Kiongozi mkuu wa Nchi anapotaka kutatua Migogoro Mizito kwa Propaganda....

STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,770
553
Tunakumbuka hotuba aliyoitoa Mkuu wa Kaya kwa wale makada walioifikisha nchi hii hapa ilipo... aka Wazee wa Dar jana ni kama ya nne hivi tangu Jk aingie pale magogoni. Mimi nimeshangazwa sana na mambo ya kiswahili I mean maneno ya ki uswahili aliyoyaongea mkuu mbele ya wale wanaoitwa wazee wa Dar ambao kilicho mbeleni kumalizia Pension zao na kupunzishwa.....

Kikubwa kilichonishangaza ni kitendo cha JK kukutana na viongozi wa madaktari ikulu na kuzungumza nao na hadi leo waTZ hatujaambiwa officialy Rais aliwaambia nini hawa madaktari hadi wakarudi kazini. Isitoshe madaktari wamemheshimu sana JK kwa kukubali kurudi kazini bila masharti yeyote.. Sasa haya maneno ya Taarabu JK anayatoa wapi? au kwa vile yeye na familia yake hawatibiwi bongo?

Maana haingii akilini kwenda kwa majuha kama wale wa jana eti ukazungumzie issue ya kiprofession kama udaktari.. Huyu jamaa alitakiwa kukutana na madaktari wakamweleza matatizo wanayopata nk. alafu akawaabia mawaziri wale wakawajibika.

jingine ni swala la kuwa na vifaa kwenye mahospitali, Jk anasema kila wilaya kuna X-RAY mimi naomba aende kwenye Hospitali ya Mkoa wowote akaangalie, kama yeye si Dk hawezi kujua kama haifanyi kazi mwambieni awachukue ma DK wamwonyeshe kama ni nzima au mbovu maana tumeshuhudia sana yeye na Makamu wake na waziri mkuu wakizindua miradi ya maji ambayo sika tatu au mbili kabla ziara yake huwa matenki yanajazwa maji na wakifika pale wanaambiwa mradi wa Kisima au bomba umekakilika na unafanya kazi kumbe kadanganywa.

Wanapokuja wasamaaria wema kama madaktari wanamwambia viongozi wa wizara wameagiza vifaa feki vya kupimia ukimwi kwa nini anawaona wabaya? kwa nin anafanya Mzaha na propaganda.. Si ni bora waTZ wafe kwa kuugua kulikoni kuharibiwa maisha kwa kuambiwa ana Ukimwi wakati hana au hana ukwimwi wakati anao...

Mimi nafikiri ingekuwa China hao kina Mponda na Nkya ni wa kunyongwa sasa sisi huku wanaambiwa wawapishe wengine kwa nini inakuwa noma?
 
I love my presdent. Ila nawalaumu sana washauri wake. tatizo kubwa ni mfumo. Rais akichaguliwa anatakiwa abebe begi lake la nguo aingie ikulu. hili suala la kubeba watu kwenye begi na kuingia nao ikulu ndo matatizo yake. kamwe hawawezi kukueleza ukweli. lazima wasikitike na kucheka pamoja na wewe. siku urais utakapogeuka kuwa taasisi haya yote yatakwisha.

My wish ni siku moja tusiwe na rais wa wapiga makofi. demokrasia imeprove wrong, inawezekana wabongo 1000000 pasipo kufaham au kwa kulinda chama asili wakachagua wrong choice huku mtu mmoja mwenye uelewa akapoteza kura yake moja. tufanye sampling ili tupige kura zenye picha halisi? halitawezekana pia. tunafanyaje sasa?

Lazima vyama vitupe candidates wenye sifa. mfumo wa kifalme ufe. kila mtu awe na sifa ya kuchaguliwa halisia. hii itawezekana mara tukapoanza kufikiria outside the box. mawazo ya membe, lowasa, slaa nk yatoke. Kuna watu wengi hawatajwi ambao wana uwezo na wameshaprove uongozi. kubwa zaid media zetu ziache njaa, kila siku wanatuaminisha tuwakubali watu wanaowataka wao. kama kuna mtu anaijua move ya Obama kuelekea state house atujuze.

Tulijua JK angeweza kuwa rais for the past 20 years throu Rai aka nguvu ya hoja. na matokeo unayaona waandishi waandamizi leo wote wako mjengoni. Tubadilike! nimesomeka?
 
Back
Top Bottom