Kipi chuo kikuu bora Tanzania?

Mkuu nakushauri nenda pale UDSM utapata hostel za vitanda bila godoro mabibo hostel lakin mwisho wa siku utatoka na jiwe la ukwel.
kweli mtu usipate mazingira mazuri useme utapata jiwe la ukweli???? we mzima kweli?? hiyo ni elimu au tunadanganyana??
 
kwa nyanja gani majengo??? hostel za kubebana kama magunia ya mpunga?? uhuni??? mchango katika kuiua tanzania yetu??elimu au nini!!! SIWEZI KUBALIANA NA KAULI YAKO!!

Yote hayo uliyoyataja sio dhamira na msingi wa kuanzishwa UDSM na vingine, hizo ni changamoto tu. mi na maaanisha kwa ubora wa elimu, Kama unabisha mpeleke mwanao Chuo cha kata Kama UDOM.
 
Yote hayo uliyoyataja sio dhamira na msingi wa kuanzishwa UDSM na vingine, hizo ni changamoto tu. mi na maaanisha kwa ubora wa elimu, Kama unabisha mpeleke mwanao Chuo cha kata Kama UDOM.
sasa hizo changamoto si ndio zinabomoa elimu...sasa utasemaje kuna elimu nzuri wakati hakuna mazingira mazuri ya kusoma(hapa naongelea zaidi hosteli)...
 
sasa hizo changamoto si ndio zinabomoa elimu...sasa utasemaje kuna elimu nzuri wakati hakuna mazingira mazuri ya kusoma(hapa naongelea zaidi hosteli)...
Hata kwa baba yako (kwenu) kuna changamoto, sasa hizo changamoto za kwenu zinaweza kukufanya useme kule sio kwenu au Yule sio baba yako? ukwelii unabaki pale pale kuwa kule ndo kwenu na Yule ndo baba yako. Changamoto za UDSM haziondoi ukweli kuwa Ndicho Chuo kukuu ambacho bado kinaaminika kutoa elimu bora kwa hapa TZ. Na kumbuka mtoa Uzi aliuliza Chuo kizuri ukilinganisha na vingine kwa hapa TZ. Hata ukiambiwa chagua mgonjwa mwenye nafuu, huwezi kwenda ICU, utakwenda wodini.
 
Haswaaaaa. TZ Nzima hakuna Kama UDSM mpaka sasa

udsm generally as university mtajisifu bt 2kija kwenye specific program udsm mnazidiwa na vyuo viiingi mfano B.com ya udsm haiwezi kucompete na Baf ya Muccobs(Sua),engenering programs ziko nyuma ya DIT,nk so dogo sema program gan unapenda watu tukusaidie bila ushabiki.
 
Mie nashauri alisoma vyuo vyote tanzania ndo ana haki ya kumake comparison!

Wewe umesoma chuo kimoja say mzumbe then una disqualify udsm wakati haujawai kusoma pale!

So hamna aliyetimiza sifa ya kusoma vyuo vyote tanzania! All the arguments are nonsense!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Yote hayo uliyoyataja sio dhamira na msingi wa kuanzishwa UDSM na vingine, hizo ni changamoto tu. mi na maaanisha kwa ubora wa elimu, Kama unabisha mpeleke mwanao Chuo cha kata Kama UDOM.

Tatizo lako hujafikiria kabla ya kuandika! UDOM imejengwa kwa kodi za Watanzania hivyo haupaswi kukikebehi kwa kusema ni chuo cha kata. Toa hoja za msingi kuonesha uwezo wako wa kufikiria na sio kukurupuka. UDOM ina Degree Programs ambazo vyuo vingine hakuna, sasa kama ndugu yako kakuomba ushauri ndiyo utajibu hivyo? Kwanza level yako ya Elimu ikoje? Usikute nakuonea
 
Chuo kikuu ni bora kutokana na kozi yake.
UDSM sheria
SUA kilimo na mifugo
Mzumbe Human rm
Dogo unazingu bila juu ya GPA 10 usijaribu hivyo vyuo.
Tafuta Tumaini ya Dar. Unakata nguo bila mtoto kuzaliwa.
ni kozi yake au kozi zake??? na kama nikisoma computer engineering UDSM ntakua nimekosea maana unasema UDSM ni sheria tu!!! na nikisoma BAF mzumbe ntakua nimkosea??? usiwe mwoga eleza ueleweke!!!!
 
udsm generally as university mtajisifu bt 2kija kwenye specific program udsm mnazidiwa na vyuo viiingi mfano B.com ya udsm haiwezi kucompete na Baf ya Muccobs(Sua),engenering programs ziko nyuma ya DIT,nk so dogo sema program gan unapenda watu tukusaidie bila ushabiki.

muccobs iko tanzania au?
 
Tatizo lako hujafikiria kabla ya kuandika! UDOM imejengwa kwa kodi za Watanzania hivyo haupaswi kukikebehi kwa kusema ni chuo cha kata. Toa hoja za msingi kuonesha uwezo wako wa kufikiria na sio kukurupuka. UDOM ina Degree Programs ambazo vyuo vingine hakuna, sasa kama ndugu yako kakuomba ushauri ndiyo utajibu hivyo? Kwanza level yako ya Elimu ikoje? Usikute nakuonea
Alimwambia nani Chuo kukijengwa kwa kodi za wananchi ndio kinakuwa Chuo kinachotoa elimu bora? Hebu soma kwenye matangazo ya kazi uone na ujiulize ni kwa nini baadhi ya Taasisi zinapotangaza nafasi za kazi kwa mtu mwenye digrii yoyote lkn wanaweka ..."isipokuwa digrii ya UDOM". Kama wewe ni mwl au kiongozi UDOM, nakushauri tafakari sana utagundua kuwa mnazalisha matatizo badala ya kiyapunguza. Poleni
 
Mbona nahisi hapa kila mwamba ngozi anavutia kwake lolz!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
1.udsm baba yao, kinafwata 2.SUA, 3.Mzumbe,4.Muhimbili....vingine ni vyoo vikuu...nasapoti kauli ya Dr Lymo

Mrembo naomba unifafanulie hapo kwenye namba 1 na namba 4, unapotaja ubora umezingatia kitu gani.

Kwa mwanafunzi anatakiwa aangalie rank ya kozi yake katika chuo husika kulingana na kozi hiyo katika vyuo vingine vitoavyo kozi hiyo.

Je kozi zinazopatikana muhimbili zinapatikana pia udsm(provided ni vyuo tofauti)?, Na kama sio hauoni kuwa unalinganisha na vitu ambavyo havifanani?
 
Angalieni ranking ya vyuo kwa afrika, mtajua chuo gani ni bora zaidi kwa Tanzania. Ila ubora unaangalia vile vile na aina ya program zinazotolewa. Kwa sheria nenda UDSM au Mzumbe, Engineering bado itakuwa ni UDSM, Agriculture SUA, Journalism (UDSM), Medicine (Mhimbili) etc. Ukweli ndo huo. Baadhi ya vyuo vingine bado vinatumia wahadhiri wa UDSM.
 
Back
Top Bottom