Kiongozi UVCCM ataka mafisadi wafilisiwe

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Martha Fataely, Moshi

SERIKALI imeombwa kwenda mbali zaidi katika vita dhidi ya ufisadi kwa kuhakikisha inawadhiti, kuwafilisi na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wanaotajwa kwani ni sawa na wahujumu uchumi.

Mjumbe wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Paul Makonda aliyasema hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani hapa ambapo pia alitaka utajiri wa wanachama wa CCM wahojiwe jinsi ambavyo wamepata mali hizo.

Madai ya Bw. Makonda yamekuja siku chache baada ya viongozi wa CCM kutoa taarifa zinazotatanisha, baadhi wakidai kuwa kwenye vikao vyake watu watatu walitajwa kuhusishwa na ufisadi na kupewa siku 90 kupima wenyewe na kuachia nyadhifa zao, huku wengine wakisema hayakutajwa majina wala orodha ya watuhumiwa hao

Bw. Makonda katika taarifa yake aliomba serikali iwahoji aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, aliyekuwa Mwasheria Mkuu wa Serikali, Bw Andrew Chenge na Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Azaz ili kujua wamepata wapi utajiri walionao.

Bw. Makonda alisema watuhumiwa wote waliotajwa katika tuhuma mbalimbali za ufisadi ndani ya nchi,wafilisiwe ili kuhakikisha rasilimali walizopora watanzania zinarejshwa.

Alisema pamoja na Kamati Kuu ya CCM kutoa muda wa siku 90 kwa watuhumiwa wenyewe kujivua nyadhfa zao lakini, ni vyema kwa serikali ikawafilisi ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ovu ya kujilimbikizia mali.

"Hawa wote wamechafuka na wananchi wanawatuhumu wanapaswa kufukuzwa CCM ikiwa ni pamoja na hatua nyingine za kisheria kuchukuliwa dhidi yao kwani wao ni majeruhi," alisema.

Alisema wapo baadhi ya vigogo ambao wana utajiri wa kutisha hapa nchini wakati waliwahi kushika nyazifa mbalimbali hapa nchini lakini pia wamekuwa wakihusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi.

"Tunaomba watu hawa wafilisiwe, utajiri wao uhojiwe kwani wameweza kuliingiza taifa katika mikataba feki mbalimbali wakati wakiwa na nyazifa za uongozi serikalini," alisema.

Aidha Bw. Makonda ameendelea kutoa madai mazito kwa viongozi wa UVCCM, Mwenyekiti Beno Malisa, James Millya, Hussen Bashe na Martine Shighela, ambao alidai ni vibaraka wa watuhumiwa hao.

Bw. Makonda aliongeza kuwa iwapo Bw. Lowassa aliwahi kujiuzulu katika kashfa ya Richmond, mapema wakati bunge likiendelea na mjadala, basi anatakiwa kufanya vivyo hivyo katika hatua hii, pamoja na watuhumiwa wengine wote.

Kwa upande wake, Makamu mwenyekiti wa UVCCM, Bw. Beno Malisa, alipohojiwa alisema masuala ambayo yanaigusa taasisi yatajibiwa na taasisi husika na mengine anayozungumzia vijana Bw Makonda atajibiwa na vijana wa saizi yake.

"Ah sasa tusipoteze muda, huyo kama amezungumza hivyo,subiri atajibiwa na taasisi anazozitaja….mengine pia atajibiwa na vijana wa saizi yake, we chukua hilo ndiyo jibu sasa, au unataka jibu unalotaka wewe?" alihoji.
 
Back
Top Bottom