Kipima Joto ITV - Matusi ya bungeni

Aquilina Aloys:

1. Wabunge wanatafuta sifa. Eti akitukana anakuwa shujaa

2. Chuki binafsi, anaamua kutoa nyongo kwa chuki binafsi

3. Wabunge hawarudi kwao, hivyo wamejikatia tamaa kwa kuwa hawana matumaini ya kurudi bungeni.

Wabunge onyesheni busara, matusi si uungwana.

Mifano mibaya kwa watoto
 
Karim Furaha Gichela.

Inasikitisha. Mwalimu alisema ili uheshimike tumikia watu. Siasa ni njia ya kutumikia watu, na sasa siasa imeshuka heshima.

Tukiwa shuleni tulifundishwa kuhusu Bunge, sasa hivi wabunge wanalishusha hadhi bunge.
 
Timothy Peter - Chuo cha Ardhi

Wabunge hawafanyi walichotumwa na wapiga kura wao. Wabunge wengine wana michango ya hovyo. Hawaji kwa wapiga kura kupewa cha kuongea.

Wabunge watambue

Kizazi cha wanasiasa wa kesho wanajifunza kutoka kwenu. Zingatieni maslahi ya wananchi kwanza, maslahi ya vyama pembeni.
 
nachukia wabongo tunaogopa kata palipo shingo.maneno mengi bure.

Kwani waongee km wanaomba ukuu wa wilaya.si waseme tuu ni magamba ndio aibu.

Kauli za jumlajumla, ni upuuzi,
 
Peter Mwandu

Bunge limekumbwa na rushwa. Kuna wabunge wanatumikiaa watu wengine na si wapiga kura wao.

Lugha za matusi na kuudhi, tunatumia vigezo gani? Kuna waliotoa hoja za msingi wakapewa adhabu, lakini vigezo gani.

Wabunge ambao ni wakuu wa mikoa wajizuie zaidi.
 
Ninaendelea kukiangalia. Taabu ni kwamba watayarishaji hawana habari kabisa kwamba tatizo bungeni ni suala la Kanuni. Mijadala kama hii hawa ITV walitakiwa ku-dowload Kanuni za Bunge ndiyo ziwe nguzo ya mjadala. Hapa hakuna hata mmoja mwenye kanuni wala anayetaja kanuni. Hawa nao ni tatizo.
 
Erick Senga.

Bunge letu lina watu wasiokomaa.

Kuna watu wanataka kujenga chama pale kilicho kibovu.

Hata asiyejua miongozo anajua kuwa kuna shida. Kiti cha spika kinatekeleza maslahi ya chama. Kiti hicho kiwe kwa mtu asiye mwanachama wa chama chochote. Katiba mpya ifanye hilo badiliko.
 
Denis Bungole

Watu wanahama kutoka masuala ya msingi. Kuna hoja za ubadhirifu wa fedha, badala ya kujadili hilo tunaona wanaanza kupeana matusi na kukashifiana.
 
Mwanaharakati mmoja kachangia vizuri sana. Bahati baya sikuweza kulinukuu jina lake lakini ni mwana-Mama.
Anasema ndani ya Bunge hakuna mazingira ya kutendeka haki maana Mawaziri ni Wabunge na wamekaa mle mle Bungeni, Spika ni Mbunge na Naibu wake na wa chama hicho hicho kimoja, unategemea haki itendeke kweli? Kwahiyo ametumia fursa hiyo kukumbusha Watanzania kutumia fursa hii ya kujadili Katiba ili haya mambo yapate kurekebishwa na Katiba mpya.
Mchango wake huyu Mama ulikuwa makini sana.
 
Henry - Mwanaharakati

Matusi ya bungeni yanatokana na kuingiliana kwa mihimili ya dola.

Inatokana na muingiliano wa maslahi. Wabunge wako kwenye bodi mbalimbali wanakwepesha hoja za msingi za bodi wanazosimamia.

Tunahamishwa mawazo toka mawazo ya msingi kwa vijembe na matusi, wanapotezea mambo ya msingi.

Kutozingatia kanuni za bunge kwa kiti cha spika. Uendeshaji ni mbaya. Aliyesema f.ck you hakupewa adhabu aliyeomba mwongozo amepewa adhabu
 
Ernest Jerry

Inashangaza Mheshimiwa kutoa kejeli na matusi kwa bifu za binafsi.

Kwa bunge letu tunakuwa kituko na kituko kinachodharaulisha wananchi. wabunge wetu wamekuwa wasanii.

Ikifika 2015 tuone wale wanaokejeli na vijembe tuwatoe ndio adhabu.
 
Issa William Nyanda

Inasikitisha na inahudhunisha mwenendo wa bunge.

Wabunge wamwogope Mungu wataepuka tabia zinazokera. Wamesahau majukumu yao, kutunga sheria, Kusimamia sheria na kukosoa serikali pale imekosea.

Wabunge waruhusiwe kukosoa pale penye ukweli, lakini kupongeza pale mazuri yaliyopo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom