Kiongozi Msafi wa Africa na Aseme - Mugabe

..Dr.Migiro amezungumza kwa niaba ya Ban Ki Moon na amesisitiza suala hili litatuliwe KIDIPLOMASIA.

..Kikwete inabidi awe careful na Mugabe. tena naona amefanya vizuri kuongea kiswahili. Hakuna anayeweza kusimama "pound-for-pound" na huyu Mzee.

Mugabe ana mdomo sijawahi kuona!! Uzuri wake ni kwamba yeye haogopi mtu na kama ikibidi atakupasha tu yale yaliyopo moyoni mwake. Kwa hilo nampa kudos lakini mengine ni sifuri kabisa.
 
Mugabe ana mdomo sijawahi kuona!! Uzuri wake ni kwamba yeye haogopi mtu na kama ikibidi atakupasha tu yale yaliyopo moyoni mwake. Kwa hilo nampa kudos lakini mengine ni sifuri kabisa.

Na anajua hasa kujieleza. He is a very good orator. But then all dictators were good orators, including Hitler, Idd Amin, etc; you mention any dictator you know one of his strength will be communicatability!
 
Na anajua hasa kujieleza. He is a very good orator. But then all dictators were good orators, including Hitler, Idd Amin, etc; you mention any dictator you know one of his strength will be communicatability!

You are absolutely right my friend!!!!
 
Summit ends without Mugabe condemnation

2008-07-01 10:57:06
By SHARM EL-SHEIK, Egypt

Zimbabwe`s President Robert Mugabe was welcomed by his peers yesterday, strolling into an African Union summit where leaders were unlikely to criticize him despite Western calls for them to condemn his widely discredited re-election.

The United States has vowed to bring the issue of Zimbabwe before the U.N. Security Council this week, and British Prime Minister Gordon Brown urged the AU to reject the result of Zimbabwe`s presidential runoff.

Mugabe was the sole candidate in Friday`s vote. Opposition leader Morgan Tsvangirai withdrew, saying his supporters had become targets of brutal state-sponsored violence.

The summit should ``make it absolutely clear that there has got to be change`` in Zimbabwe, Brown said in London.

``I think the message that is coming from the whole world is that the so-called elections will not be recognized.``

But instead of condemnations, the AU`s leaders were expected to gently urge Mugabe to engage in some sort of power-sharing agreement with the country`s opposition, along the lines of a deal that ended violence in Kenya earlier this year.

Africa should ``do everything in its power to help the Zimbabwe parties to work together in the supreme interests in their country so as to overcome its current challenges,`` African Union Commission chairman Jean Ping told delegates.

In his opening address to the gathering in this Egyptian Red Sea resort, the African Union�s head, Tanzanian President Jakaya Kikwete, congratulated the Zimbabwean people and AU mediators but not Mugabe himself. He called the elections ``historic`` but also said there were challenges.

A draft resolution written by AU foreign ministers and due to be approved by leaders at the summit does not criticize the runoff election or Mugabe.

The draft, a copy of which was obtained by The Associated Press, condemned violence in general terms and called for dialogue.

The summit is an opportunity for Mugabe to gain some symbolic international recognition a day after he was sworn in as president for a sixth term following Friday`s voting.

Tsvangirai on Monday said Mugabe should have no place at the summit and the AU now had a responsibility to deal with the crisis.

``Robert Mugabe is not the legitimate leader of Zimbabwe,`` Tsvangirai told The Associated Press. �He is usurping the power of the people. He has brutalized his own people.``

The African Union`s own observers said yesterday that the runoff fell short of the continental body`s standards, citing violence and noting that the opposition was denied equal access to the media during the campaign.

U.N. deputy secretary-general, Asha-Rose Migiro, called the situation an ``extremely grave crisis.``

Most African governments - including regional powerhouse South Africa - have been reluctant to criticize Mugabe, whether because of long-standing ties to the Zimbabwean leader or because they do not want to be seen as backing the West against a fellow African.

Mugabe has threatened to point fingers at African leaders if they speak out against him.

Zimbabwe`s government mouthpiece, The Herald, reported Monday that Mugabe ``was prepared to face any of his AU counterparts disparaging Zimbabwe`s electoral conduct because some of their countries had worse`` elections records.

Zimbabwe is far from Africa`s only experience with flawed elections. For example, the summit`s host nation, U.S. ally Egypt, is often criticized by international rights groups for jailing dissidents to Hosni Mubarak`s nearly 27-year rule, and recent elections saw violence as police barred opposition supporters from the polls.

Electoral officials said Sunday that Mugabe won 85 percent of the vote in Friday�s runoff, which observers said was marred by violence and intimidation.

Just hours after he was declared the winner, Mugabe, who has been Zimbabwe�s leader since independence in 1980, sounded a conciliatory note.

``Sooner or later, as diverse political parties, we shall start serious talks,`` he said in a speech following his swearing-in Sunday. He also had promised talks on the eve of the vote.

Many world leaders have condemned Friday`s runoff. On Monday, French Foreign Minister Bernard Kouchner said France ``decided that this government is illegitimate`` and called the re-election of Mugabe a ``farce, a criminal electoral comedy.``

He expressed hopes African leaders would be firm with Mugabe at the summit. But he also acknowledged that ``for many Africans, Mugabe was long a great liberator`` as an anti-colonial hero, which complicates matters.``

Zambia`s President Levy Mwanawasa, who has been a critic of Zimbabwe`s political crisis, was not in attendance at the summit. He was rushed to a local hospital Sunday after falling ill while meeting with African leaders here, said Egypt`s official news agency, MENA.

According to the government-owned Zambia Daily Mail, Foreign Affairs Minister Kabinga Pande said that Mwanawasa was admitted to Sharm-el-Sheikh International Hospital for high blood pressure.
Mwanawasa suffered a stroke in 2006. (Agencies).

SOURCE: Guardian
 
I personal get sick the way waafrika tunakubali brainstorming za western media when it comes to politics za Zimbabwe, hizo stereotyping sidhani kama factor ya mimi binafi kuamini kuwa STILL MUGABE HE IS RIGHT!!, no matter what we will say upon him and what is happening in Zimbabwe so far!!

Hivi when it comes to kunauchaguzi BOMU in Africa uliotokea hivi karibuni kama wa Nigeria?, kama wa Kenya?, hivi kuna violater mkubwa wa Human Rights Duniani kama Zenawi?, Mu7?, what are talking jamani?, juzi naangalia CNN nakutana na picha ya political casuality wa vurugu, hiyo clip since December wanairudia tena na tena!, waulize Wakenya ODM esp. what the policemen did for them!!

This is Africa jamani!!, the definition of ''democracy'' in Africa is not the same as in America, as in Europe, As in Pakistan, as in Afghanstan, as in Palestina......etc etc..

Kitu ambacho i was thinking personally, ni kwa SADC kupitia Mbeki wajaribu kumshawishi(last time), kuwa for the sake of the country as a whole Mugabe should step down, na amsimamishe candidate mwingine.....'coz for me is the war btn the WEST and Mugabe na not ZAFU-PF per se!

Stand up!! viva Mugabe&Obama hata yakiwashinda mmeonesha sisi sio vilaza kihivo bwana!!

.....vipi Wazimbabwe zaidi ya million ambao wame end up kuwa wakimbizi kwa sababu ya siasa za Mugabe? hao nao ni "WEST"? na unachotaka afanye hopeless Mbeki ndicho hicho hicho hao so called west wanafanya ila kwako ni unafiki kwa sababu ni wazungu
 
Mwacheni mzee wa watu afanye kazi zake kwa amani. Bado anaonyesha ujasiri wa kweli, hana unafiki kama akina kikwete vibaraka wakubwa wa us na uk. Tunawataka Bush na Brown wamkome babu yetu kipenzi cha waafirika halisi.

Tunamuomba mwenyezi Mungu amjalie afya njema babu yetu ili awape fundisho akina kikwete!

niko pamoja na wewe mkuu, maana watu wengi wamekuwa washabiki tu bila kujua hali halisi, hawa akina tsangirai wenyewe ndiyo wanafiki wakubwa maana walikubaliana wote wawafukuze wazungu halafu leo huyu kibaraka anageuka, sasa kama kuna njaa walitaka mugabe aingie shambani akawalimie chakula? wazimbabwe waache uvivu, mashamba wameshapewa sasa walime, mungu akujalie afya mugabe
 
Huu ujumbe wa Mugabe una maana kubwa sana kwa Afrika na viongozi wa Afrika kwani hili ni tusi kwao kuwa hakuna aliyemsafi?

