Kipandauso (migraine): Chanzo, Dalili, Tiba na jinsi ya kujikinga na tatizo hili

hata dada yng ana miaka 10 anaumwa kichwa mpaka analia machozi!! tumemaliza hispital zote mpaka muhimbili hana tatizo lililoonekana.

Kwa wote wenye kuumwa kichwa kila siku tena kwa mda mrefu wanipm, samahani kuomba pm kwasababu suala la ugonjwa ni la mtu binafsi. Anyway binafsi nilikuwa muhanga wa hilo tatizo nimeumwa kichwa zaidi ya miaka 12, sasa nina nafuu kubwa baada ya kupata matibabu sahihi japo ni ghali kidogo. Madr. wetu sio wataalamu wa masuala ya neurological disorder, wengi wana guess tatizo matokeo yake unapewa dawa ambazo siyo sahihi kwa tatizo la kichwa.
Otherwise mcheki MziziMkavu ye huwa anajua sana natural remedial.
 
Last edited by a moderator:
Hebu jaribu kufanya vipimo vya u.t.i. Kuna mtu namjua alikuwa anasumbuliwa na kichwa Muda mrefu sana. Hivi karibuni ndio imekuja gundulika kuwa ni u.t.i.
 
msaada wadau nikienda hosptl.napima cna shida yoyote ila kichwa kinauma sn na maji nakunywa sn pia


AINA KUMI NA MBILI ZA KUUMWA NA KICHWA

Kuumwa na kichwa kumegawanyika sehemu kuu nyingi sana japo kuwa 1% yake ni hashirio la matatizo ya kiafya ambayo yameadvance. Kama vile concussion of brain,meningitis,encephaliti, na stroke. Kuumwa na kichwa pia inawezatokana na matatizo ya taya, meno au hata kula vitu vya baridi zaidi. Vyakula vyenye nitrite au monosodium glutamate.

Sehemu ambazo huuma ni kama ifuatavyo.mfumo wa fahamu ambao upo kwenye fuvu la kichwa.
Baadhi ya neva za fahamu zizlizoko usoni
Misuli ya kichwani

Mishipa inayopatikana kwenye fuvu la kichwana chini ya ubongo kuna mifumo ya fahamu yenye hisia. Kumbuka fuvu na tishuu za ubongo kwa zenyewe haziumi kwani hazna mifumo ya fahamu ambayo inahisia.
Mambo haya 12 nayo yanahusika sana.

1:Nervous tension headaches;
Ni maumivu ya kichwa endelevu upande mmoja au pande zote za misuli ya shingo na upande wa juu wa mgongo,kuumwa na kichwa pamoja na kusinzia. Tumia vitamin b2 na c , ounguza au acha matumizi ya sukari,kahawa,chakula chenye kukusababishia mzio,misongo ya mawazo na ufanye mazoezi yakutosha.

2: Cluster headaches;
Kichwa kuuma haswa upande mmoja wa kichwa kwa maumivu makali, machozi humtoka mtu na makamasi kwa mbali. Kitu cha kwanza ni kutumia chakula chenye protein ya kutosha, epukana na chakula chenye mzio kwako.

3: Hangover headaches;
Hii ni hali ya kichwa kuuma kwa sababu ya matumizi makubwa ya vinywaji vikali haswa pombe. Weka barafu chini ya kichwa yaani maeneo ya kichogoni au shingoni,kunywa maji mengi na juice ya matunda freshi na uache pombe.

4: Exertion headaches;
Hutokea pale ambapo mwili utatumika sana na haswa kwenye ngono. Weka barafu linalouma, kula mlo kamili na usifanye mazoezi.

5: Caffein headaches;
Hali hii hutokea pale ambapo umeacha matumizi makubwa sana ya kahawa kwa ghafla. Kunywa kiasi kidogo cha kahawa kuondoa maumivu na upunguze matumizi kidogokodogo mpaka utakapo acha kabisa.

6: Sinus headaches;
Maumivu haya huanzia upande wa kulia na kushoto wa pua na kupanda mpaka kichwani. Kula vitamini C kwa wingi na umuone mtaalamu wa afya maana saa zingine hii utkana na maambukizi.

7: Bilious headaches;
Kichwa na macho huuma haswa kipanda uso na husababishwa na kula sana, kula vibaya, kutofanya mazoezi na kukosa choo. Fanya mazoezi na kunywa maji yakutosha na kasha fanya enema.

