Elections 2010 Kipindi cha pata-pata WAPO RADIO FM

leo nimefanikiwa kusikiliza kipindi cha PATA PATA katika radio ya WAPO FM 98.0. Kulikuwa na wasikilizaji wanatuma ujumbe wa maandishi kuhusu taarifa zilizokuwa zinatolewa. katika kipindi nilichokuwa nasikiliza jumla ya sms 12 zimesomwa na zililenga katika maeneo matatu:-

  1. zilizokuwa zinasema Dr. Slaa songa mbele, Tutawang'oa mafisadi = 9 = 75%
  2. Zilizosema Upinzani hauwezi kushinda kiti cha uraisi bila kuungana =1 = 8.3%
  3. Zilizoungamkono kitendo cha jeshi kutoa tamko hapo juzi = 2 = 16.7%
  4. Zilizosema JK Juu = 0 = 0%
Mbarikiwe, Amen

QUALITY,
Kuwa mwangalifu sana na thread kama hizi. Maana zinachochea hisia mbaya hasa mambo kama haya yakiletwa na chombo cha Kikristo katika wakati ambapo sisi m iko kwenye wakati mgumu.

Jambo moja linalonishangaza mpaka leo, neno likitoka upande wa kikristo, whether kanisani au kama hivi kwenye chombo cha habari cha kikristo kunakuwa na outcry kubwa sana kutoka kwa ndugu zangu waislamu. Hata viongozi wa nchi wanaingilia kati kuonya kuhusu udini.

Lakini nimesikia mimi mara nyingi ndugu zangu waislamu wakisema blunders kama hizi kwenye TV na radio, na hata kuna vijarida na magazeti yaliyo na uchochezi wa dhahiri wa kidini na hakuna anayejali including viongozi hawa hawa wa nchi kuwakemea. Lakini likitokea upande wa wakristo hilo basi litashikiwa bango na kila mheshimiwa wa nchi hii.

Na hapa ndipo nadhani, wamenoa step. Moto huu hautazimika sasa hivi. Maana dhambi hii imeachwa bila kutubiwa mwisho tutakula matunda yake wote. Hapa tusidanganyane. Lazima kiongozi wetu yeyote atakayekuwa kachaguliwa aliepuke. Hii ndio ilikuwa tradition yetu.

Tena namuonya sana ndugu yangu Omarilyas kwa kujidai hakusimama upande wowote wakati namuona wazi anachojidai kukichochea hapa. Usemi kuwa hakuna kiongozi sijui nini, sijui nini, ni uongo na unafiki tu. Siku zote nimeheshimu sana michango yake lakini polepole naanza kumuelewa. Viongozi wenye dhamila nzuri tunao na wapo na hata hawa wanaogombea wengi wana dhamila nzuri tu. Kwa sababu na wewe uko kwenye kundi la udini, udini unakupeleka mahali ambapo tunaziona true colors zako. Nimeona baadhi ya michango yako iko kwenye hali hiyo.

Lakini lazima tuwe wawazi kwamba viongozi wetu wa sisi m leo wame fuel hii mivutano ya kidini kwa kujaribu kuleta uchonganishi huo kwa maslahi yao na matokeo yake ndio haya. Mara ni hao hao waliodai CUF ni chama cha kiislamu na leo wanasema Chadema ni chama cha wakristo, wakijidai wao ndio neutral. Lakini kwani wao ni neutral kweli? mbona hata wao tunaona mapungufu makubwa upande wao katika jambo hili? Naam, hata hivyo, hii haina maana viongozi waliobaki walio katika race hii ya urais hawana dhamila nzuri, bali wapo wenye dhamila nzuri katika umoja wa taifa letu na wapo wenye dhamila mbaya.
 
Tusiwe na mtizamo wa udini. Suala la Dr. Slaa kuongoza katika kura za maoni siyo katika chombo kimoja. Ebu kumbuka vyombo hivi:-

1. Daily news: Ingawaje poll yao ilifungwa lakini ni baada ya kuona Dr. Slaa anaongoza
2. Radio Free Africa; walianzisha polls mpaka Jumamosi, Dr. Slaa alikuwa anaongoza
3. gazeti la Majira limeanzisha poll; Dr. Slaa anaongoza kwa 68% (by now 04/10/2010 at 22:12 hrs)MAJIRA: GAZETI HURU LA KILA SIKU
4. Jamii Forum Pia Dr Slaa anaongoza kwa 69% (by now 04/10/2010 at 22:12 hrs)

Je hapo una maoni gani???
 
Hivi kuna chama mbadala ama mgombea wa chama chochote anayeamini katika kuondoa matabaka???

Mwalimu alijaribu hivi sasa mnamkejeli.....kama alishindwa yeye tutegemee nini kutoka kwa wenye kuamini katika ubepari....Tuache kujidanganya, hakuna mwenye nia wala uwezo wa kuondoa matabaka nchini. Na wengi wanaolia kuhusu matabaka tayari wamekaa mkao wa kula for THEIR TURN TO EAT na ndio maana wako tayari kutishia, ku -condone, kujustify ubagazuzi na hata umwagaji damu kama matakwa yao hayatafanikiwa ama kukubaliwa.....

.
Hatujisumbui sana pale Jk na serikali yake inapokiri kwamba haiwezi kuondoa matabaka kwa maana kwamba hata Nyerere alishindwa. Sasa hili linatupa uhalali wa kumjaribu Slaa kwa kazi iliyomshinda Jk. Hakuna haja ya ccm na serikali yake kulilia kazi iliyowashinda, hebu wakae pembeni waone kazi inavyofanywa na mwanaume asie na uswahibi na mafisadi.
 
YANI TATHMINI YAKO UMEIFANYA KWA WATU 7 TU?, SHAME ON U. MI NILIDHANI UNGENIAMBIA ASILIMIA KADHAA YA WATANZANIA NDUGU YANGU, HEBU AMSHA AKILI.:hat:
 
sio leo tu.....kila wapo wakitoa habari za siasa hasa uchaguzi na ukisikiliza MAONI YA WENGI AKIWEMO MIMI YANAONESHA JINSI CCM ILIVYOCHOKA MBAYA.........SIELEWI HUO USHINDI WA LAZIMA WATAPAJE?
 
Back
Top Bottom