Huu ni ujumbe mzito sana kwa mustakabali wa demokrasia ya Afrika kama aliwaambia na hakuna hata mmoja aliyejitokeza na kusema kuwa yeye ni msafi basi Afrika ipo kwenye leadership crisis kama sio kukosa uongozi kabisa.
 
Mgabe utauwa watu na kuwanyanganya haki yao lakini that which goes round will definetely come round, zamu yako itafika kwa sababu injustice anywhere is a threat to justice every where. Kwa mda huu Mugabe anakuwa na kiburi na mbwebwe eti aliyemsafi asimame na kumyooshea kidole wanasema kuwa even a fool has his own day!!
 
.....vipi Wazimbabwe zaidi ya million ambao wame end up kuwa wakimbizi kwa sababu ya siasa za Mugabe? hao nao ni "WEST"? na unachotaka afanye hopeless Mbeki ndicho hicho hicho hao so called west wanafanya ila kwako ni unafiki kwa sababu ni wazungu

Mkuu nilichokuwa najaribu kusema ni vile western media zinavolichukulia soo la Zimbabwe na Mugabe personal (incl sisi waafrika) as s'thing which is ''extraordinary na worst across the region". hicho ndicho ninacho pinga!!

What is happenning in Zimbabwe na sababu kuu ya yooooote hayo, pengine hata ingekuwa hapa kwetu huenda hata wewe usingekubali, tatizo ni kwamba mimi na wewe tunaangalia zaidi outcomes bila kujua kiini cha tatizo hilo, they are other Zimbabweans wana-take oportunity hio kuweza ku-fled the country kwa kisingizia hicho..

All in all still for me Mugabe ni shujaa wa kweli!!
Heri chai ya mluzi kwako kuliko pilau la masimango kwa jirani..!!
 
Kikwete hana ujasiri wa kumkabili Mugabe


Lula wa Ndali-Mwananzela Julai 2, 2008

JE, mtu akipanda mpunga atarajie kuvuna mbaazi badala yake? Je, mtu akipanda viazi atarajie kuvuna mahindi?

Si kweli kwamba kile mtu apandacho ndicho avunacho? Sasa iweje leo tushangae yanayotokea Tanzania na Zimbabwe? Iweje tupigwe tahamaki tulipoyaona yaliyotokea Kenya, Rwanda, Burundi, na wiki chache zilizopita Afrika Kusini na sehemu nyingine za Afrika kana kwamba hatujui tulichopanda ni nini?

Si jambo la wazi kuwa walichopanda Ujerumani ndicho walichovuna chini ya Adolf Hitler, na kile kilichopandwa Serbia ndicho kilichovunwa chini ya Slobodan Milosevic?

Mojawapo ya kanuni za chanzo na matokeo inasema kwamba kila matokeo yana chanzo chake. Kwamba hakuna kitu kinachotokea ambacho hakina chanzo. Hivyo, mara nyingi tunapoona jambo limetokea badala ya kujikuta tunashangaa “imekuwaje” tunapaswa kujiuliza kwanza “kimetokana na nini”. Ni katika kujua chanzo cha kitu ndipo hapo basi tunaweza kuanza kutafuta suluhisho lake.

Ni wazi kuna wakati ambao tunatakiwa kushughulikia tatizo kwanza ndipo tuweze kujua chanzo chake ni nini ili kuhakikisha tatizo hilo halirudii tena. Tunapoona bomba linavuja kitu cha kwanza tunachojaribu kufanya ni kuziba ufa au upenyo huo ili tuweze kufanya upembuzi wa kujua ni hatua gani inafaa kuchukuliwa ili kuhakikisha tunakomesha kabisa kuvuja kwa maji.

Endapo tunagundua kuwa tatizo ni sehemu ya bomba iliyochakaa basi suluhisho ni kuleta bomba jipya.

Ni kutokana na mawazo haya leo najikuta nalazimika kuzungumzia hali ya uongozi katika Afrika na kujenga hoja ya kwamba uongozi tulionao katika Tanzania na sehemu nyingi za Afrika (wengine nitawaacha wazungumzie mabara yao) unatokana na kile ambacho tumekipanda katika uongozi.