8: Hunger headaches;
Maumivu ya kichwa ambaya husababishwa na kutokula kwa muda. Kula chochote ilimradi kiwe ni protein au carbohydrates .

9: Eyes ram headaches
Haya ni maumivu yanayotokea kwenye macho na wengi hudhani labda wameangalia vibaya japo saa zingine inaweza kuwa sababu. lakini chanzo chake haswa ni ubongo kufanya kazi kupita kiasi. Badili mtindo wa maisha na kama ni mtumiaji wa miwani ni vyema ukamuana mtaalamu aangalie kama lensi zimepotea nuru au la.

10: Menstrual headaches;
Hali hii hutokea kwa kina mama kipindi cha yai kupevuka. Hutokana na mabadiliko ya hormone, muone mtaalamu wa afya.

11: Arthritis headaches;
Haya ni maumivu ya kichwa yanayosikika mpaka shingoni na saa zingine mpaka mgongoni ambayo husababisha maumivu haswa unapozidisha mwendo au shughuli. Kitu kikubwa ni kutibu ugonjwa unaosababisha hali hiyo.

12: Hypertension headaches;
Ni maumivu ya kichwa chote, mwendo mkubwa pia huongeza maumivu. Hali hii husababishwa na shinikizo la damu. Tibu au pambana kushusha shinikizo la damu na halii itaisha bila shaka.

Ushauri wangu nenda hospitali kapime damu unayo damu ya kutosha? Nenda kapime macho? Je unapata Usingizi wa kutosha? Je unatapa choo laini kwa wiki unakwenda haja kubw amara ngapi? Je uanyo mawazo au Stress? Kapime Mapigo ya Moyo wako (High blood Pressure ) Yanakwenda sawa? Kisha uje hapa unipe majibu yako.@
DANIEL MWITA

Dawa ya Maradhi ya Kichwa Fanya hivi: Fikicha (Sugua) Tangawizi kwa maji na weka kwenye paji la uso. pia hii ni dawa kwa maumivu ya jino na maumivu ya sikio kwa maumivu ya sikio dondoshea tone moja kwenye sikio.


Ukiwa na Swali au Tatizo lolote linalokukera usikose kunitafuta kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano

kipanda uso.jpg
 
Itakuwa labda unamatatizo ya macho

Kwa wote wenye kuumwa kichwa kila siku tena kwa mda mrefu wanipm, samahani kuomba pm kwasababu suala la ugonjwa ni la mtu binafsi. Anyway binafsi nilikuwa muhanga wa hilo tatizo nimeumwa kichwa zaidi ya miaka 12, sasa nina nafuu kubwa baada ya kupata matibabu sahihi japo ni ghali kidogo. Madr. wetu sio wataalamu wa masuala ya neurological disorder, wengi wana guess tatizo matokeo yake unapewa dawa ambazo siyo sahihi kwa tatizo la kichwa.
Otherwise mcheki MziziMkavu ye huwa anajua sana natural remedial.

hello dogo tundu hata mimi mke wangu anasumbuliwa na ilo tatizo nisaidie namba yako ya simu tuweze kuasiliana
 
Last edited by a moderator:
Kapime macho haraka mimi kinauma tangu utotoni nikajajua nahitaj miwani nilivyopata miwani hewaaaa pole mkuu
 
Nenda kwa waganga wa kienyeji. Nakushauri kutokana na experience.

NB: Wasiokuwa na imani hiyo mtanisamehe.

Mkuu tena hao wanaojifanya hawaamini hizo mambo ndio walozi wakubwa.....jamaa inabidi awahi kwa babu mapema sana...
 
Nasumbuliwa sana tatizo la kipandauso, yaani kana kwamba paji la uso linadondoka! Hosp naambiwa ni mchafuko wa damu. Nimetumia dawa za kichwa lakini hupata nafuu tu baadae kinarudi!

MSAADA JAMANI
 
Tafuta mti mmoja unaitwa ng'hatya unapatikana sana kule usukumani. Ukipata unga wa mizizi yake unasaidia sana kwa hilo tatizo lako.
 
nasumbuliwa sana tatizo la kipandauso,yaani kana kwamba paji la uso linadondoka! hosp naambiwa ni mchafuko wa damu..nimetumia dawa za kichwa lakini hupata nafuu tu baadae kinarudi! MSAADA JAMANI
NI KITU GANI KINACHOSABABISHA UUMWE KIPANDA USO?








DALILI ZA KIPANDA USO



Kipanda uso (Migraine) ni ugonjwa au maumivu makali ya kichwa anayokuwa nayo mtu baada ya mshipa wa damu (Enlargement of Artery ) kutanuka katika kichwa chake. Baada ya kutanuka kwa mishipa hii ya damu, pia kuna kemikali ndani ya mwili zinazozalishwa na kuizunguka


mishipa hii na kupelekea mtu apate maumivu makali ya kichwa na kutanuka zaidi kwa mishipa.Maumivu makali ya kichwa hupelekea mfumo wa utendaji kazi wa mwili pia ubadilike,


mtu atapatwa na kichefuchefu, kutapika, kuharisha, katika utumbo chakula hakitanyonywa vizuri kiingie mwilini, mtu atashindwa kuona vizuri maeneo yenye mwanga na kutopenda kukaa mazingira yenye sauti au kelele.Vipo vitu mbalimbali vinavyoweza kuchangia mtu apate tatizo


la kipanda uso, vitu hivi haimaanishi kuwa ni lazima vikusababishe upate na hata kama haupo katika mazingira ya vitu hivi haimaanishi kuwa huwezi kupata tatizo la kipanda uso, miongoni


mwa vitu hivyo ni kama vile: sauti kali au kelele, harufu kali, aleji, mwanga mkali, kuvuta sigara, matatizo ya kukosa usingizi, kukaa bila kula kwa muda mrefu, pombe, kubadilika badilika kwa siku za mwanamke (menstrual cycle fluctuations).Inawezekana ukawa na tatizo


hili la kipanda uso, miongoni mwa vitu vinavyowasaidia watu wenye kipanda uso ni kutumia dawa mbalimbali ukijumuisha dawa za maumivu zenye mchanganyiko na caffeine, pia utumiaji wa chai au kahawa umesaidia baadhi ya watu kuwapa nafuu ya maumivu makali ya


kichwa.Tunaweza kupunguza hatari (risk) ya kupata kipanda uso kwa kubadilisha staili ya maisha yetu ya kila siku, kuepuka vitu vyenye harufu kali, kuepuka utumiaji wa tumbaku


(sigara), kupata muda wa kutosha kuupumzisha mwili (kulala), kufanya mazoezi, kutokaa bila kula kwa muda mrefu, kunywa maji ya kutosha.Je, unalo tatizo la kipanda uso (Migraine),


dalili zako ni zipi na ni vitu gani ukitumia unapata nafuu ?.




JITIBU KIPANDAUSO:

(maumivu ya kichwa katika paji upande) chukua manemane gram 5


Bakalhadi gram 5 na Shubiri ya dukani Vidonge hata viwili ponda laini loweka na ujipake kichwani hadi sehemu ya paji

angalia isiingie machoni. Fanya 2x1 siku3 ni vizuri uwe na nywele zisizo kubwa. Ukipona ulete Feedback zako. Ukiwa na Swali au Tatizo lolote unaweza kuwasiliana na mimi kwa kubonyeza hapa.
Mawasiliano
 
Punguza stress...badilisha diet yako, nikimaanisha angalia kama unapata viturubisho muhimu kwenye chakula
 
nasumbuliwa sana tatizo la kipandauso,yaani kana kwamba paji la uso linadondoka! hosp naambiwa ni mchafuko wa damu..nimetumia dawa za kichwa lakini hupata nafuu tu baadae kinarudi! MSAADA JAMANI
Nilikuwa na tatizo hilo nilihangaika sana kuna daktari mmoja aliniambia kukosa kufanya sex muda mrefu au kufanya kwenye chumba below 20degC ndiyo sababu. Tiba ni kufanya kwenye 28 - 30degC mara 2 au 3 itapona forever. This isnt a Joke hata mimi sijui sababu but it worked out
 
Kutuliza maumivu,tumia antimigraines kama ergotamine(vasograine kwa mfano) au sumatriptan
 
Kuumwa kichwa kuzunguka paji la uso hadi kwenye macho ni tatizo gani! Wenye kujua tafadhali
 
Back
Top Bottom