Kipi muhimu: Madawati na vitabu au vitambulisho

TANURU

Senior Member
Jan 13, 2010
162
6
Wakuu,

Natumaini wote tumesikia kuwa Serikali itatumia jumla ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya Vitambulisho. Haya yanafanyika wakati karibu watoto milioni 4 wa shule zetu za msingi wanakaa chini na mbaya zaidi hali ya vitabu katika shule zetu zote ni ya kukatisha tamaa. Sekondari za kata ndiyo usiseme. Binafsi sioni umuhimu wa kutumia shilingi bilioni 200 kwa ajili ya vitambulisho wakati elimu yetu iko ICU.
 
Man, be serious!
Nani agombanie tenda za vitabu vya shilingi elfu moja moja badala ya hizo bilioni 200?
 
Ndugu yangu vyote ni muhimu labda ungesema kipi kipewe kipaumbele..lakini ukumbuke kwamba changamotoya vitabu na madawati ni tatizo sugu hapa nchini hivyo hata kama vitambulisho vikiwekwa pembeni bado pesa hizi zitaelekezwa kingine..tatizo ni priorities.
 
Serikali yetu haina vipaumbele. Vitambulisho vya urai tunavitaji sana lakini sio sasa! Wakati wake utafika tu.

Elimu Kwanza!
 
Serikali yetu haina vipaumbele.
...Na hili ndilo jibu la "Kwa nini nchi yetu ni masikini sana baada ya miaka yote hiyo ya uhuru". Hatujui tuanze na nini cha muhimu na tumalizie na kipi kingine! Watu hawana makazi kilosa kutokana na mafuriko, wanahitaji makazi bora, lakini sie twakimbilia kuchapa vitambulisho...
 
Ndugu yangu vyote ni muhimu labda ungesema kipi kipewe kipaumbele..lakini ukumbuke kwamba changamotoya vitabu na madawati ni tatizo sugu hapa nchini hivyo hata kama vitambulisho vikiwekwa pembeni bado pesa hizi zitaelekezwa kingine..tatizo ni priorities.

Nakubaliana na wewe kuwa ukosefu wa priorities ndiyo tatizo letu kuu.
Mkuu GS, tatizo la madawati tukiamua ndani ya mwaka mmoja tunauwezo wa kulimaliza kwani hatuhitaji zaidi ya shilingi bilioni 80 kulimaliza. Hayo ni makisio ya juu.
Ni bora mara mia hizo shilingi bilioni 200 tungeziwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji na matunda na faida yake ndiyo yakatumika kwa ajili ya hivyo vitambulisho.
Kwa utaratibu huu wa matumizi, tusahau kabisa kutoka hapa tulipo.
 
kama wakuu wengine walivyo sema na tulikwisha sema sana tu, tatizo ni priorities za CCM na serikali yake.

Kuna wakati unaweza kufikiri kuwa Tanzania haina watu wenye akili ndani ya serikali, hasa wizara ya elimu, miundo mbinu, madini na nishati, sayansi na teknolojia, mali asili, ardhi, n.k. angalau kidogo wizara ya mifugo na uvuvi.
 
Wakuu,

Natumaini wote tumesikia kuwa Serikali itatumia jumla ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya Vitambulisho. Haya yanafanyika wakati karibu watoto milioni 4 wa shule zetu za msingi wanakaa chini na mbaya zaidi hali ya vitabu katika shule zetu zote ni ya kukatisha tamaa. Sekondari za kata ndiyo usiseme. Binafsi sioni umuhimu wa kutumia shilingi bilioni 200 kwa ajili ya vitambulisho wakati elimu yetu iko ICU.

watakuja na sarakasi nyingi sana, personally sijaona hivyo vitambulisho vya uraia kwa nchi yetu vitasaidia nini, yaani watu wanajifanya kama sisi ni USA,! kuna interaction kubwa mipakani.

Bado kama tumeshaprove ufisadi, hivyo vitapatikana tu hata ambaye si raia, tena wanavyotangaza wengi watakuja watavichukua na kurudi makwao

Tulishapoteza system za ubalozi wanyumba kumi kumi, kutoa taarifa kwa mtu mgeni anayepanga mahali, vyeti vya kuzaliwa n.k

kwa mfano tungesema lazima kila raia awe na cheti cha kuzaliwa, na mtu anaanza kukitumia kuanzia anapoingia darasa la kwanza na kuwenye huduma nyingine muhimu za jamii!

Hii haina tofauti na alichosema JK 'flyovers' yaani tunawaza mambo makubwa bila kuprove au kuonyesha haya madogo yameshindikana
 
Hivi kipi muhimu.........!
Kumpeleka mwanao sekondari au kumpeleka veta?
 
Kinachonifurahisha hoja hii ya vitambulisho bungeni wote wanaitetea kua ni muhimu!! For now our system is corrupt na hakuna ground zozote zilizowekwa kuzuia huu ufisadi! Bilioni 200 zitatumika then what? kila mtu hata asie raia atapata hicho kitambulisho!! ila Elimu itabaki vile vile na hao ambao sio raia wenye ID yetu ndo watachukua kazi za watoto wetu!! Nimesikitishwa na Taaarifa kua Form 4 exam Zero 65,000!! wataenda wapi hawa?
 