Tulipopanda viongozi wabovu, tumevuna uongozi mbovu! Haiwezekani mtu aupate uongozi kwa ufisadi halafu baadaye awe kinyume cha ufisadi! Kile tulichopanda, ndicho tunachovuna.

Leo tunashuhudia uonevu mkubwa kabisa katika Afrika ambao umeendelea kumdhalilisha mtu mmoja chini ya mkono wa mtu mwingine. Yaliyotokea Zimbabwe siku chache zilizopita, yanaendelea kuthibitisha jambo moja muhimu kuwa Waafrika bado hatujafikia mahali pa kuhakikisha kile tunachopanda ndicho tunachovuna.

Kwa muda mrefu Robert Mugabe amekuwa kama mbegu nzuri iliyopandwa Zimbabwe na kwa muda watu waliona mazao mazuri yaliyotoka katika nchi ile na hivyo kutoangalia sana mbegu yenyewe iliyopandwa ni mbegu gani.

Baada ya maamuzi ya Robert Mugabe kunyang’anya mashamba ya Wazungu na hatimaye kuingiza siasa kwenye maamuzi ya kiuchumi, Zimbabwe imejikuta ikiwa na mfumuko mkubwa wa bei ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia iliyoandikwa ya mataifa.

Kuvurugika kwa hali ya kisiasa Zimbabwe ambako kumeshuhudiwa na dunia nzima ndani ya miaka hii michache iliyopita hakukutiliwa maanani na jamii ya Kiafrika.

Viongozi walikaa pembeni na kuwaacha Wazungu walipigie kelele wakati tunaona Zimbabwe ikitokomea taratibu kwenye shimo la giza.

Tumeshuhudia wananchi wa Zimbabwe kwa maelfu yao wakiikimbia nchi yao. Tumeshuhudia raia wa Zimbabwe wenye asili ya Ulaya wakinyang’anya mashamba yao kwa kisingizio cha sera mpya ya kugawanya tena ardhi. Tumeshuhudia katika nchi ya Zimbabwe raia wa kweli wa Zimbabwe ni yule mwenye rangi nyeusi.

Ukimya wetu umethibitisha jambo moja kuwa tulikuwa tunakubaliana na sera hizo za kibaguzi za Zimbabwe chini ya Robert Mugabe. Mara kadhaa tumepata nafasi ya kuchukua msimamo lakini kama watu waliolishwa limbwata viongozi wetu wamekuwa waoga kusema ukweli.

MUGABE akisikiliza kwa makini kwenye kikao cha AU Misri.

Hata juzi wakati Rais Jakaya Kikwete anafungua mkutano wa AU Misri yeye kama wengine alishindwa hata kutaja jina la Mugabe! Huu woga si wa Watanzania. Huu woga wa viongozi wetu kuchukua msimamo katika medani ya kimataifa umeanza lini?

Yawezekana Mwalimu Julius Nyerere alikuwa na mapungufu yake lakini kwenye suala la msimamo hakuwa na utata. Wengi tulijua jinsi gani Mwalimu alipinga ubaguzi wa rangi au uonevu wa mtu mmoja dhidi ya mwingine.

Ni msimamo ambao Mwalimu alikuwa nao maisha yake yote. Mwalimu aliupinga ubaguzi pasipo utata na hakuwahi kuhalalisha aina yoyote ya ubaguzi kwa maneno yake au kwa ukimya wake.
Watawala wetu wamesahau.

Agosti 1972, Jenerali Idi Amin aliwatimua kutoka Uganda raia wa Uingereza wenye asili ya Asia (Wahindi) na akafuatia na amri ya kuwatimua raia wa Uganda wenye asili ya Asia pia. Na hata alipojaribu kubadilisha sera kidogo wale waliobakia walijikuta wakiishi katika mazingira ya kubaguliwa kwani si raia kamili.

Agosti 21 mwaka huo huo, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akiwa kwenye shughuli Chuo cha Ualimu Chang’ombe, aliamua kuzungumzia suala hilo lakini kwa mapana yake na kuonyesha ni kwanini Waafrika hawatakiwi kubaguana na kutendeana vibaya kwa misingi ya rangi, au nasaba zao.

