Kipima joto itv. Kuyumba kwa huduma za afya katika hospitali za serikali nini kifanyike????

commited

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,626
870
Wadau karibuni tupate data za juu ya hili tatizo la afya na nini kifanyike..... Kipima joto cha itv kipo hewani sa 3 usiku huuu... karibuni


kuna washiriki wanne hapa... wanajaribu kiutoa data data za gharama za kumuuandaa dokta mmoja ni takribani milioni 30 kwa dokta mmoja, na ratio ya dokta mmoja kwa wagonjwa, ni dokta 1: kwa wagonjwa 30,000, wakati WHO standard ni dokta 1:10,000(wagonjwa).. kwa hiyo unaweza kupiga hiyo milioni 30 mara gharama ya hao madokta 360 waliofukuzwa kama intern ni shilingi ngapi zimepotea...
kuna mbunge mmoja wa ccm anasema anaipongeza serikali na anadai gali si mbaya... yupo ki serikali zaidi hivi naona
 
Kune zee moja hapo lilikuwa litawala, limesema limetembelea nchi nyingi kwa maana kwamba halitibiwi nchini!
 
naona huyu mbunge dk (steveni kebwe) wa serengeti yupo hapa.. kuaminisha watu kuwa huduma hazijayumba sanaa, na pia anadai kutokuwepo kwa vifaa si ishu kubwa,.... so anasema tatizo ni menejimenti zaidi... na anasema madokta wao wamejifil wenyewe kuwa hivyo so wanapaswa kuwatumikia wananchi, anadai marekani pia bado kuna mahitaji ya madokta, lakini anadai tz hapa ndiko ambako ma dk wanademand kubwa sana kuliko nchi nyingine

naona ukiwa na profession yako then ukiingia katika siasa bila shaka hata uwezo wa kuwafikiria wananchi wa kawaida unapungua.. ndio kama huyu dokta mbunge wa serengeti
 
Kune zee moja hapo lilikuwa litawala, limesema limetembelea nchi nyingi kwa maana kwamba halitibiwi nchini!

ni kweli mzee hili lizee naona limekaa kisiasa zaidi wakati nalo ni li dk kwa miaka 25, naona hizo 10 millioni kwa mwezi zimesha mpumbaza daah kweli peswa mwanaharamju... hakumbuki tena shida za ma dk wenzie ..daah
 
hao waongezewa bajeti na kurudisha nidham ya fedha.. Na moyo wa dhat kwa madokta na manesi kufanya kaz kuwa udokta ni witi.. 'This is tanzania where health system are poor but we jus hav?ng fun'
 
Mdau rusha namba ya simu niwapigie simu ili niwape live!!

hahaaaa haya mkuu ngoja watoke kwenye kuwasikiliza wa tz wa mtaani wakirudi bila shaka masako atataja no za cm.. ntakutumia... bongo kila kitu ni siasa tu huyo dokta mbuge wa serengeti wa ccm naona yupo full kisiasa hachambui mambo kwa kina leo miaka 51 ya uhuru hata ct scan hatuna ya 80 millioni wakati watu kama shimbo wamelimbikiza trilioni 4 south bank daah mbongo.... sijui tutatokaje hapa....
 
hao waongezewa bajeti na kurudisha nidham ya fedha.. Na moyo wa dhat kwa madokta na manesi kufanya kaz kuwa udokta ni witi.. 'This is tanzania where health system are poor but we jus hav?ng fun'

Sir. JAPHETI sante kwa ushauri lakini kwa hii serikali ya 1o percent hi.lo sahau wao wanajiangalia wenyewe tu.. unajua mshahara wa waziri.. loh hata mbunge tu sasa anakwenda kwenye milioni 10, lakini dokata waliyemuandaa kwa zaidi ya milioni 30... hawako tayari kumsikiliza kila kitu wao wananjiangalia wenyewe...
 
Jamaa anatoa takwimu sasa kuprove kwamba sekta ya afya imedolola

1.Anasema afya na elimu ndio vinapswa kuwa vipaumbele vikubwa sana.. kwani maendeleo yanakuja watu wakiwa na afya njema, jamaa anasema katika bajeti zoote tangu 2008/2009 mpaka leo inakwenda ikipungua toka 18% mpaka 8% mwaka 2011/2012 kuonyesha kwamba afya si kipaumbele sana... coz bajeti yake inashuka kwa kasi kila mwaka

anaendelea...
 
magamba si mchezo, sanaa kila mahali.

hawa jamaa ndio adui no moja kwa watz maana ct scani jamaa anasema ni milioni 350 lakini je ni ct scan ngapi ambazo tungeweza kuzipata toka katika zile pesa za epa tu kama kweli kama tungekuwa tuko serious tangu 1995 mpaka leo tuna ct scan 1 tu miaka 51
 
ata ccbrt kwa dk slaa hakuna

ccbrt ni ya private mkuu.. lakini kweli unaamini serikali inakosa milioni 350 kila mwaka kununua ct scan moja moja kila mwezi kweli mkuu??


jamaa anauliza kwamba hii migomo imeanza tangu mwaka 91 je wakati huo pia vyama vya upinzani pia vilikuwepo?? kwani baadhi ya watu wanadai kuwa hii migomo imekuwa inginereed na vyama pinzani
 
Hivi kweli hawa watu huwa wana zkili timamu? Unajua huyu mbunge wa Serengeti simuelewi! Hivi anajua kwamba yuko hewani? Siyo anahara tu maneno asiyoyajua.
 
Hivi kweli hawa watu huwa wana zkili timamu? Unajua huyu mbunge wa Serengeti simuelewi! Hivi anajua kwamba yuko hewani? Siyo anahara tu maneno asiyoyajua.

mkuu huyu jamaa ni nomaa sasa anasema bajeti kila mwaka ya wizara ya afya inaongezeka... naona yeye yupo hapa kuitetea serikali.... siasa mbaya kama bajeti inaongezeka kwanini vitu kama vifaa tiba havipatinkani.. hata madawa ni shida sasa hiyo bajeti inakwenda wapi??
 
Back
Top Bottom