Ee bwana ee! Hawa jamaa na hadithi za vitambulisho wametuchosha manake kila kukicha vitambulisho! kama vipi si waache wanunue zana bora za kilimo tulime ili tuishinde njaa?

Nadhani huu ni mradi tu wa vigogo ndo maana kila mara tunaambiwa uchambuzi yakinifu unaendelea. Mtaona mwaka utapita kama mingine ilivyopita bila vitambulisho wala vitumbua.

Tatizo letu wabongo ni siasa za maneno tu bila matendo. na huyu Masha sijajua atatueleza wakati wa kampeni. Dawa ya magugu shambani ni kuyang'oa tu!
Gene!
 
Huu mradi wa vitambulisho ni #$%$^$^&(**(^@#!@#** kabisa. Serikali yetu haijathibiti makazi ya wanachi wake halafu eti inataka kutumia mabilioni ya shilingi kununulia vitambulisho: vya nini?

Tanzania hatuna rekodi nzuri za vizazi na vifo na wala hatujui makazi ya raia wetu, je vitambulisho hivyo vitasaidia nini? Halafu ongea na Profesa Mbele akuambie kuwa watanzia ni wajinga wazembe hawakusoma ndiyo maana wanailaumu serikali bure.
 
watakuja na sarakasi nyingi sana, personally sijaona hivyo vitambulisho vya uraia kwa nchi yetu vitasaidia nini, yaani watu wanajifanya kama sisi ni USA,! kuna interaction kubwa mipakani.

Bado kama tumeshaprove ufisadi, hivyo vitapatikana tu hata ambaye si raia, tena wanavyotangaza wengi watakuja watavichukua na kurudi makwao

Tulishapoteza system za ubalozi wanyumba kumi kumi, kutoa taarifa kwa mtu mgeni anayepanga mahali, vyeti vya kuzaliwa n.k

kwa mfano tungesema lazima kila raia awe na cheti cha kuzaliwa, na mtu anaanza kukitumia kuanzia anapoingia darasa la kwanza na kuwenye huduma nyingine muhimu za jamii!

Hii haina tofauti na alichosema JK 'flyovers' yaani tunawaza mambo makubwa bila kuprove au kuonyesha haya madogo yameshindikana

Na tumeyasikia aliyokutana nayo Lukuvi hiyo jana wakati akitembelea Sekondari za kata. Kakuta wanafunzi wamekalia kanga na mifuko katika madarasa yao. Naona haya ndiyo madawati yetu mapya.
 
Kuwepo kwa proper citizen identification kunaweza kusaidia madawati yakapatikana mapema... so Vitambulisho kwanza.
 
Kinachonifurahisha hoja hii ya vitambulisho bungeni wote wanaitetea kua ni muhimu!! For now our system is corrupt na hakuna ground zozote zilizowekwa kuzuia huu ufisadi! Bilioni 200 zitatumika then what? kila mtu hata asie raia atapata hicho kitambulisho!! ila Elimu itabaki vile vile na hao ambao sio raia wenye ID yetu ndo watachukua kazi za watoto wetu!! Nimesikitishwa na Taaarifa kua Form 4 exam Zero 65,000!! wataenda wapi hawa?

Mbaya zaidi ni wanafunzi elfu 42 tu ndiyo wamepata Division I, II na III kati ya wanafunzi zaidi ya 339,000 waliofanya mtihani. Zaidi ya wanafunzi 230,000 wameambulia Division IV. Balaa tupu. Badala ya kuboresha elimu, shule zetu na vyuo vya ualimu tunakimbilia vitambulisho. Mimi sioni hicho kitambulisho kitanisaidia nini katika uhalisia wetu. Hivi na watoto wetu walio chini ya umri wa miaka 18 nao watapewa hivyo vitambulisho?
 
msiseme kuwa serikali ya ccm haijui ku prioties mambo!
vitambulisho vinapewa kipaumbele zaidi kwa sasa kwa kuwa muda si mrefu kutakuwa na uchaguzi na hivyo raia wenye hivyo vitambulisho ndio watakaokuwa na uwezo wa kupiga kura..kwa hiyo kitu cha msingi hapa ni kuhakikisha wamewapa watu vitambulisho ili wakawapigie kura na kushinda kwa kishindo japokuwa hata wahindi walioko india kwa sasa(watu wasio raia) watavipata hivo vitambulisho tena fasta hata kabla ya babu yangu kule kijijini kupata. so madawati ya nini? wakati madawati yatakwenda kutumiwa na watoto wa primary ambao hata hawajafikia umri wa kupiga kura? wewe huoni kuwa hiyo ni loss kwao?
 
Pia mkumbuke kuwa idadi ya Watanzania wasiojua kusoma na kuandika ni zaidi ya milioni 13---Asilimia 30 ya Watanzania wote. Aibu tupu. Hapo hujaweka mamilioni ya Watanzania ambao hawana ujuzi wa aina yoyote ile. Kazi ipo.
 
Tanzania ni nchi 'isiyo na mwenyewe'; kwa hiyo 'hairuhusiwi' kuwa na vitambulisho vya taifa.
 
Kwa utaraibu wa nchi yetu muhimu ni kile kinachowaneemesha wakuu..............ufisadi kila mahali
 
Back
Top Bottom