Mwalimu akasema kitu kimoja ambacho ni muhimu kukifikiria kwa sekunde; “Afrika lazima ikatae kudhalilishwa, kunyonywa, na kusukumwa sukumwa. Na kwa nguvu hiyo hiyo ni lazima tukatae kuwadhalilisha, kuwanyonya na kuwasukuma sukuma wengine. Siyo kwa maneno tu bali pia kwa vitendo”.

Hili viongozi wetu wamelisahau. Viongozi wetu walikaa kimya wakati Mugabe anawadhalilisha, kuwanyonya, na kuwasukuma sukuma wananchi wake. Tulimwacha afanye hivyo kwa sababu tukiamini kuwa ni “shujaa wa Afrika”.

Mugabe akapata kichwa na kitendo cha kumkaribisha kwenye mkutano huu wa Umoja wa Afrika ni kilele cha woga wa viongozi wa bara letu. Hivi ni kweli hakuna kiongozi katika bara letu ambaye angeweza kumwambia Mugabe kwa jina lake kuwa anachokifanya na alichokifanya Zimbabwe ni uovu na ubaguzi mkubwa?

Nyerere katika maelezo yake hayo aliongezea na kuonyesha uzito wa viongozi wenye kusukuma sukuma raia wake. Alisema “Fikiria kuwa na sisi Tanzania tunaamua kuwafukuza baadhi ya raia wetu, tufanyeje?

Tuwaswage hadi mpaka na Kenya halafu Kenya wanasema ‘hapana siyo raia wetu’, na tunawapeleka Uganda, Malawi, Zambia, Burundi na Rwanda na kote wanasema hivyo hivyo. Tufanyeje sasa? Tuwaue?

Hivyo ndivyo alivyofanya Hitler miaka ile ya 1930 na 1940. Akawaweka kwenye matanuri ya moto na kuwaua Wayahudi milioni sita! Hawa walikuwa watu si sokwe.

Rais Thabo Mbeki mwoga, Rais Hosni Mubaraka mwoga, Mwai Kibaki mwoga, Kikwete mwoga! Wote waoga kwani wameshindwa kusimama mbele ya ukweli na kutetea haki ya wananchi.

Si kwenye suala la Zimbabwe tu, si tumeshuhudia maelfu ya wananchi wa Sudan wakiuawa chini ya mkono wa Janjaweed? Nani kati ya hawa viongozi wetu ameikemea serikali ya Sudan? Si wote wanaendelea kukaribishana kwenye vikao vyao vya utukufu?

Wamembeba na wamemlea Mugabe na sasa analiaibisha bara zima na tunu yetu kama Waafrika. Tumeendelea kuwa kichekesho cha dunia.

Inawezekana vipi kukaa meza moja na mtu ambaye ameiba uchaguzi mbele ya macho yenu halafu mkamkumbatia?

Viongozi wasiokuwa na msimamo wa jambo jema wa nini katika bara letu?

Mwaka 1961 wakati bado tukiwa chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa ulifanyika mkutano wa Jumuiya ya Madola. Katika mkutano huo mada ambayo ilikuwa inawagawa viongozi wa nchi hizo ilikuwa ni kama kuikubalia Afrika Kusini kuingia tena kwenye Jumuiya hiyo.

Mwalimu Nyerere akiendeleza kanuni yake ya kutobembeleza ufisadi wa ubaguzi wa rangi aliandika makala kwenye gazeti la London la “The Observer” la Machi 7.

Katika makala yake hiyo Mwalimu kwa umahiri wa lugha alionyesha ni kwanini Afrika ya Kusini iliyokuwa na sera ya ubaguzi wa rangi isingeweza kuwa mmoja wa wanachama wa Jumuiya hiyo.

Mwalimu aliandika na kusema kuwa kanuni za haki za binadamu na usawa wa wanadamu wote unalilazimisha Taifa letu kuchukua msimamo dhidi ya mwanachama ambaye ni wa zamani zaidi, mwenye fedha zaidi na ambaye ana watu wengi wenye asili ya Ulaya.

Alisema ni msimamo ambao unatokana na kanuni kuwa binadamu wote ni sawa na haiwezekani kukaa meza moja na Kaburu. Ndipo aliposema maneno yale maarufu kuwa “kupiga kura ya kuiingiza Afrika Kusini, itakuwa ni kutupigia sisi kura ya kutoka”. Hoja ya Mwalimu ilishinda na Afrika ya Kusini haikuingizwa.

Leo viongozi wetu wanagwaya mbele ya mtu asiye na nguvu zozote, utajiri au mvuto wowote duniani. Sababu pekee ya kushindwa kumkemea ni rangi yake! Kwamba kwa vile ni Mweusi mwenzetu basi tusimkemee kwani tutawapa furaha Wazungu na maadui zetu! Hiyo ni hoja ya kipuuzi.

Nelson Mandela akisimama katika kizimba ya Kaburu Aprili 20, 1964 (siku tano kabla ya Tanganyika na Zanzibar kuungana) alielezea ni kwanini yuko tayari kufa kutetea msimamo wake kuwa anapinga kuonewa na mtu Mweupe, kama vile anavyopinga kuonewa na mtu Mweusi.

Akasema kwa uthabiti kuwa “hili ni wazo ambalo nimeishi kwalo, na ikibidi niko tayari kufa kwalo”. Huo ndugu zangu ndio msimamo; msimamo ambao hauko ndani ya Kikwete, Mbeki, Kibaki au kiongozi mwingine wa Afrika. Mashujaa wa kweli hawaonekani tena katika bara letu!

Ni kwa sababu hiyo naamini Tanzania inaweza kurudia katika nafasi yake ya kihistoria, nafasi ya kusimama na kusema ukweli mbele ya wenye nguvu, nafasi ya kutetea haki ya binadamu wote.

Tumekaa kimya muda mrefu ndiyo maana kina Mugabe wameshamiri. Tumemung’unya mno maneno ndiyo maana leo hii Mugabe na makuwadi wake wanaujasiri wa kuzamia mkutano wa viongozi tena akiwathubutisha wamnyoshee kidole ili aone “ni nani kati yao ni msafi”.

Lakini tutarajie tofauti kutoka serikali ya Kikwete kuhusu suala hili? Je, tutarajie kuwa Rais Kikwete anaweza akanyoosha mkono na kumuambia “mzee Mugabe” kuwa Tanzania inamuondoa Balozi wake na hatutambui “ushindi wake” hadi pale utakapofanyika uchaguzi huru na wa haki?

Hivi kweli Rais Kikwete anaweza kusimama na kusema ubaguzi dhidi ya mtu Mweusi unaofanywa na mtu mwingine Mweusi haukubaliki.

Kweli Kikwete anaweza kusema ipo haja ya Mugabe kukaa meza moja na wapinzani wake ili waone jinsi wataiendesha serikali wakati miaka miwili na nusu sasa yeye mwenyewe ameshindwa kukaa na wapinzani wa Tanzania na ameshindwa kuwakutanisha Seif na Karume Zanzibar?

Ndugu zangu, tulichopanda ni viongozi hawa tulionao, na hawa ndio tunaowavuna! Na kama rafiki yangu mmoja alivyosema kuwa viongozi wetu ni taswira yetu sisi wenyewe. Viongozi wetu wanatoka kwetu na wao ni kama sisi.

Hivyo tutarajie tofauti kwa hawa walioko madarakani sasa? Binafsi sitarajii lolote tofauti kwani kama rafiki yangu mwingine asemavyo (japo kwa kebehi zenye dalili ya ukweli” kuwa Waafrika ndivyo tulivyo! Ama tunasingiziwa?


Makala ya mwenzetu Lulandala imenisisimua kupita kiasi.Ni wakati wa kuambiana ukweli pasipo kificho.

Hizi ni salamu za kikwete, hata kama chungu dawa inaponyesha!
 
Hivi kweli mnategemea AU inayoongozwa na Kikwete , Rais aliyeshindwa kupambana na wezi wa EPA ,awe na ujasiri wa kumkabili Mugabe ? Tuna tatizo gani katika hii forum , Kikwete ni mzuri katika kutoa short term promises halafu baada ya hapo atajiuma jiuma tuu . Hili sio kosa lake bali ni character ya watu wa pwani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom