kipindi cha mapigano kule Msumbiji

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Nakumbuka miaka mingi nyuma, kipindi kile cha mapigano kule Msumbiji,
wamakonde wengi waliingia Mtwara kwa njia za panya. Na serikali
ikaamua kuwatafuta na kuwaweka wamakonde wote wa Msumbiji kwenye camp
maalum.
Nakumbuka watu wengi walikamatwa wakiwemo Watz na hao wa Msumbiji,
tatizo likawa kila mtu anadai kuwa yeye ni Mtz.
Ikabidi Mkuu wa Kituo cha pale Newala kuwatumia Askari wa JKT watumie
mbinu moja ya kuwauliza maswali na kusikiliza rafudhi zao. Na mnajuwa
tena enzi zile JKT, walivyokuwa na nongwa... (Kumbuka kipindi kile cha
wahujumu uchumi... Nakumbuka kuna jamaa mmoja alikamatwa na sabuni
moja ya Lifeybouy... yaani alikoma...!! Aliambiwa apige push up kwa
maelekezo ya Afande wa JKT, kwa kuambia hivi... Nikisema UP unakwenda
UP nikisema JUU unakwenda JUU, sawaaa... haya Juu... Up... Juu...
Up... Juu... Up..., jamaa kaganda ajui afanye nini. Akaambiwa
unajifanya Fwara sisi ndo mafwara yenyewe kabisa...)
Tuendelee na kisa chetu cha Wamakonde... sasa mambo yalikuwa Hivi:
Baada ya watu wengi kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi halali wa
serikari ya jamuhuri ya Bongo, mahojihano na watuhumiwa yalianza.
Kulikuwa na makundi mawili, kundi la kwanza (A) ni lile ambalo ni raia
halali wa Bongo na kundi la pili (B) ni la kutoka Mchumbiji, I mean
Msumbiji...
Afande wa JKT: Jina Rako rinani kijana
Mtuhumiwa1: Naitwa Chikirimu...!
Afande wa JKT: Kaa kure kundi 'B'
Afande wa JKT: Na wewe ndo rinani...!?
Mtuhumiwa2: Chigara
Afande wa JKT: Kaa kureeee... kundi 'B'
Afande wa JKT: Na wewe...?!
Mtuhumiwa3: chelikali Kuu (Huku akitoa mimacho kumtisha Askari wa JKT
kwa jina lake)
Afande wa JKT: kaa kundi 'B', tafadhari
Afande wa JKT: Na wewe jina rako ri nani
Mtuhumiwa4: chipoti
Afande wa JKT : kure kundi 'B'
Afande wa JKT : na wewe...
Mtuhumiwa5: miye chichemi kitu
Afande wa JKT: Kundi 'B'
Mtuhumiwa5: lakini chijachema kitu...( huku akikokotwa na askri
kuelekea kundi 'B')
Afande wa JKT: na wewe
Mtuhumiwa6: Mi jina langu refu chana...
Afande wa JKT: sawa lakini tuambie tupate kuandika
Mtuhumiwa6: Naitwa reli ya kati (akifikiri kuwa kwa kuwa reli ni ndefu
watashindwa kumsajiri).
Afande wa JKT: iri jamaa rijamaa ra kundi 'B' tuu...
Afande wa JKT: na wewe...!
Mtuhumiwa7: Jina langu la ntu nkubwa
Afande wa JKT: ndio tuambie unaitwa nani...?
Mtuhumiwa7: (kwa kunong'ona) Naitwa Chintu binti Karume Nyerere
Kuangalia muda wangu ukawa unaniishia ikabidi niawaache niendelee na
shughuli zangu, nikawaacha wakina Chantumavi, uchingizi nuchu,
churuali ya nchungu na wengine wakisubiri zamu zao...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom