Kipi Choo?

Chomsky

Member
Jul 15, 2012
31
5
Nini maana halisi ya neno "choo"?

Hospitali ukiagizwa choo unapeleka kinyesi. Hii sawa.

Sehemu watu wanakwenda haja pia panaitwa choo. Na hii ni sahihi.
Je, wadau, "choo" nini? Ni kinyesi au ni sehemu ya kwenda haja? Au kuna maana nyingine zaidi?
 
mkuu kiswahili kigumu na nisomo gumu kwa upande wangu analiogopa kuliko masomo mengine yote.

Choo Nomino (noun) - Kinyesi (hii ndiyo tafsiri yangu)
|
Shimo la choo - shimo la kinyesi (haja kubwa) - {(kumbuka hakuna shimo la choo (kinyesi) kwa maana ya haja ndogo

(mkojo) ni kwa haja kubwa tu}.
Sio lazima sehem ya haja ndogo kuwa choo (sehemu ya kinyesi), lakini kwa haja

kubwa (choo) inawezekana kutumika kwa haja ndogo yaani (mkojo)

Nyumba inachoo ??? ( nyumba inasehemu ya kuhifadhia choo? hapa kuna kama tafsida kulainisha lugha na kutoa

muugurumo mzuri zaidi wenye utamu masikioni na kwa ufupi kuwakilisha ujumbe.

Naenda chooni - Naenda sehemu kilipo kinyesi (sehemu ya kuhifadhia Kinyesi) - Naena Dukani, naenda mkutanoni

Hivyo kwa mtazamo wangu neno Choo linamaanisha Kinyesi, na pia kulingana na matumizi linawakilisha sehemu ya

kujihifadhi - haja zetu (haja kubwa)
Haijalishi ni cha kike au kiume kote ni sehemu ya kuhifadhia kinyesi
Wataalamu wa kiswahili watatusaidia zaidi.
 
Nini maana halisi ya neno "choo"?

Hospitali ukiagizwa choo unapeleka kinyesi. Hii sawa.

Sehemu watu wanakwenda haja pia panaitwa choo. Na hii ni sahihi.
Je, wadau, "choo" nini? Ni kinyesi au ni sehemu ya kwenda haja? Au kuna maana nyingine zaidi?

mkuu upo?
 
Sometimes maana ya maneno tunaijua kutokana na jinsi ilivyotumika.Mambo ya hospital yalianza kwa wenzetu hata maneno mengi yanayotumiwa kwa vipimo vya maabara tukitaka the swahili version ya hayo maneno maisha yatakuwa magumu.
Kwa wenzetu katika medical stool=The solid waste that is left after food is digested. Stool forms in the intestines and passes out of the body through the anus.Na urine inajulikana ni nini.
Sasa tukija kwenye kiswahili stool utaiitaje kwa jina na siyo maelezo marefu?Kwa hiyo kufanya shughuli ziwe rahisi Stool=choo kwa kutumia fafsida,ukimwambia mtu kalete kinyesi chako au lile neno jingine ma** yako kidogo hayajakaa vizuri.Kwa hiyo,ni sahihi hilo neno linavyotumika sehemu za hospitali tu.
Ni kama hoteli zetu,nani ugali nyama?nani chipsi kavu?Unaitikia mimi hapa,ingawa wewe siyo ugali nyama au chipsi kavu.
 
Chomsky

Neno choo lina maana 3

1. choo = toilet, restroom, latrine.

2. choo
= faeces:

Sampuli ya choo =
stool, specimen.

(1) choo kikubwa = faeces;
(2) choo kidogo = urine;
(3)Funga choo =
be constipated;
(4) pata/enda choo =
have a motion, defecate.

3. choo = light-brown worm used as fish bait.
 
Nadhani ni tafsida au upunguzaji wa ukali wa neno mavi/kinyesi kutoka kwa wataalamu wetu wa afya.

Walikaa chini wakajadili wakaamua kutumia neno CHOO badala ya maneno mengine ambayo ni makali zaidi.

Sasa CHOO kama CHOO ni sehemu maalum iliyojengwa kwa madhumuni ya mwanadamu kwenda haja ndogo au kubwa.
 
Yote ni sawa. Ina maana ya mahali palipotengwa kwa kwenda haja. Pia msalani. Vilevile, choo inamaanisha uchafu unaotoka kwenye tupu ya mbele au ya nyuma.
 
nini maana halisi ya neno "choo"?

Hospitali ukiagizwa choo unapeleka kinyesi. Hii sawa.

Sehemu watu wanakwenda haja pia panaitwa choo. Na hii ni sahihi.
Je, wadau, "choo" nini? Ni kinyesi au ni sehemu ya kwenda haja? Au kuna maana nyingine zaidi?

unafahamu maana ya neno tafsida? Kama hapana, tafuta kamusi ya kiswahili, utapata majibu mazuri humo!!!!! Kwa nini choo si kinyesi au mavi....!!
 
Back
Top Bottom