Kipindi cha mpito kuelekea kwenye utawala mwingine

Mndokanyi

JF-Expert Member
Sep 6, 2012
629
119
Leo katika vyombo vya habari nimemsikia Mh. Mbowe akiitaka serikali itunge sheria au kuingiza kifungu kwenye katiba kinachohusu makabidhiano ya utawala kutoka chama kimoja na kingine.Amesema kwa nchi kama Marekani inachukua siku hadi 72 kwa kiongozi mwingine kukabidhiwa madaraka,ila hapa kwetu ni masaa 48.

Wazo langu:
1. Je CCM iko tayari au inakubali kwamba siku moja wataachi nchi watawale wengine?
2.Je itaweza kupeleka sheria bungeni au kuingiza hiki kifungu kwenye katiba?

Ningependa Wana CCM watoe maoni yao
 
CCM hawataki huo utaratibu na watapinga sana maana hawako tayari kuachia madaraka. Wanataka wakiiba kura chap chap mtu anaapishwa, hapo tayari kesi imeisha
 
marekani ni marekani na bongo ni bongo.....hayo masaa 48 yanatosha....wewe yaani ccm ipigwe chini alafu ipewe siku 72 kukabidhi madaraka eeh hizo siku 72 si wataiba mpaka toilet paper huko makazini..yani mbongo apewe siku 72 huku akijua anaondoka..nyie nyie msifanye mchezo
 
Hahahaaa...
 
Hilo nalo neno
 
Hii ni kwa maslahi ya taifa hailengi ccm au chadema au cuf ,hivi vinabaki kuwa vyama maslahi ya taifa kwanza chama baadae .pia mkumbuke hali hii huleta taharuki sana pindi chama fulani kinapokosa kura za kutosha ,na endapo kuna mipango madhubuti hakuna kinacho haribika ,watendaji serikali watafanya kazi zao kuweka kila kitu sawa .hakuna kuhujumiana , mi naunga hoja mkono .
 
Back
Top Bottom