Kipi Kiswahili sahihi?

Babuyao

JF-Expert Member
Jun 6, 2009
1,741
272
Kina mama wenye watoto daima wanaitwa kwa majina ya watoto wao, mf. kama mtoto wake anaitwa "Mfaume" basi mama yake ataitwa "Mama Mfaume". Miaka ya karibuni - kama sikosei - kina mama wamekuwa wakiitwa kwa majina ya waume zao pia. Mfano utasikia "Mama Kikwete" wakimaanisha mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Swali 1. Kiswahili kipi ni sahihi kati ya misimamo hiyo miwili hapo juu?
Swali 2: Kwa nini kina baba wanaitwa kwa majina ya watoto wao tu na si ya wake zao? Mf. utasikia "Baba Mfaume" lakini si "baba . . . (likitajwa jina la mkewe)?
 
Jina kazi yake ni kumtambulisha mtu na mara kadhaa kwa kumtofautisha au kumhusisha na watu wengine(wakati mwingine vitu) ambao tayari wanajulikana.

Inategemea pia ni nani anaita:

- Kama ni mtoto wake (ataita "mama")
- Kama ni mume au watu wengine wanaofahamu kuwa ana mtoto anaitwa mafaume (wataita "Mama Mfaume")
- Watu wanaofahamu kuwa ameolewa na Mumewe anaitwa Kikwete na pengine hawajui kama ana mtoto au hawafamu majina ya mmojawapo wa watoto wake (wataita " Mama Kikwete" - Mama hapa inabadilika maana na kuwa 'mke wa' au 'Mrs')

Mazingira pia yanaweza kubadili jinsi ya kuita: kwa mfano mama yako akiwa kwenye umati wa kina mama, utamwitaje?

Kumbuka kuwa kimazoea, si 'adabu' kumuita mama mtu mzima (aliyekuzidi umri) kwa jina lake la mwanzo katika mazungumzo au mawasiliano ya kawaida ya kinyumbani na yasiyo rasmi (informal). Wazungu wenzetu hii siyo shida kabisa!
 
Katika desturi za Kiswahili ukisema "Mama kikwete" unamaanisha yule mwanamke aliyemzaa / mama yake Kikwete.

Haya mambo ya kumwita Salma Kikwete "Mama Kikwete" yanatokana na kuiga kiingereza cha "Mrs. Kikwete".It can be really confusing.
 
Kuhusu wanaume kutoitwa kwa majina ya wake zao nadhani ni matokeo ya mfumo dume mbao wanawake bado wanapambana nao. Kumbuka kwamba katika jamii nyingi mwanamke alikuwa ni kama "mali" ya mume na kwa lojiki ya kawaida mmiliki hawezi kuitwa kwa jina la mmilikiwa. Kufanya hivyo ni kumdogosha yeye na umiliki wake.
 
Jibu lipo katika uIslam, kila mmkoja anabaki na jina lake kama lilivyo, hakuna kubadili jina au majina kutokana na kuolewa.
 
Jibu lipo katika uIslam, kila mmkoja anabaki na jina lake kama lilivyo, hakuna kubadili jina au majina kutokana na kuolewa.

Kwasababu talaka ni nje nje katika uislamu ndo maana mnafanya hivyo. Mnaoa kwa kuegeshea tu si hivyo katika ukristo. Sisi ni mpaka kifo kiwatenganishe ndo maana tunadiriki kubadili majina baada ya ndoa. Marriage is a godly bond in christianity.
 
Kwasababu talaka ni nje nje katika uislamu ndo maana mnafanya hivyo. Mnaoa kwa kuegeshea tu si hivyo katika ukristo. Sisi ni mpaka kifo kiwatenganishe ndo maana tunadiriki kubadili majina baada ya ndoa. Marriage is a godly bond in christianity.

Waungwana,

Kujibu swali ni kulielewa swali. Kipi Kiswahili sahihi? Hapakutajwa dini kwenye swali? Jinsi gani sahihi katika utamaduni wa Kiswahili? sio utamaduni wa kidini!

Mama katika Kiswahili sanifu ni yule mzazi, awe mzaa mtoto au mzaa chema. Lakini, katika utamaduni wa Kiswahili, jina la 'mama" linaweza kutumika kama ishara ya 'kuheshimu.'

Katika hali hii mtu anaweza kumwita mwanamke yeyote 'mama." Ndipo mtu anaweza kusikika akimwita hata binti yake mwenyewe, "mama."

Anapoitwa mtu "Mama Fulani." Maana halisi ni kuwa huyo ni mzazi wa huyo "fulani." Na kiutamaduni, ndani ya mwito huo, mna heshima ya aina yake.

Hili la kuitwa mwanamke kwa jina la mumewe ni la uigaji wa tamaduni za kigeni.
Si sahihi katika lugha wala utamaduni wa Kiswahili.
 
Kwasababu talaka ni nje nje katika uislamu ndo maana mnafanya hivyo. Mnaoa kwa kuegeshea tu si hivyo katika ukristo. Sisi ni mpaka kifo kiwatenganishe ndo maana tunadiriki kubadili majina baada ya ndoa. Marriage is a godly bond in christianity.
Hivi wakiristu hawaachani... eh!? Hivi upo dunia ya wapi?
 
Hili la kuitwa mwanamke kwa jina la mumewe ni la uigaji wa tamaduni za kigeni. Si sahihi katika lugha wala utamaduni wa Kiswahili.

Jamani lugha ya kiswahili inakua. Neno haliachi kuwa sahihi eti tu kwa sababu limeigwa kutoka tamaduni/lugha nyingine! Kiswahili ni zao la tamaduni/lugha za kigeni pamoja na kibantu na kinaendelea kukua katika mazingira hayohayo ya kukopa au kutohoa maneno mbalimbali kutoka kibantu na lugha za kigeni.
 
mwanamke kubadili jina na kutumia jila la mumewe badala la baba yake mzazi ni kujidhulumu na kujidhalilisha mwenyewe.

Kila mtu atumie jina lake hata kama mnaoana
 
Back
Top Bottom