Kipawa kunani?

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Nakumbuka miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na tetesi mbili, ya kwanza, kwamba aliyekuwa Rais wa Marekani, George Walker Bush na wenzake, walikuwa wamekingia mkataba na Serikali ya Awamu ya Tatu, kuja kuwekeza kwenye eneo la Kipawa, kujenga majengo ya kisasa ya kibiashara pamoja na hoteli za kifahari. Tetesi ya pili ilikuwa Serikali yetu hiyo ya Awamu ya Tatu ilikuwa imeingia mkataba na Marekani kutumia eneo la Kipawa kujenga kambi maalum ya Jeshi la Anga la Marekani, ili kuwawezesha kutumia eneo hilo katika mikakati yao ya kupambana na "ugaidi".

Sasa wameondolewa Watanzania waliokuwa wakiishi Kipawa, kuna walioridhika na ambao hawakuridhika na jinsi ambavyo waliondolewa, katika kile kilichoitwa "upanuzi" wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Mojawapo ya magazeti ya leo linatamka kwamba eneo la Kipawa sasa kujengwa hoteli za kifahari. KULIKONI?

Wadau naomba ufafanuzi.

Asanteni.

./Mwana wa Haki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom