Kipimajoto ITV: Tundu Lissu ndani ya nyumba

I am keenly listening word to word from Lissu's mouth with a solely intention of picking any partial or full ambigous word to raise allegations propaganda but to the moment I've got none! Bravo Lissu-Proud of our country.
 
Anasema masuala ya udini kwenye vurugu za Zanzibar ni hoja ya kujishikiza tu. Suala zima ni utata wa muungano..

Hii point inamfaa sana [MENTION]Mzee Mwanakijiji [/MENTION] aliyetaka watu waamini kuwa vurugu zile ni za kidini.
Big up LISSU
 
I am keenly listening word to word from Lissu's mouth with a solely intention of picking any partial or full ambigous word to raise allegations propaganda but to the moment I've got none! Bravo Lissu-Proud of our country.
 
Kuna hili dubwashika lenye koti la kijani linasema hoja ya kupinga muungano ni hoja ya Cuf,Lissu anampinga anasema Mzee jumbe na wanasheria wake waliwekwa kizuizin kwa kutaka kuujadili muungano,so suluhu ni kuruhusu mjadala wa Muungano!

naamini huyu jamaa katumwa na TISS
 
Simu toka tabata:

Muungano ni haki ya wazanzibar kuujadili kabla ya kwenda kwenye katiba, ombi langu mweshimiwa rais atoe fursa ya kuujadili
 
Mwanasheria: Ninini kilipelekea muungano? je sababu zile za kuwepo muungano bado zipo? je matatizo yaliyopo hayatibiki? mfano: kuna mfuko wa muungano wa pesa, na katika matumizi ya mambo ya tanganyika pesa zinazotumika ni za mfuko wa muungano! je serikali tatu zikiwepo tatizo halitatibika?
 
Simu toka kibaha steven: Kuna sababu gani muungano usijadiliwe? muungano ni wa watu wote sio wa mtu mmoja, watu waachwe waujadili na wawe huru
 
Simu IDDI wa arusha: kwa nini vyombo vya habari haviwapi fursa UAMSHO kujieleza baada ya kuwaelezea uamsho kama watu wabaya? maoni yangu binafsi vyombo vya habari viwaite uamsho na viwahoji ili tupate maoni yao........mimi nina wasiwasi kuwa huenda serikali ikafanya haya mambo yenyewe kwa maslah yao
 
Yaani watu wanaongelea jinsi ya ku-maintain amani huyu jamaa anasema kuna vurugu kubwa zaidi itatokea! Sijui yuko level ipi maskini!
 
Mjumbe:Fujo zilizotokea ni kidogo tu na ninategemea fujo zaidi kutokea, wazanzibar tokea siku ulipotangazwa muungano waliupinga
 
Huyu mwenye barghashia sio member wa uamsho? Manake nae alikamatwa hapo nyuma..
Simu IDDI wa arusha: kwa nini vyombo vya habari haviwapi fursa UAMSHO kujieleza baada ya kuwaelezea uamsho kama watu wabaya? maoni yangu binafsi vyombo vya habari viwaite uamsho na viwahoji ili tupate maoni yao........mimi nina wasiwasi kuwa huenda serikali ikafanya haya mambo yenyewe kwa maslah yao
 
Cha ajabu kipimajoto kimebadilika watu wanajadili MUUNGANO TU sio uamsho tena.
hahahahahahahahahaha
 
Mjumbe: Ukweli ni kwamba hakuna kitu muungano, kuna fikra ya muungano. kwa sababu kama suala la muungano ni sheria, na ukiangalia mfumo wa kisheria hakuna muungano. kwa hiyo kisheria hakuna muungano.
 
Kwa imani yangu, siku ya mwisho (kiama), kuna mambo matano ambayo mtu hatahukumiwa bila Mwenyezi mungu kumuuliza juu ya jinsi gani aliyatumia hapa duniani.Mambo hayo ni umri, mwili,madaraka, mali na ELIMU.
Napata shida kidogo na jinsi wasomi wetu (baadhi yao) wanavyotumia elimu yao kwa manufaa ya uma.Tuache ubinafsi na kuangalia masilahi yetu tu ktk mambo ya msingi kwa jamii zetu, TUTAULIZWA NA MWENYEZI MUNGU.
Tundu Lisu, ni mwanasheria kwa taaluma, ni mbunge kikazi na ana uanaharakati in background ILA inaonyesha kwenye mjadala huu hajaelewa mswada wa katiba alioupitisha bungeni baada ya kualikwa magogoni AU anakataa kuuelewa kwa maslahi anayojua yeye.
Kujadili Muungano hakujakataliwa bali mjadala uwe ni kwa jinsi gani tuuboreshe na sio kuuvunja.Mara nyingi (past history) hua anamnukuu Mwl Nyerere lkn naona ktk mambo yaliyona maslahi fulanifulani. Nyerere was a Pan-Africanist, i dont think if at all Lisu buys into the idea of Pan-Africanism.
CHONDE-CHONDE TUTUMIE ELIMU NA NAFASI ZETU KUUTUMIKIA UMA NA SIO WATU WACHACHE KWA MASLAHI FULANI FULANI.
 
Muungano ni mfumo wa sheria,na si mfumo wa siasa,hakuna muungano bali kuna nadharia ya muungano
 
Back
Top Bottom