Kipaumbele cha MKIKWATA kiwe ni umiliki wa ardhi kwa mlala hoi

Apr 4, 2012
56
3
Sisi kama wadau wakubwa wa ardhi, hususan mashamba, viwanja na nyumba, tunapenda kuhimiza serikali kuweka kipaumbele cha umiliki wa ardhi kwa mlala hoi katika Mkakati wa Kilimo Kwanza Tanzania - MKIKWATA.

Bila ya walala hoi kuwezeshwa katika kumiliki ardhi, pengo la walio nacho dhidi ya wasio nacho litaongezeka na kukwamisha maendeleo yaliyokusudiwa katika dhana nzima ya MKIKWATA.

Tunaunga mkono kwa dhati MKIKWATA, ila tunatoa tahadhari kwa jamii juu ya changamoto zinazojitokeza katika suala zima la umiliki wa ardhi, kwa nia njema kabisa ya kufikia malengo yaliyokusudiwa.
 
MKIKWATA?!, mbado mimi kusikia.!
Gama sera ya kilimo imebainisha wazi kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa hili. MKIKWATA = Mkakati wa Kilimo Kwanza Tanzania, na tayari Rais Obama ametoa shavu kwa kuahidi mamilioni ya dola za marekani kusapoti MKIKWATA ili kuondoa njaa na kuinua pato la taifa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom