Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana...

Mgomo ulikwaza wengi, kuna ndugu walifiwa na ndugu zao kwa ajili ya siasa za wachache hivyo perpetrators wanaweza kuwa wengi...
 
sidhani kama kikwete atamaliza mda wake, inabidi apewe ulinzi mkali mana anaweza kujinyonga!
MTU ukiwa ukawa au chadema bwana , uki refer baadhi ya comment zako waweza kuhisi aibu, sasa mbona kamaliza mda wake
 
mmeona faida ya kumteka? mgomo uliisha na maisha yanasonga yeye hatujui yuko na msaidizi wake Dr Mashinji ni Katibu mkuu wa Chadema. leo hii mtafute mwambie aanzishe mgomo atakupiga ngumi 8 za pua fasta fasta
 
Sasa uchokozi umefikia pabaya na hii sasa ni vita!!

Taarifa iliyonifikia hivi punde ni kuwa jemedari Dr. Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye face to face kwa ajili ya reconciliation.

Taarifa zimekwisha fikishwa polisi na sehemu zingine kwa ajili ya ufuatiliaji. (source chanzo cha kuaminika).

UPDATE:
Inaelekea waliomteka si watu wema kabisa, Dr. Ulimboka kaokotwa sehemu akiwa katika hali mbaya sana!



Tutaendelea kutoa updates kadiri muda unavyoruhusu.

attachment.php
attachment.php
attachment.php


attachment.php

PICHANI: Dkt. Ulimboka akiwa katika hali mbaya mara baada ya kuokotwa akiwa hajitambui.
Ulimboka alitekwa jana usiku mida ya saa 6 usiku baada ya kupigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Abeid na alitekwa na watu wawili waliokuwa na silaha. Kufuatia hali hii wafanyakazi wa chumba cha maiti Muhimbili nao wamegoma na mgomo huenda ukawa mkubwa zaidi!

IMG_20180909_205834_938.jpg
IMG_20180909_205828_887.jpg
IMG_20180909_205822_878.jpg
 
Aisee yupo zake ulaya anakula bata now
Utakula bata na meno ya bandia? Matendo mengine aliyofanyiwa je, kweli yatamtoka kichwani kwa kukaa ulaya?
Kuna utabili ulitolewa miaka hiyo kwamba serikali inaanzisha mchezo huu baadaye hata watu binafsi wataiga na kufanya utekaji na mauaji kama mtindo wa maisha. Tuko wapi leo hii? Waanzilishi ni utawala wa awamu ya nne. Hamukufokewa lakini tumeachiwa uchafu wa maisha yote.
 
Kama habari hii ni ya kweli, Suluhisho la ukweli halitokani na kuteka watu, ni kwa kuwapa madaktari haki yao.

Serikali badala ya kuteka mafisadi inateka wanaodai maslahi yao. Aibu!. Baadhi ya madai ya madaktari ni ya Msingi, wanataka huduma ziboreshwe hospitalini, wanataka wasiwaandikie watu aspirini wakati wanahitaji dawa ya malaria isiyokuwepo.

Haya ni madai ya haki, hayatatatuliwa kwa kuteka watu.
Kuna watu wamepotea kitambo humu JF . Huyu jamaa katokomea wapi?
 
Back
Top Bottom