Kiraka
JF-Expert Member
- Feb 1, 2010
- 3,837
- 3,079
Ndugu yangu Mangaline, kama umeona post nyingi za juu hapo wapumbavu wakubwa wamefurahia huyu jamaa kunyimwa alichokuwa anadai.Hapa ndipo tunapotofautiana. Kazi nyingine tunaambiwa tutangulize utaifa mbele, wakati wengine wanatakiwa watangulize maslahi mbele. Juzi wabunge wamapewa 1Milioni kila mmoja kwa ajili ya kuhamasisha sensa, wakati ambapo wabunge haohao hadi sasa tangu wamalize kikao cha bunge, wamebana huko mijini, na huku majimboni hawajafika. Hiyo milioni waliyopewa haijafanyiwa kazi, na wala haitarejeshwa. wakati huohuo, karani analazimishwa aende kituoni bila kulipwa, eti atangulize utaifa, akale nini huko????, akalale wapi????, akafanye nini????. Hivi utaifa ni kutesana????
Tunaambiwa eti Ualimu ni kazi ya wito, Udaktari ni kazi ya wito, je! ubunge si kazi ya wito??????? Tuache siasa, tufanye kazi.
Huyo alijitolea kuongoza wenzie kudai haki amekatwa jina, na wengine wamelipwa kupitia mgongo wake wapumbavu wengine wanalifurahia hilo, ndio uone ni aina gani ya mijitu mijinga imejaa huku uraiani, yaani hatuwezi kutoka kwa kuwa na wapuuzi kama hawa wasioelewa nini maana ya kudai stahiki zao!