Kipima Joto ITV: Kambi rasmi ya Upinzani kususia bungeni ni suluhisho?

M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
151
Swali lipo hivi

"Kambi rasmi ya upinzani kususia mjadala wa katiba, je ni suluhisho?"
 
hayo majibu hayataki maelezo ya ni ndio au hapana basi bila ya kuuliza hivyo huwezi jibu ndio au hapana..
 
Ilitakiwa imalizie "Je, ni hatua sahihi", kama huna background ya jinsi surveys zinavyofanyika huwezi kujua haya mambo.
hayo majibu hayataki maelezo ya ni ndio au hapana basi bila ya kuuliza hivyo huwezi jibu ndio au hapana..
 
kweli swali hili ni la kishabiki, lakini jibu la ndio, hapana au sijui ni sawa na ndo majibu yao awa wazee wa (ITV) kipima joto
 
Naomba baadae mtupe jibu limekuwaje,maana wengi tupo mbali na tv.
 
Ndio, ni suluhisho mbadala kabisa.. Natabiri MATOKEO :NDIYO 70% , HAPANA23%, SIJUI 7%.
 
Swali lipo hivi

"Kambi rasmi ya upinzani kususia mjadala wa katiba, je ni suluhisho?"

Kumbukumbu yangu inaonyesha leo (alhamis) ITV wanakuwa na kipindi cha malumbano ya hoja na kesho ijumaa ndipo wanakuwa na kipindi cha kipima joto!
 
Wangeuliza WABUNGE WA CCM KUENDESHA MIPASHO BUNGENI JE NI SULUHISHO LA KATIBA MPYA?

Hili ndilo lilikua swali la kuuliza,
Hilo la upinzanu sijui nini ni uzushi tu.
Inawezekana hao wapinzani wamesusa labda Mara 4 tu Tena kwa sababu maalumu,
hiyo mipasho ya kila siku kutoka CCM hao ITV hawaioni???
 
Matokeo yametangazwa na yako kama kama ifuatavyo:
Ndio 75% Hapana24% Sijui1%
 
Swali lipo hivi

"Kambi rasmi ya upinzani kususia mjadala wa katiba, je ni suluhisho?"
75% wamesema NDIYO, 24% wamesema HAPANA, na 1% sijui....
chuja mwenyewe uone nani mshindi ingawa swali lilikuwa limekaa kizushi fulani ivi.
 
kipimajoto cha ITV ovyo sana....

wanatoa asilimia za ndiyo, hapana na sijui lakini hawaonyeshi idadi halisi ya watu waliopiga hizo kura???

Mfano:

Inawezakana asilimia 80% ya ndiyo ni SMS za watu nane (8) tu & asilimia 20% ya hapana ni watu wawili (2) .......

Je watu 10 wanawezi wakilisha watu milioni 40........
 
Nakubaliana na wewe mkuu! Kwa hali inavyoendelea nchini, inakuwa vigumu sana kuchakachua kila kitu.
75% wamesema NDIYO, 24% wamesema HAPANA, na 1% sijui....
chuja mwenyewe uone nani mshindi ingawa swali lilikuwa limekaa kizushi fulani ivi.
 
Pamoja na muundo usiokidhi wa swali la kipima joto, bado wananchi wakubaliana na kitendo cha wabunge wa upinzani kutoka nje ya bunge kwa asilimia 75!
 
Back
Top Bottom