Kipandauso (migraine): Chanzo, Dalili, Tiba na jinsi ya kujikinga na tatizo hili

Mkuu FLASH HIDER Sijatosheka na maelezo yako na siwezi kukupa dawa mpaka uniambie kwa kirefu je ulikwenda Hospitali gani? Je umefika hata Muhimbili? Huna Matatizo ya Ukosefu wa kupata choo?

Kuumwa na kichwa / kipandauso

Maumivu ya kawaida ya kichwa huweza kutulizwa na dawa za kuzuia maumivu za aina ya Panadol au aspirini.Iwapo unahisi hayo maumivu kwenye kipji cha uso wako, mashavuni na

sehemu zilizo karibu na macho zikifura, kuna uwezekano kuwa umeambukizwa sehemu za kukaza pumzi puani.Iwapo utashikwa na maumivu makali ya kichwa ambayo hayapoi, haikosi

kuna uwezekano kuwa umeanza kushikwa na ule ugonjwa sugu wa kipandauso.
Kipandauso (migraine) kina maumivu zaidi kuliko kuumwa kichwa kwa kawaida.Kipandauso

huathiri upande mmoja wa kichwa na kuleta kisunzi,au kutaka kutapika.Iwapo unahisi kipandauso unaweza kuona vimulimuli kutokana na muangaza.Pia unaweza kuhisi maumivu

makali kwenye jicho moja mara kwa mara.

Ukipatwa na kipandauso, muone daktari wako akuchunguze ili akupe ushauri .Unapopatwa na kipandauso lala chini palipo na utulivu katika chumba kilicho giza kuzuia miale ya jua

yanayosababisha kichwa kiume zaidi.

Jaribu usinywe kakao, pombe ama kinywaji chochote kilicho na kakao.Hivi vinaweza kusababisha kipandauso, kunywa maji mengi kila siku.

Utahitajika kumuona daktari ikiwa:
  • Unaumwa na kichwa na hakipoi kwa muda wa juma moja ingawa umemeza dawa za kuzuia maumivu.
Utahitajika kwenda kwa chumba cha dharura ikiwa:
  • Una matatizo unapozungumza, au unasikia kizunguzungu, miguu haina nguvu. Kuna uwezekano kwamba umeanza kupatwa na ugonjwa wa pigo.

Nashukuru sana kwa maelezo. Nahisi hizi ni dalili za kipanda uso kama ulivyoelezea. Sina tatizo na choo. Mmwezi May nilienda Mwananyamala Hopital nikaambiwa huenda ni tatizo la macho. Nilionana na mtaalamu huyo ambaye baada ya kunipima nikaonekana nipo safi tu. Nikapewa dawa za maumivu ambazo nilizitumia nikapona. Baada ya wiki mbili nikaanza kuumwa tena. Ninachoomba ni msaada wa njia nzuri ya kupata matibabu maana afya ndo kila kitu. Sina raha, nina hofu hata ninaposafiri, nifanyi kazi kwa ufanisi mzuri. Naombeni msaada wenu.
 
Dawa ya Maradhi ya Kichwa Jaribu kutumia Moja kati ya hizi Dawa zangu.

(1) Chukua Haba Sawda kisha kaanga na utie kwenye kitamba cheupe na uwe unanusa kila mara itakusaidia kwa kuumwa na kichwa.

(2) Chukuwa Mafuta Zeti Zaituni Fresh Tia Kidogo Katika Puwa Pakaa pakaa Ndani Ya Puwa Yako Kabla Ya Kulala itakusaidia kupona kichwa chako.

(3)Dawa ya Maradhi ya kichwa Fikicha (sugua) tangawizi kwa maji na weka kwenye paji la uso
(4) Kunywa maji ya uvuguvugu Kila asubuhi glasi 2 kabla ya kula kitu, na ukae kama dakika45ndio waweza kula chakula.

Kunywa tena maji ya uvuguvugu glasi moja wakati wa mchana kabla kula kitu kisha ukae kama dakika 45 kisha waweza kula

chakula cha mchana. Kunywa tena maji ya uvuguvugu glasi 1 wakati wa chakula cha usiku kabla ya kula, kisha

ukae saa 1 baada ya hiyo sa waweza kula chakula. Na wakati wa kulala kunywa tena maji ya uvuguvugu glasi moja kisha ndio ulale fanya hivyo kila siku matatizo yako ya kuumwa na kichwa yataondoka.

(5) Unga wa Pilipli mboga nyekundu unga wake unasaidia Maradhi ya kichwa ukila pamoja na maji ya Uvuguvugu.

(6) Grapes juice: Juice ya zabibu zilizoiva ndio dawa ya migrane, utumie kiwango kidogo cha juice hiyo atumia hadi atakapo ona kuwa amepata nafuu! Inshallah itamsaidia shemeji atumie kisha uje hapa unipe Feedback.

Grape Juice Juisi ya Zabibu Dawa ya Ugonjwa wa Kipanda uso Migraine. Chanzo. MziziMkavu Mtafiti wa Dawa za Mitishamba.

Mkuu.@FLASH HIDER Tumia moja kati ya dawa zangu hizo kwa muda wa siku 3 Asubuhi ,mchana na usiku usipopona tumia Dawa ingine kwa muda wa siku 3 usipo pona badilisha Dawa ingine kisha uje hapa unipe Maendeleo yako umefikia

wapi? Na pia uende hospitali kupima Mapigo ya moyo (high blood Pressure) pia inachangia wewe kuumwa na hicho kichwa ukiwa huna hiyo (High blood Pressure) na umetumia hizo dawa zangu hujapona basi utakuwa una matatizo ya

kiswahili umerogwa au una Shetani mbaya mwilini mwako itabidi uwasiliane na mimi kwa njia ya Barua ya pepe nitaweza kukusaidia nitumie barua ya pepe Email Address yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com
 
eheheee nimepima pressure ipo 107/71 ni mbaya ?


Hiyo pressure yako inakoelekea siko hivyo jitahidi kuipandisha kidogo ili isikupe shida mara kwa mara. Jaribu kunywa kahawa na chakula chako ongeza chumvi kidogo hasa wakati unapogundua kuwa imeshuka.
 
Jamani mimi nasumbuliwa na kuumwa kichwa aina ya Migraine kwa muda mrefu sana, nimeenda Muhibili nimeonana na
Daktari bigwa Kichwa wa Muhibili na kuchukuliwa vipimo vingi hawakuaini kitu chochote kile. kwa yeyote anaye juu dawa anisaidie napata masumbuko mengi sana.:help::help::help::help::help:
 
Try to avoid the factors that triggers the migraine lazima ukiwa katika hali fulani au ukifanya kitu fulani ndio unapatwa na hizo migranes like stress,alcohol n.k...Umejaribu kutumia painkillers za kawaida kama paracetamol au ibuprofen bila kupata nafuu?
Dawa za migraine
Imigran-Sumatriptan
Rizatriptan
Eletriptan
Zolmitriptan
Almotriptan
Naratriptan
 
Wakuu dawa ya kipanda uso, kichwa kinauma sana kwa mbele mwenye kujua dawa anisaidie
 
wakuu dawa ya kipanda uso ,kichwa kinauma sana kwa mbele mwenye kujua dawa anisaidie
Hujatuambia wewe ni Mwanamke au Mwanamme? una umri wa miaka mingapi? umeolewa au umeowa? umeshatumia dawa za hospitali? Au bado? Matatizo yako ya kuumwa na kichwa yana muda gani? Unapata choo kirahisi? unapata usingiz kwa siku unalal masaa mangapi?
 
DALILI ZA KIPANDA USO


Kipanda uso (Migraine) ni ugonjwa au maumivu makali ya kichwa anayokuwa nayo mtu baada ya mshipa wa damu (Enlargement of Artery ) kutanuka katika kichwa chake.

Baada ya kutanuka kwa mishipa hii ya damu, pia kuna kemikali ndani ya mwili zinazozalishwa na kuizunguka mishipa hii na kupelekea mtu apate maumivu makali ya kichwa na kutanuka zaidi kwa mishipa.


Maumivu makali ya kichwa hupelekea mfumo wa utendaji kazi wa mwili pia ubadilike, mtu atapatwa na kichefuchefu, kutapika, kuharisha, katika utumbo chakula hakitanyonywa vizuri kiingie mwilini, mtu atashindwa kuona vizuri maeneo yenye mwanga na kutopenda kukaa mazingira yenye sauti au kelele.

Vipo vitu mbalimbali vinavyoweza kuchangia mtu apate tatizo la kipanda uso, vitu hivi haimaanishi kuwa ni lazima kusababishe upate na hata kama haupo katika mazingira ya vitu hivi haimaanishi kuwa huwezi kupata tatizo la kipanda uso, miongoni mwa vitu hivyo ni kama vile: sauti kali au kelele, harufu kali, aleji, mwanga mkali, kuvuta sigara, matatizo ya kukosa usingizi, kukaa bila kula kwa muda mrefu, pombe, kubadilika badilika kwa siku za mwanamke (menstrual cycle fluctuations).

Inawezekana ukawa na tatizo hili la kipanda uso, miongoni mwa vitu vinavyowasaidia watu wenye kipanda uso ni kutumia dawa mbalimbali ukijumuisha dawa za maumivu zenye mchanganyiko na caffeine, pia utumiaji wa chai au kahawa umesaidia baadhi ya watu kuwapa nafuu ya maumivu makali ya kichwa.

Tunaweza kupunguza hatari (risk) ya kupata kipanda uso kwa kubadilisha staili ya maisha yetu ya kila siku, kuepuka vitu vyenye harufu kali, kuepuka utumiaji wa tumbaku (sigara), kupata muda wa kutosha kuupumzisha mwili (kulala), kufanya mazoezi, kutokaa bila kula kwa muda mrefu, kunywa maji ya kutosha.Je, unalo tatizo la kipanda uso (Migraine), dalili zako ni zipi na ni vitu gani ukitumia unapata nafuu?
 
Kwa wenye kuumwa na kichwa kila mara pendeleeni kula Lozi (Almond) punje 12 maumivu ya kichwa yatondoka haraka

iwezekanavyo fanyeji hivyo mutaona matokeo yake kazi kwenu. kula Lozi punje 12 ni Sawasawa na kula Dawa ya Asprin vidonge 2.

Badala ya kunywa dawa ya kutuliza kichwa dawa ya Asprin wewe unatumia hiyo Lozi punje 12 kila siku Asubuhi,mchana na usiku kutwa mara 3 inasaidia sana pia kuongeza nguvu za kiume.
 
Inawezekana ndio maana Siumwi kichwa simu hizi? Nakula mbegu nyingi wakati WA staftahi. Thanks to you, nikichanganya na mtindi AMA matunda napata chakula murua.

farkhina, mbona wanasema an asprin a day keeps the heart attack away?
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana ndio maana Siumwi kichwa simu hizi? Nakula mbegu nyingi wakati WA staftahi. Thanks to you, nikichanganya na mtindi AMA matunda napata chakula murua.

farkhina, mbona wanasema an asprin a day keeps the heart attack away?

Sijui mwenzangu ila mie kuna pain killers zina aspirin nimekatazwa kula nlikua natumia sana kwa kichwa ikabidi nibadili.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom