa.
 
Last edited by a moderator:
Watu wanakimbilia ubunge kutafuta riziki na kutengeneza maisha yao.wadanganyika wasioelewa wanakimbilia kutoa kura.

Haf muwe mnajifunza mbunge hana nguvu ya kuleta maendeleo ccm na serikali yake ndo wanajukumu la ulinzi na usalama wa wanamadale yani nakwambia halima wala cdm kwa sasa bado hawana mamlaka ya kuwapoka watz maeneo yao wala atutumii ilani ya cdm kwa hiyo uwezi mlaum mdee kwa sasa ipigie cdm 2o15 uone kama kutakuwa na malalamiko kama yenu hata majimbo yatakayo chukuliwa na magamba kina majimarefu
 
Asante sana Mwanaukweli kwa kutupeleka kwenye chanzo hcho hapo juu. Nimeingia na niliyokutana nayo mengi ndio yale yale, "Mnamlaumu Mdee hakufanya kitu mbona hamuulizi nani na nani wa chama hiki au kile". Watu tunashindwa kutoa hoja; hoja kama hii ni kukataa kujituma kiakili na kuwa mtumwa wa kujituma.

Nimeona hii makala ya Privatus Karugendo na nimedondoa hiyo hap chini kwa faida ya mleta mada na wengine wenye imani kama zake. Zaidi nawaomba wenye hoja dhaifu kidogo wasome kwenye nyekundu na blue:

Katika pitapita zangu nimekutana na bango linalomnadi mbunge wa sehemu fulani hivi: Baadhi ya misaada mbalimbali niliyotoa kwa wanajimbo langu, Binafsi:
- Nilisaidia upatikanaji wa majeneza pamoja na kusafirisha marehemu kutoka wilaya yangu waliopata ajali ya treni huko Dodoma na kushughulikia majeruhi kwa kuwawahisha hospitali ili kupata matibabu ya haraka.
-Nilifanikisha uletwaji wa mwili wa marehemu Mathias Kasoso kutoka Dar-es Salaam; Nilisaidia sana uwezekano wa usafiri wa ndege pamoja na usafiri wa gari wa kutoka uwanja wa ndege kwenda alikozikwa.
-Nilitoa baiskeli kwa mlemavu wa .... yenye thamani ya Tsh 60,000 na 100,000/- kumnunulia mlemavu mwingine baiskeli ya gurudumu tatu.
-Nilimsaidia mama mtu mzima kupata haki zake Dodoma zilizokuwa hatarini kupotea bure.
-Nilimsaidia Salehe na rafiki yake (shs 40,000) nauli ya kutoka Dar es Salaam, waliokuwa wamekwama.
-Niliwasafirisha vijana wawili kutoka jimboni mwangu waliokwenda Dar es Salaam baada ya kudanganywa waende huko ambako wangepatiwa ajira.
-Nilitoa ada ya mtoto wa mzee wa Mahakama ya Mwanzo binti yake aliyekuwa akisoma sekondari ya kata.
- Tarehe 24/6/09: Nilihudhuria mazishi ya mzee Maddu aliyezikwa huko Mtakuja na kuchangia sh 100,000 kama rambirambi.

Tunaweza kuzifahamu kazi za mbunge, kwa kuangalia kazi za Bunge, maana mbunge, ni mwakilishi wa jimbo (wananchi) katika Bunge: " Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi. Kuisimamia na kuishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba hii," Ibara ya 63(2), pia na Ibara ya 64(1) inaelezea kazi za Bunge, juu ya kutunga sheria.

Hivyo basi, Mbunge ni mwakilishi wa jimbo lake katika chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kina madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake.
Hivyo kutoa misaada, kusalimia misiba na kuwatembelea wagonjwa si kazi za mbunge. Huu ni wajibu wake yeye kama mwananchi katika jamii anamoishi. Hata asingekuwa mbunge, angetakiwa kufanya hivyo maana wananchi wote wanafanya hivyo, wawe madaktari, walimu, viongozi wa dini au viongozi wengine wa vyama na serikali. Inawezekana pia kwamba hata wananchi wanafikiri kwamba kazi za mbunge ni kujenga madaraja, ni kuleta maji, ni kuleta umeme, ni kusalimia misiba na kujenga shule.
 
Nadhani si halima mdee tu, majombo yote ya upinzani dar-es-salaam yako hoi. Huyu bwana wa ubungo ndo bomu la ffu. Alidiriki kumwita rais mdhaifu lakini ukweli ukiondoa miradi ya rais jk ya barabara, maji na upimaji viwanja mbunge mnyika hakuna anachoweza kujivunia kuwafanyia wananchi wa ubungo zaidi ya kugawa bodaboda kwa wale vijana waliompigia kampeni. Tunakaribisha mtu yeyote kutoka chama chochote mwenye ubavu tumpe tafu tuondoa hii minyororo ubungo. Yeye akafanye kazi makao makuu ya slaa huko kinondoni. Hatujawahi kuwa na mbunge dhaifu ubungo tangu enzi za wakina derek brycon. Hata kawe wana afadhali
 
Mbunge wa ubungo wakati wa kampeni tuliambiwa alipata A zote form six lakini tumeangalia kwenye mtandao wa baraza la mitihani tunaandaa protest. Alipata three dhaifu na hwkuchaguliwa kwend chuo kikuu labda kama alijipeleka kwenye masomo ya jioni. Huyu bwana hapana
 
Uwezo wa kufikiri na kupata ufumbuzi vinategemea na uwezo wa ubongo wa anaye fikiri!
Huwezi kuruka mkojo uka kanyaga mavi ukajisifia!
kuwa una macho mazima!
Huwezi kuotesha bagi ukavuna mchicha!
Pesa zilizo ibiwa kwenye migodi na mafisadi huzioni ma majaga ya kusafirisha wanyama hai kwa ufisadi pesa ambazo zingetosha kukuondowa ujinga leo unakuja kutufanya wavivu wa kufikiri.endelea kukanyaga mavi baba Aluta...... m4c daima
 
Mkuu MAMMAMIA nadhani Halima mwenyewe anaweza kuja kujibu haya madai hata kama ni ya kipuuzi ili kuwaweka sawa wale waliopotoshwa na taarifa hizi, ama msaidizi wake anaweza kuja kutolea ufafanuzi, vinginevyo wakaazi wa jimbo la kawe najua tunao wengi hapa JF wanaweza kushuhdia ni mambo gani mbunge wao aliahiodi na ameyatejkeleza kwa kiwango gani.

Natarajia kukutana na Halima kesho kutakuwa na mkutano Kigamboni na yeye ndiye anatarajiwa kuwa msemaji mkuu, niatamfikishia salamu hizi ili atoe taarifa ya kazi alizofanya so far ili kukomesha huu upotoshaji unaofanyika hapa.
Mwita Maranya Mkuu, kwanza nikiri kuwa hata mimi nilitaka kuburuzwa na nia mbaya ya mleta hoja. Naomba upitie, na hasa ninamuomba MAFILILI apitie post yangu nambari #65 hapo juu au kurejea post ya #80 ya Mwanaukweli hapa HAPA badala ya kuumizana vichwa na watu wasiotumia akili kutetea hoja zao.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani si halima mdee tu, majombo yote ya upinzani dar-es-salaam yako hoi. Huyu bwana wa ubungo ndo bomu la ffu. Alidiriki kumwita rais mdhaifu lakini ukweli ukiondoa miradi ya rais jk ya barabara, maji na upimaji viwanja mbunge mnyika hakuna anachoweza kujivunia kuwafanyia wananchi wa ubungo zaidi ya kugawa bodaboda kwa wale vijana waliompigia kampeni. Tunakaribisha mtu yeyote kutoka chama chochote mwenye ubavu tumpe tafu tuondoa hii minyororo ubungo. Yeye akafanye kazi makao makuu ya slaa huko kinondoni. Hatujawahi kuwa na mbunge dhaifu ubungo tangu enzi za wakina derek brycon. Hata kawe wana afadhali

Hii siyo kweli, Ubungo tunaijua na wabunge waliopita Ubungo tunawajua. Mnyika anafanya kazi nzuri kuliko mbunge yeyote DSM (muono wangu). Mnyika yupo karibu sana na wananchi wake kwa kuwasikiliza na kufuatilia masuala mbalimbali ya utekelezaji. Hata hiyo miradi ya JK inafanyika kwa push kubwa ya Mnyika. pole bro upenzi wa vyama anakupofusha usione ukweli.
 
We kweli akili magamba!!!....unamuona Halima Mdee zigo lisilosaidia wapiga kura badala yake anajisaidia mwenyewe...lakini wakati huo huo humuoni DHAIFU alivyo zigo kwa wapiga kura na kujisaidia mwenyewe, mafisadi wenzake, wageni wanaojifanya wawekezaji na familia yake!!!! Ama kweli Nyani haoni......

Mie nilidhani utajibu hoja unakuja na uzezeta ule ule, pamoja na kukubali kuwa Mdee ni zigo bado hujionyeshi katika hoja, badala yake unavamia wengine. Hizo fitna acha unayemwita dhaifu kwa sababu baba yako Mnyika kasema nawe kuwa kasuku butu. S itashangaa akisema vingine nawe utaukasuku maana huna ya kwako, nawasikitikia wazee wako.
 
Nadhani si halima mdee tu, majombo yote ya upinzani dar-es-salaam yako hoi. Huyu bwana wa ubungo ndo bomu la ffu. Alidiriki kumwita rais mdhaifu lakini ukweli ukiondoa miradi ya rais jk ya barabara, maji na upimaji viwanja mbunge mnyika hakuna anachoweza kujivunia kuwafanyia wananchi wa ubungo zaidi ya kugawa bodaboda kwa wale vijana waliompigia kampeni. Tunakaribisha mtu yeyote kutoka chama chochote mwenye ubavu tumpe tafu tuondoa hii minyororo ubungo. Yeye akafanye kazi makao makuu ya slaa huko kinondoni. Hatujawahi kuwa na mbunge dhaifu ubungo tangu enzi za wakina derek brycon. Hata kawe wana afadhali
Kuna mengi ambayo ameyafanya huyu mbunge:
1. Barabara toka Millenium Tower, kupitia Chekechea ya Hindu Mandal hadi Shoppers Plaza inawekwa lami.

2. Daraja la njia fupi toka Rose Garden kwenda School of Journalism Mikocheni limejengwa.

3. Amesaidia kuhamisha soko la Tegeta na Stendi ya Daladala Tegeta toka barabarani kwenda sehemu nzuri zaidi.

4. Amesimamia vema ujenzi wa barabara toka Tegeta Nyuki hadi Bahari Beach kiwango cha lami. Ujenzi umekamilika.

5. Amesimamia vema ujenzi wa New Bagamoyo road na upgrade ya Old Bagamoyo Road.

6. Amepambana sana na uvamizi na ubadilishaji holela wa matumizi ya ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya kijamii (KUNDUCHI, WAZO, MADALE n.k.) na kubatilishwa na kupewa watu wenye pesa. Katika hili kikwazo ni madiwani (wa CCM), ambao ndio wawakilishi wa maeneo husika kwenye vikao vya halmashauri pamoja na maafisa wa Halmashauri (inaongozwa na CCM) ambao ndio watekelezaji na ambao hawampi ushirikiano. Hapa ushirikiano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ulihitajika sana.

Mchango kwenye Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Tarehe 16/08/2011

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nukushukuru kwa dhati kwa kunipa fursa hii. Lakini vile vile siungi mkono hoja si kwa sababu sina imani na Waziri wala Naibu Waziri, hapana. Ni kwa sababu licha ya wao kuwa na nia njema ya kufanya kazi mbali ya kuwa na fedha finyu. Lakini nadhani hapati ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini kwa ujumla.


Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mzungumzaji mmoja nadhani ni mama Kikwembe if I am not mistaken wakati nimetoka akapiga mawe kidogo. Lakini nimhakikishie kwamba siwezi kuzungumza kitu ambacho sina ushahidi nacho. Aliniambia nimtajie majina ya Madiwani waliokwenda Marekani siku nne. Nitamtajia Kata, majina itakuwa kazi yake yeye kutafuta. Kuna Diwani wa Kata ya Magamba, kuna Diwani wa Kata ya Sitalike, kuna Diwani Viti Maalum Karema na kuna Diwani Viti Maalum Uruwira. Sasa majina akayatafute yeye.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini inasikitisha. Unapoona Mbunge mnajaribu kutetea eneo lake yeye, anakuja ana-crash down pasipo hoja za msingi na kwa sababu ya uvivu wa kusoma. Juzi kwenye SADC Forum iliyokwisha tu majuzi. Moja ya ajenda ilikuwa ni Land Crabbing Africa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wazungu huko walishamaliza kwao, wanakuja kurudisha ukoloni. Kibaya zaidi mtaalam wa Canada, mzungu huyo huyo akaenda na mikataba mizito hivi na mkataba uliotolewa mfano, kama West Case Scenario ni mkataba wa Agrisoil Tanzania. Nasikitika jana namsikia Mbunge mmoja kutoka Kigoma, anasema eti wenzake wa Kigoma wameshindwa kutumia ardhi, wakati kuna hekta 80,000 wameshindwa kutumia ardhi, kwa hiyo walete wawekezaji. Tena msomi mzuri, inasikitisha. Kwa hiyo, niseme hili la suala la Agrisoil mbali na
upungufu wake wote na upuuzi wake wote umekiuka Sheria ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria zetu ziko wazi kabisa na hii namwambia Mheshimiwa Waziri Mkuu asipoli-handle vizuri anaweza akaanguka nalo. Ataanguka nalo kabisa. Kwa sababu kuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba Ofisi yake ilihusika. Kwa hiyo tutumie busara tuokoe nchi. Sheria ya Ardhi iko wazi. Muwasaidie Mawaziri, mumsaidie Naibu Waziri. Sheria ya Ardhi iko wazi kabisa. Mgeni ama mwekezaji anapotaka kuja kumiliki ardhi ya nchi imeeleza wazi, kifungu cha 19, Kifungu cha 20(i) hadi 20(iv) mabadiliko ya 2004. Very clear na imesema wazi kabisa kama kuna joint venture inamhusu raia na Sheria ya Uraia haijatambua kampuni, haijatambua Halmashauri, haijatambua kitu kingine chochote raia mmoja mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mtuambie huko Rukwa ni raia gani anamiliki hekta laki mbili na kitu. Huko Lugufu Kigoma kuna raia gani anamiliki hekta 80,000 ambaye anaingia ubia sasa ili ule mchakato wa kufuata TAC usifuatwe. Naomba tuache ushabiki. Hii ni crisis?
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza taarifa yake siitaki. Lakini pili, mimi mwenyewe hivi kiwanja changu sina Hati Miliki. Hati Miliki siyo issue.


Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tatu, kuna kitabu cha makubaliano waliyoingia baina ya Halmashauri na Agrisoil na mkitaka nitaleta kwenye Meza yako. Wao wenyewe hapa wamekiri, kuna hivyo vitu vinavyoendelea Bungeni. Kwa hiyo, kama nyinyi ambao ndiyo mnatakiwa mtekeleze Sheria mnakuja hapa mnatetea wahalifu, tunakoelekea kama nchi kunatisha. Hatutafuti umaarufu wa kisiasa, umaarufu upo tayari, tunataka kujenga nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nirudi Jimboni maana nilisimama kwa ajili ya Jimbo. Lakini alinivurugua system Mama Kikwembe ikabidi nirudi kule ambacho sikutaka kurudi.

Suala la kwanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunilinda. Katika Jimbo langu na nadhani katika Majimbo ya Dar es Salaam ndiyo yanaongoza katika migogoro ya ardhi. Naomba Mheshimiwa Naibu Waziri na Mheshimiwa Waziri suala la Mabwepande. Miaka minne iliyopita mlikwenda pale, mkawaambia wananchi wasiendeleze maeneo yao. Mkawalipa wengine kama 160. Mheshimiwa Naibu Spika, namwonea huruma sana kwa sababu 2015 sijui kama atarudi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la Mabwepande. Naomba na muda wangu huu pia uzingatiwe. Miaka minne iliyopita Serikali ilikwenda kufanya tathmini na ninavyozungumza hivi pia na katika mfumo huo huo nazungumzia eneo la Kwembe kwenye Jimbo la Mheshimiwa Mnyika. Nilikwenda kufanya tathmini, wananchi wakaambiwa wasiendeleze maeneo yao na kwamba Serikali ina mipango ya kuja kulichukua lile eneo kwa ajili ya matumizi mapya. Jimbo la Ubungo lilikuwa ni kwa ajili ya kujenga Chuo cha Muhimbili kwa mantiki ya Campus nyingine. Lakini vile vile Mabwepande kulikuwa kuna chuo cha IFM na miradi mingine 20,000 ya viwanja.

Mheshimiwa Naibu Spika, imepita zaidi ya miaka minne. Wananchi hawajui mustakabali wao. Waliolipwa ni wananchi 160 tu kwa kipindi hicho zaidi ya wananchi 600, hawajui mustakabali wao ukoje. Lakini vile vile kwa upande wa Kwembe Serikali iliwaahidi wananchi kuwalipa pamoja na thamani ya ardhi na siyo mimea, kwa sababu pia Sheria zinasema hivyo na wananchi wa Kwembe hawana tatizo la kuhama. Tatizo lao la msingi ni ile haki yao waliyokubaliana kimsingi walipwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Mabwepande tunavyozungumza leo hii na nakumbuka wakati wa Kamati, nilivyokuja kwenye Kamati yao, nilimwambia kuna uvamizi wa hali ya juu unaendelea. Wananchi ambao waliiamini Serikali yao hawakulima, hawakujenga kwa sababu waliambiwa kwamba kuna mipango ya maendeleo, wakaa pembeni leo wamegeuka wakimbizi kwenye ardhi yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa namwomba Mheshimiwa Waziri kwa sababu nimeshapiga kelele katika Halmashauri, nimekwenda kwake kwa njia ya barua. Lakini hali kule ni mbovu. Naomba Serikali ichukue hatua. Mimi kama Mbunge wa Kawe silindi mvamizi hata mmoja. Wasije watu wakawa huko kwa maslahi yao, wanasema Mheshimiwa Halima Mdee anatuunga mkono. Sijatuma mvamizi yoyote akavamie eneo,nataka haki itendeke. Kwa hiyo, naomba suala la Mabwepande na suala la Kwembe naomba myafanyie kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini suala lingine Mheshimiwa Waziri kuna hili suala la Boko Dovya katika Shamba la Bwana Somji. Kuna taarifa hapa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kipindi kile alipokuwepo Mheshimiwa Chiligati, alikiri kwamba hili tatizo limekwisha. Serikali itachukua lile eneo kwa ajili ya kugawiwa kwa wananchi. Mpaka leo hakuna kinachoeleweka Somji anaendelea kuwasumbua wananchi ambao wako kwenye maeneo hayo. Kwa hiyo, naomba tafadhali tafadhali niweze kupata ufafanuzi kwa haya masuala.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini lingine ni suala la Chasimba. Hili suala siyo dogo kama watu ambavyo wanataka walifikirie. Ni suala ambalo linahusisha wananchi zaidi ya 10,000. Ni suala ambalo ushahidi wake uko wazi na nimeeleza kwa kina sana kwenye hotuba yangu. Lakini nitalizungumza hapa. Inawezekana Serikali mkaja na scenario kwamba hili suala ni la zamani, lilienda Mahakamani na limeamualiwa Mahakamani. Kwa hiyo, wananchi waondoke, naomba mtumie busara. Nina hukumu ya Mahakama hapa. Nina documents hapa nitamletea Mheshimiwa Waziri zinazoonesha jinsi kijiji kilivyosajiliwa zinazoonesha kwamba mmiliki wa kiwanda hamiliki viwanja vyote vitatu kwa mantiki ya moja, nne na saba. Lakini nimesoma hukumu hapa, inasema naomba ninukuu kidogo: "It is the respondent case from a total twelve witnesses that the village officials of Boko". Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba muda wangu kidogo, kengele ya kwanza? It is the respondent case from a total of twelve witnesses that the village officials of Boko and Tegeta were contacted with the view of securing more land by organizing meetings with the villages. At the end of the day the respondent managed to buy a number of villages by wealth composition. Hukumu sababu katika hii kesi respondent alikuwa ni TUGHE. Kwa sababu ilikuwa ni Mahakama ya juu kabisa. Wanakiri kwamba walioweza ku-manage ni a number of villages sio all of the villages. Ndiyo maana nashukuru tu kwa maana ya Mheshimiwa Ole-Medeye. Nashukuru sana. Wananchi waliokuwepo pale ni watu wazima, tofauti na maeneo mengine ya uvamizi, unaona ni vijana vijana tu wamekuja juzi. Naomba Serikali iliangalie hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, Lakini kesi ambayo ilikuwa inahusu watu takriban 1,000 ikaamuliwa on technical grounds kwamba linapokuja suala la ardhi, hatuangalii suala la representative's suit hairuhusiwi. Ikiwa ni Mahakama ya Rufaa Court of Appeal, haki za maelfu za wananchi zikaminywa simply because kwa uelewa wao labda mdogo waliamua wenzao 13 wakawakilishe Mahakamani na kati ya wenzao 13 waliokwenda kuwakilisha Mahakamani still walishindwa kuthibitisha wanne kati yao kwamba walilipwa fidia. Kwa hiyo, naomba Waziri asiwe mkali, naomba mtumie busara. Nawaombea wapiga kura wangu. Najua kuna haki imeminywa sehemu. Najua kuna interest za watu zinataka kuwaumiza watu maskini.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasikia wanataka kuhamishiwa Mabwepande. Sisi hili hatuliafiki. Tunajua eneo la kiwanda ni kubwa. Wakitaka kujipanua wataacha chenji. Tunaomba muwasaidie wananchi na niwaambie kwa hili, maana Madiwani wa Kata hizo mbili ni wa CCM. Moja, tumesema iwe jua, iwe mvua, sisi tutakufa na wananchi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hatufanyi uchochezi. Lakini nadhani natumia lugha laini sana. Ukienda Chasimba mwenyewe, sijui! Ole Medeye, tulikwendanae na anajua zaidi, naomba tuwasaidie wananchi wetu. Kuna siasa hapa, kuna vyama vyote viko kule, tuweke utu kwanza; eneo lipo la kutosha, la msingi ni kwenda kufanya vikao na wananchi, kujua eneo la kiwanda liko wapi, wananchi wanaweza wakakaa wapi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mwisho, hivi viwanja 20,000. Kunakuwa kuna tatizo kwamba, Wizara kwa nia njema kabisa mnaandaa miradi mbalimbali. Lakini tatizo ni kwamba, miradi hiyo haimilikishwi kwa wananchi ili waweze kujua viwanja vya wazi ni vipi? Viwanja vya shule ni vipi? Viwanja vya huduma za jamii ni vipi? Matokeo yake viwanja hivi vimegeuka kuwa sehemu ya Wenyeviti wa Mitaa kupata kula yao! Kwa hiyo, naomba katika miradi yoyote ambayo mliifanya, mwende mkai-review, muangalie maeneo ya wazi, maeneo ya umma ni yapi? Myafanye yawe wazi, ili wananchi kwenye maeneo hayo wawe walinzi wa ile rasilimali. Bila kufanya hivyo!

Mheshimiwa Naibu Spika, leo sheria haitambui kama Mwenyekiti wa Mtaa, anaweza akagawa eneo, lakini nitakwambia huko Dar-es-Salaam, wanagawa kwa kwenda mbele! Wakati nyie mnatoa maagizo huku, Wenyeviti wa Mitaa na baadhi ya Madiwani ambao sio waaminifu wanaendelea kuuza maeneo kwa kushirikiana na watu wa Manispaa ambao sio waaminifu. Kwa hiyo, naomba haya myaangalie kwa makini.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho kabisa na ambalo pia sio la muhimu, ni viwanja vya wazi Mkoa wa Dar-es-Salaam. Tunajua mna changamoto kubwa kwa sababu, wengi ambao wamewahi kupewa hayo maeneo ya wazi, hususan katika maeneo strategic, ni wakubwa! Wengine wamejenga ma-bungalow yao! Sasa naomba leo mtuhakikishie wakati mnahitimisha, ile taarifa iliyotolewa na Kamati iliyoundwa na Mheshimiwa Lukuvi, mtaitekeleza kwa ukamilifu wake na ndani ya kipindi gani? Nakuhakikishia Mheshimiwa Tibaijuka, ukiniahidi hilo nitakuona kweli wewe ule moto wako unaendelea. Ukiwa unasitasita nitajua yale ambayo yanasemwa, ulianza kwa speed wenzio wakakuminya! Tunakuamini mama, namwamini Mheshimiwa Naibu Waziri sana kama ambavyo namwamini yeye sana, hii sekta ndio uhai wa nchi. Hii sekta tukiipuuza na naiambia Serikali, tukiipuuza watoto wetu, wajukuu zetu watakuja kuchinjana na hatutaki tutengeneze Tanzania ya kuchinjana!

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana.

7. Amekusanya data za viwanda na mahoteli yote ya jimboni kwake ili kuhakikisha wanalipa kod inayoongeza pato kwa shughuli za maendeleo ya jimbo la Kawe.

8. Amekuwa anakutana na wananchi na kusikiliza kero zao na kupata maoni yao. Angalia video hii


9.Amepigania chuo cha IMTU Kilikuwa kinatoza ada kwa dola za marekani sasa kinatoza kwa fedha za TZ, pia ada ya imeshuka na kuwa fixed.

10. Eneo la Tegeta amesimamia ujenzi wa Shopping mall ya kisasa. Imekamilika.

11.
Amehamasisha na kuamsha ari ya vijana na kina mama katika kushiriki kwenye siasa na ameonyesha umahiri na kujiamini kwa hali ya juu jambo ambalo lemesaidia sana kubadili mtazamo wa wamama na wasichana walio wengi kwamba wakina dada nao wanaweza.

12. Ameshiriki
unanzishaji na uendelezaji wa vikundi vya kina mama Kawe.

13. Amekuwa na mchango mzuri sana katika kujadili miswada bungeni, na katika kuibua hoja za kitaifa.

Na mengine mengi sana mnisaidie kuongeza.

Ameyafanya yote haya licha ya juhudi za makusudi za Halmashauri (ambao ndio wanapokea fedha za maendeleo za jimbo) na madiwani (ambao ndio wawakilishi wa wananchi wa kata zao kwenye halmashauri) kumkwamisha.

Nahisi nyuzi nyingi zinaletwa hapa kwa sababu wanataka kuona juhudi za makusudi za kumkwamisha zimefanikiwaje.

By the way, kati ya wabunge wote wa Dar hakuna ambaye amezorota kama Abas Mtemvu. Mbona haanzishiwi threads nyingi kama Mdee? Na kuna thread ipo nimejaribu kwa makusudi kupost ili iwe juu tuone kama kweli watu wako objective lakini hakuna anayepost kitu kule.

Fikiria vema!
 
Last edited by a moderator:
Mwita Maranya Mkuu, kwanza nikiri kuwa hata mimi nilitaka kuburuzwa na nia mbaya ya mleta hoja. Naomba upitie, na hasa ninamuomba MAFILILI apitie post yangu nambari #65 hapo juu au kurejea post ya #80 ya Mwanaukweli hapa HAPA badala ya kuumizana vichwa na watu wasiotumia akili kutetea hoja zao.

Mkuu MAMMAMIA tayari majibu yameanza kupatikana kama unavyoona hii post ya Mwanaukweli. Sasa wafitini sijui watakuja na single gani tena.

Kuna mengi ambayo ameyafanya huyu mbunge:
1. Barabara toka Millenium Tower, kupitia Chekechea ya Hindu Mandal hadi Shoppers Plaza inawekwa lami.

2. Daraja la njia fupi toka Rose Garden kwenda School of Journalism Mikocheni limejengwa.

3. Amesaidia kuhamisha soko la Tegeta na Stendi ya Daladala Tegeta toka barabarani kwenda sehemu nzuri zaidi.

4. Amesimamia vema ujenzi wa barabara toka Tegeta Nyuki hadi Bahari Beach kiwango cha lami. Ujenzi umekamilika.

5. Amesimamia vema ujenzi wa New Bagamoyo road na upgrade ya Old Bagamoyo Road.

6. Amepambana sana na uvamizi na ubadilishaji holela wa matumizi ya ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya kijamii (KUNDUCHI, WAZO, MADALE n.k.) na kubatilishwa na kupewa watu wenye pesa. Katika hili kikwazo ni madiwani (wa CCM), ambao ndio wawakilishi wa maeneo husika kwenye vikao vya halmashauri pamoja na maafisa wa Halmashauri (inaongozwa na CCM) ambao ndio watekelezaji na ambao hawampi ushirikiano.



7. Amekusanya data za viwanda na mahoteli yote ya jimboni kwake ili kuhakikisha wanalipa kod inayoongeza pato kwa shughuli za maendeleo ya jimbo la Kawe.

8. Amekuwa anakutana na wananchi na kusikiliza kero zao na kupata maoni yao. Angalia video hii


9.Amepigania chuo cha IMTU Kilikuwa kinatoza ada kwa dola za marekani sasa kinatoza kwa fedha za TZ, pia ada ya imeshuka na kuwa fixed.

10. Eneo la Tegeta amesimamia ujenzi wa Shopping mall ya kisasa. Imekamilika.

11.
Amehamasisha na kuamsha ari ya vijana na kina mama katika kushiriki kwenye siasa na ameonyesha umahiri na kujiamini kwa hali ya juu jambo ambalo lemesaidia sana kubadili mtazamo wa wamama na wasichana walio wengi kwamba wakina dada nao wanaweza.

12. Ameshiriki
unanzishaji na uendelezaji wa vikundi vya kina mama Kawe.

13. Amekuwa na mchango mzuri sana katika kujadili miswada bungeni, na katika kuibua hoja za kitaifa.

Na mengine mengi sana mnisaidie kuongeza.

Ameyafanya yote haya licha ya juhudi za makusudi za Halmashauri (ambao ndio wanapokea fedha za maendeleo za jimbo) na madiwani (ambao ndio wawakilishi wa wananchi wa kata zao kwenye halmashauri) kumkwamisha.

Nahisi nyuzi nyingi zinaletwa hapa kwa sababu wanataka kuona juhudi za makusudi za kumkwamisha zimefanikiwaje.

By the way, kati ya wabunge wote wa Dar hakuna ambaye amezorota kama Abas Mtemvu. Mbona haanzishiwi threads nyingi kama Mdee? Na kuna threads ipo nimejaribu kwa makusudi kupost ili iwe juu tuone kama kweli watu wako objective lakini hakuna anayepost kitu kule.

Fikiria vema!
 
Last edited by a moderator:
Kutoka thread hii : https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ra-mbunge-wa-kawe-mheshimiwa-halima-mdee.html

Kuna post hii
Napenda kumpongeza mbunge wa jimbo la Kawe mheshimiwa Halima James Mdee kwa jinsi alivyokuwa bega kwa bega na wapiga kura wake wa maeneo ya Tegeta Namanga waliovunjiwa nyumba zao na mwarabu mmoja mwenye sheli ya mafuta.

Tuna amini kuwa utapigania haki zao mpaka zipatikane na huyu mwarabu awalipe fidia wananchi kwa uharibifu aliowafanyia.

Wabunge wengine hasa wa magamba igeni mfano huu wa kuwa karibu na wapiga kura wenu hasa waoapnkuwa na matatizo.

Ni kati ya mashahidi wa moja kwa moja akishuhudia jinsi wanvyoguswa na mbunge wao. Yuko karibu na wananchi.
 
Mkuu MAMMAMIA tayari majibu yameanza kupatikana kama unavyoona hii post ya Mwanaukweli. Sasa wafitini sijui watakuja na single gani tena.
Nimependa sana hii, lakini bado wananchi tunapaswa kuelewa kuwa si jukumu la mbunge kufanyakazi za maendeleo kwa kutumia mshahara wake, isipokuwa ametengewa kiasi fulani na serikali kwa ajili hiyo, wala kupita nyumba hadi kuuliza watu wameamkaje na kuhudhuria misisba kama mbunge bali kama jirani katika eneo lake.

Katika yote yaliyotajwa, hilo la kuchangia mawazo bungeni na kuishauri serikali ndio wajibu wake, sasa kama yupo wa kulaumu ni serikali na watendaji wake, hasa viongozi wa chama cha serikali, kinapokataa kufuata ushauri wa mbunge au kwa makusudi kufanya hujuma jimbo kwa mbunge huyo ama kwa ufisadi au kwa lengo la kumpaka matope mbunge husika.

Hongera Mdee!
 
Back
Top Bottom