Kipanya kaua bendi leo

Mi sijuia vyuo vikuu huwangali nini au mchango gani hasa ili kumtunuku mtu degree ya heshima...mimi naona Kipanya nae anastahili Phd ya heshima kwa mchango wake katika jamii
 
Mi sijuia vyuo vikuu huwangali nini au mchango gani hasa ili kumtunuku mtu degree ya heshima...mimi naona Kipanya nae anastahili Phd ya heshima kwa mchango wake katika jamii

offcourse anastahili ila wanasiasa wanapewa hiizi sio kwa kile walichoifanyia jamii ila kwa sababu wanalipwa fadhila kutoka kwa wale waliowateua
 
hivi kitu gani wabongo tuliwahi kushinda!?labda yaanzishwe mashindano ya wizi, ufisadi kuchakachua na kupiga dili hapo nnaimani tutakua washindi no 1 duniani
 
tumepata sababu ngapi leo?

Taifa Stars yachafua hali ya hewa

<tbody>
</tbody>
Wednesday, 29 February 2012 21:06
0digg

nyuma-ni-ngasa.jpg
Beki wa timu ya Taifa ya Msumbiji Almiro Lobo (mbele), akijaribu kumdhibiti winga wa Taifa Stars, Mrisho Ngassa (nyuma) wakati wa mechi ya kwanza kuwania nafasi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na Jackson Odoyo

Sosthenes Nyoni
HALI ya hewa ilichafuka kwenye Uwanja wa Taifa jana baada ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kulazimisha sare ya 1-1 na 'The Mambas' katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kucheza Fainali za Afrika 2013 nchini Afrika Kusini.Wakati mpira ulipokuwa unaanza, kila mmoja alikuwa na mtazamo wake, baadhi walikuwa wanaipa nafasi Taifa Stars kuwa itashinda na wengine hapana, hasa baada ya kuona orodha ya wachezaji watakaocheza.

Mara baada ya mchezo, baadhi ya mashabiki walikuwa wakipiga kelele kuwa kocha wa timu hiyo, Jan Poulsen aondoke pamoja na benchi la ufundi linalosimamiwa na Sunday Kayuni, huku wengine wakilaumu wachezaji kuwa hawana uwezo.

"Mnalaumu kocha ili afanyeje, hao ndiyo wachezaji wenu, mnataka nini hapo, nafasi alizokosa Boko mnataka kocha afanye nini?," alisikika shabiki mmoja baada ya mchezo.

Hali hiyo iliwafanya polisi kuanza kuwatawanya mashabiki hao waliokuwa wamejikusanya huku wakipiga kelele za kutaka Poulsen atimuliwe pamoja na TFF nzima.

Matokeo hayo ni mwanzo mbaya wa Tanzania katika safari ya kuwania tiketi hiyo ya 2013.

Stars walitawala mchezo kwa kiasi kikubwa hasa kipindi cha pili, lakini walicheza ovyo kipindi cha kwanza licha ya kumaliza kwa sare ya 1-1.

Kocha wa Msumbiji, Gert Angles alisema amefurahishwa na sare hiyo ambayo kwake ni kama ushindi baada ya kushuhudia kikosi chake kikizingirwa na mashambulizi mfululizo sehemu kubwa ya kipindi cha pili.

"Ni matokeo mazuri kwetu, (sare) tunajiandaa kwenda kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano nyumbani," alisema kocha huyo ambaye ni wazi alikuwa na kila sababu ya kushangilia sare hiyo.

Msumbiji walikuwa wa kwanza kuliandama lango la Stars katika dakika tano za kwanza, baada ya washambuliaji wake kumjaribu kipa wa Stars, Juma Kaseja kwa mashuti ya mbali.

Dakika tano baada ya filimbi ya kwanza, mshambuliaji wa Msumbiji, Jerenias Sitoe alipiga shuti la mwendo mrefu lililopaa juu ya lango la Stars, kabla ya Stars nao kujaribu kwa stahili hiyo baada ya shuti la kiungo Mwinyi Kazimoto kupaa juu ya lango la Msumbiji dakika ya 8.

Msumbiji ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 23 kupitia mshambuliaji wake, Bauque baada ya kuwazidi mbio mabeki Juma Nyosso na Aggrey Moris kisha kupiga shuti lililomshinda Kaseja.

Baada ya bao hilo, Stars walionekana kama wamepoteana lakini walijipanga kadri dakika zilivyosogea huku wachezaji wake, Mwinyi Kazimoto, Abdi Kassim na Vincent Barnabas wakijaribu kupandisha mashambulizi.

Mipango yao ilitimia zikiwa zimesalia dakika tatu kabla ya mapumziko baada ya Barnabas kunyunyiza majalo na mpira kumkuta Kazimoto umbali wa mita 30 na kuachia fataki iliyokwenda wavuni.

Kipindi cha pili Poulsen aliwapumzisha Nizar Khalfan aliyecheza ovyo na Barnabas na kuwaingiza Mrisho Ngassa na Hussein Javu katika dakika ya 55 kabla ya kumtoa Kassim na kumuingiza Salum Aboubakar.

Mabadiliko yawaliwapa nguvu Stars lakini tatizo kubwa ni mipango ya kufunga. Hata hivyo, dakika ya 66, mpira wa Mrisho Ngassa uligonga besela kabla ya Kaseja kuokoa 'boko' la Nyosso aliyetoa pasi kiduchu kwa Mwasika na Sterio Ernesto akaunasa kabla ya Kaseja kufanya kazi ya ziada kuokoa mpira huo.

John Boko aliyesimama mbele, alishindwa kabisa kufunga huku akikosa mabao matano ya wazi, matatu kipindi cha kwanza na mawili dakika 45 za mwisho.

Akizungumza baada ya mchezo, kocha wa timu hiyo, Poulsen alielezea kufurahishwa na matokeo, lakini akasema mechi ilikuwa ngumu.

Alipoulizwa juu ya Mbwana Samatta ambaye pengine angeweza kuzitumia nafasi za Boko, alisema kuwa alikwishampa majaribio mechi za Morocco na Chad lakini habadiliki na hakufunga na kamwe hawezi kumuita.

"Kama Watanzania mnamtegemea Samatta, mtasubiri hadi Krismasi, kamwe simuiti, nilishampa nafasi kashindwa, kazi yake anapenda 'anaoanao' na hafungi...hataki kubadilika," alisema kwa ghadhabu na kugonga meza kisha kunyanyuka na kuondoka.

Mwananchi ilimfuata katika viwambaza vya Uwanja wa Taifa na kumuuliza kama atajiuzulu nafasi hiyo alisema: "Siyo mimi, ni wachezaji wenu, mimi siwezi kujiuzulu...nijiuzulu kwa kipi?."

Tanzania na Msumbiji zitarudiana baadaye Juni, mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Machava, Maputo.

<tbody>
</tbody>
 
Haika utakuwa lazma mtumishi wa umma! Yaani wakale bata kenya kujifunza kukimbia? Manake umenikumbusha trip za wakubwa kwenda kujifunza wenzetu wanatreat vipi maji taka,lol

umesahau mama mwanaasha anavyozunguka kuwafundisha watz kunawa mikono kwa hisani ya wamarekani!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom