Kipi Kimemkuta Jairo?

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
182
Ndugu zangu,
Nchi yetu sasa imekumbwa na masika ya habari, imekuja na mafuriko pia. Ndio, kuna tuliofunikwa na mafuriko ya habari, hatujui ni ipi ya kuanza nayo.

Lakini, hili sakata la Jairo na Bunge ni burudani pia. Tafsiri yangu inakuja siku sijazo. Nimeona nianze na mkanganyiko huu; najiuliza, hivi Jairo kapelelekwa likizo, kasimamishwa au kapumzishwa?
Si tuliambiwa kuwa Jairo alikuwa kwenye likizo fupi ya malipo? Juzi hapa karudishwa kazini kwa mbwembwe, au tuseme kakatishwa likizo yake na Katibu Mkuu Kiongozi. Na sasa karudishwa kwenye likizo ndefu na Mheshimiwa Rais!

Ni likizo ndefu kwa vile itasubiri mpaka Kamati Teule ya bunge imalize uchunguzi wake, si leo, si kesho. Maana, ripoti ya uchunguzi itasomwa na kujadiliwa bungeni Novemba mwaka huu. Ndio, mwezi kabla ya Krismasi na kufunga mwaka. Hivyo tunaweza kusema; likizo ya Jairo inaweza kuunganishwa na likizo yake ya Krismasi. Huu ni mkanganyanyiko, au?

Na vipi hao watumishi wanaosukuma gari la Jairo pichani? Yaonekana walichukua ' Mapumziko mafupi' . Wakaacha ofisi zao na kwenda kusukuma gari la Jairo. Au labda walikuwa wanakwenda kazini na njiani wakaliona gari la Katibu wao Mkuu, kisha wakaitana na kuanza kulisukuma!

Na aliyechangisha fedha za maua ya kumkaribisha Katibu Mkuu naye aliacha ofisi yake na kupita kila idara kuchangisha, au?

Na Utumishi wa Umma una miiko na maadili yake. Inasemwa; Goverments will come and go, but civil servants will stay. Ndio, Serikali huja na kuondoka, lakini utumishi wa umma hubaki pale pale.

Ni kukiuka miiko na maadili ya Utumishi wa umma kwa jamaa hao pichani kuacha kuutumikia umma na kumtumikia mtendaji wa Serikali, tena kwa kusukuma gari lake! Tunajua, kuwa Civil servants nao ni binadamu; wana ushabiki wa Simba na Yanga, Man United na Chelsie, CCM na Chadema na mengineyo. Lakini, weledi kwa maana ya profesionalism ni kuweka ushabiki kando na kufanya kazi ya utumishi wa umma, kwa serikali yeyote iwayo, ali mradi imechaguliwa na wananchi.

Na Ngeleja nae kwenye picha ndogo? Naye ni habari, ni burudani pia. Lakini, hata kwenye football kuna half time. Twendeni kwenye ' mapumziko' mafupi! Vinginevyo, tutapelekwa ' likizo ndefu'- Isiyo na malipo itakayopelekea ' pumziko la milele'!

Maggid,
Iringa.
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
 
sarakasi nchi yetu hii hazitaisha mkuu. kwa inshu hii mtu unajiuliza maswali mengi yanayokosa majibu mpaka kichwa kukaribia kuuma! lakini acha tu,,hakuna marefu yasiyokuwa na ncha!
 
Majjid maswali ni mengi sana ya kuhusu Jairo hayataisha mpaka tutakapo kuwa na serikali ya wananchi lakini sio hii ya majambazi
 
"of course" hii inaonesha jinisi hali ilivyo mbaya kwenye utumishi wa umma serikalini! Kuna watu ni wafalme katika viofisi vyao na hakuna mtu wa kuwagusa. Sasa huyu anaonesha ufalme wake pale nishati na madini!!

Hii inaendelea kutuma ujumbe ulio wazi kwa kila mtu kuwa mambo hayaendi vizuri serikalini, ikiwa utawala wa sheria ndo kitu tunachozungumzia.
 
Sasa watu wameshaanza kujionea wenyewe bila hata kuambiwa na chadema na hili ni funzo kubwa sana kwa wananchi wasipo elewa hapa hakuna sehemu nyingine watakapoelewa somo na ndipo hapa pa kuanzia kuchukua uamuzi mgumu bila kusubiri mkuu wa kaya kwa sababu yeye kaonesha udhaifu wake mapema
 
tatizo ni mzunguko unaolazimishwa kuwepo kwa ajili ya jairo kwani maamuzi yalitakiwa yawe mara moja c kwa kupingana na kukinzana
 
Huyo David Jairo asikae bure wkt
analipwa mshahara bure, NASHAURI
APEWE VIPINDI VYA HESABU KATIKA
SHULE MOJA YA SEKONDARI
AFUNDISHE!
 
Jairo amekuwa mtu wa kwenda likizo tu, nadhani kanuni za utumishi wa umma zinzruhusu likizo ya siku 28 kwa mwaka sasa yeye anaelekea kuzidisha siku hizo maana kala siku zake 28 + alipewa na Luhanjo 20 + alizopewa na Swahiba wake (JK) hazijzjulikana!
 
Huyo David Jairo asikae bure wkt
analipwa mshahara bure, NASHAURI
APEWE VIPINDI VYA HESABU KATIKA
SHULE MOJA YA SEKONDARI
AFUNDISHE!

Ooh! Gagurito inabidi huu ushauri wako uangaliwe kwa makini asije akaleta mambo ya yule mwalimu wa computer kwenye tangazo la Haki Elimu aliyeandika SIPIYU kwa mbwembwe akimaanisha CPU. Au ya yule mwalimu wa hesabu aliyeng'ang'ania kutamka square root bila kufundisha kitu mpaka kipindi kinaisha.
 
Jairo kapewa likizo ndefu ya malipo na rafiki yake JK. Walikubaliana kabisa kwamba wewe nenda ukapumzike hawa wapige pige kelele zao wakishatulia utarudi uendelee na shughuli zako bila matatizo yoyote. Kama hawakukubaliana haya, tutaona kama Jairo atachukuliwa hatua yoyote.
 
Back
Top Bottom