Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,408
- 31,392
Full blood picture ni kipimo kinachotumika kuelezea hali ya damu kwa ujumla wake hasa pale ugonjwa unapokuwa hauna chanzo kamili au unapokuwa na vyanzo vingi vinavyoingiliana. Humsaidia daktari kupunguza wigo wa kutafuta chanzo.
Damu inatengenezwa na Red blood cells, white blood cells na platelets ambazo kila kimoja kina kazi yake. Mfano red blood cells ni kwa ajili ya kubeba Oxyegen( Haem= Iron, globulin= protein).
White cells zimegawanyika katika makundi zaidi kama neutralphil, aesinophils, lymphocytes n.k. Kila kimoja katika kundi hili kinajihusisha na ulinzi wa mwili na kinapambana na wadudu maalum kwa mfano bacteria, virus, fungus, protozoa n.k.
Daktari anapoona wingi au upungufu wa kimoja katika hivyo hujikita zaidi kutafuta nini chanzo. Kwa mfano kuna magonjwa yanayoathiri lymphocytes tu na hapa daktari atajikita kufahamu kwanini mgonjwa ana lymphocytes nyingi kuliko au chache kuliko na tayari anakuwa anajua ni magonjwa gani yanayoweza kuleta hali hiyo na atakuwa amepunguza wigo mkubwa wa kutafuta kila kitu.
FBP haionyeshi wadudu bali ina suggest ni tatizo gani na limesababishwa na nini. Kwa mfano kuna cells zinaweza kuonekana katika hali isiyo ya kawaida lakini hazitokani na bacteria, virus au fungu bali inaweza kuwa ni auto immunity au vitu kama cancer. Isijeeleweka kuwa FBP inaonyesha ugonjwa halisi, hapana inatoa mwelekeo wa tatizo lilipo.
Baada ya kupata uelekeko Daktari anaweza kukuagiza kwenye kipimo halisi kinachohusiana na ugonjwa huo. Mfano akiona cells flani kama lymphocytes si za kawaida anaweza kukueleza ukapime makohozi. Kipimo kikirudi na kitu kama TB atajua una backeria wa TB. Atarudi kwenye FBP na kuangalia cells za immunity zipo sawa? akiona zina mushkeli atakuagiza ukapime kile kipimo cha hofu (HIV)
Huko wataangalia cells za immunity yako ndipo wanaweza kutoa majibu kuwa mambo nia aje.
Kwakuwa FBP inaangalia damu kwa ujumla basi hata red blood cells zinaweza kutoa mwelekeo. Mfano kama ni chache au nyingi atakuagiza ukapime Haemoglobin level ili kujua una damu kiasi gani au una tatizo gani linalosababisha ongezeko la damu au kwanini red blood cells haziko sawa.
Mfano kama ni haemogloni ni chache unaweza kuwa na upungufu wa damu(anemia) na hapo atajiuliza kwanini una anemia. Inaweza kuwa ni malaria na atakuagiza ukapime malaria, au zaweza kuwa zina umbo lislo la kawaida (sickle shape) hapo utakuwa na sickle cell.
Kwa ufupi ni kipimo kinachotoa mwonekano wa damu kwa ujumla wake ili kujua wapi pa kuelekeza nguvu.Mfano rahisi wa mtaani (msicheke) unapooona nyumba inafuka moshi kitu cha kwanza ni kufungua mlango ili ujue nini kinaungua (hapa unatafuta Full house picture). Ukisikia harufu ya mahindi utajua tatizo linaweza kuwa jikoni, ukisikia perfume utajua chumbani, ukisikia mbaya utajua chooni na ukisikia plastic utajua ni chumbani hasa kwa watoto kwenye ma-toy. Hapo itakupunguzi muda wa kuanza kufunua kila kila kitu bali utakwenda moja kwa moja kule unakojua harufu inapoweza kuwa inatokea.
senti sumuni.