Kinyume na Ulaghai: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliridhiwa na chombo halali cha Zanzibar!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
attachment.php

attachment.php

My Take:

Madai ya muda mrefu kuwa muungano haukuridhiwa na Wazanzibari hayana msingi. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni halali kwani vyombo halali viliridhia pande zote za Muungano.

Uhalali wake hata hivyo hauzuii Wazanzibar kutaka kujitoa kwani hata leo chombo kile kile kilichoridhia Karume atie sahihi makubaliano ya Muungano bado kipo na kinaongozwa na Dr. Shein.

Wazanzibar wakitaka wakishawishi chombo hicho kuondoa ridhaa yake ili hatimaye Baraza la Wawakilishi lipitishe utaratibu wa Zanzibar kurudi katika status quo ya April 25, 1964.z
 
Attachments

  • zanzibar1.jpg
    zanzibar1.jpg
    76.4 KB · Views: 1,083
  • Zanzibar2.jpg
    Zanzibar2.jpg
    99.4 KB · Views: 1,062
MMKJ, acha kupotosha watu,

Msome mwanasheria Pasco

Mkuu Mzee Mwanakijiji, with due respect, Muungano uliridhiwa bara tuu na sio Zanzibar!.

Sio lazima kila mkataba uwe ni wa maandishi, lakini mkataba wowote wa ardhi, land au pango, lazima uwe wa maandishi!. Wewe unaweza kununua gari na kumzawadia mpenzi/mke/ ndugu au mzazi kwa kauli tuu na ukawa ni mkataba halali!.

Lakini kama una land yako, ukiamua kumzawadia yoyote, hata ukimzawadia kwa kauli, lazima maandishi yafuatie ndio yatakayo halalisha hiyo kauli!.

Mzizi asili haswa wa muungano ni kauli, ya Nyerere na Karume.

Nyerere " Sisi ni ndugu, kwa nini tusiungane?".
Karume " Tuungane, wewe rais. mimi makamo".

Shughuli ilianza na kumalizika in a split of a second!.

Kwa vile hizi ni nchi mbili tofauti zenye uhuru wake na zote ni Jamuhuri huru, kauli pekee haitoshi kuziunganisha, lazima kufuata taratibu, sheria na kanuni ili kuhalalisha nia na kauli hizo, ndipo zikaandaliwa hizo articles of union!.

Articles zile japo zilikosa sifa ya kisheria ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisheria liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisheria, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.

Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.

Kisheria Muungano ni wa bara tuu, ndio maana Dourado alipomtonya Jumbe kuhusu Zanzibar kutouratify muungano na wakataka kuweka mambo sawa, Jumbe alishughulikiwa ipasavyo!.

Tumewanyanyasa sana, its about time now, we just lets them go!
 
Last edited by a moderator:
MMKJ, acha kupotosha watu,

Msome mwanasheria Pasco

nimeisoma na haina msingi wa historia; yote anayoyasema ni kweli lakini ana assume (kwa makosa makubwa) chombo halali cha Wazanzibar wakati ule hakikuridhia Muungano. Halafu inaonekana umesoma alichoandika Pasco kana kwamba ndivyo ilivyotokea (as historical fact) wakati alichoandika ni ubunifu tu wa fikra zake.
 
kwanza wanaojiita wanzibaari asili yao siyo zanzibar....................wengi wao asili yao ni msumbiji katika kisiwa cha pemba............wanadhani udini utawapeleka mbali ...........la hasha hawafiki kokote kule...............waulizeneni taiwan walipotaka kujitenga na uchina nini kilitokea. mwanzilishi wa uamsho ni dk shein kwa taarifa yenu kama hamjui.............swali kwanini shein?

NAOMBA NIISHIE HAPA KWA LEO HOPE 2SEE U 2MORO

UKIWA NA MASWALI NIPM

SENIOR INTELLIGENT OFFICER (CIA)
 
Anayetaka kubisha abishe tu; hakuna Mzanzibari hata mmoja kwenye Revolutionary Council aliyepinga Muungano!

Kaka unaakili sana natamani nikutane na wewe nibadilishe mawazo hata dakika 10 kama inawezekana . Kunakitu bado Wazanzibari hawaelewi kuhusu muungano.................naomba wale wanaoshabikia kuuvunja muungano wasome kuhusu tiananmen square china

_40256105_man_blocks_tank_238.jpg
 
kaka unaakili sana natamani nikutane na wewe nibadilishe mawazo hata dakika 10 kama inawezekana . kunakitu bado wazanzibari hawaelewi kuhusui muungano.................naomba wale wanaoshabikia kuuvunja muungano wasome kuhusu tiananmen square china

_40256105_man_blocks_tank_238.jpg

kulitokea nini? mbona waweka vifaru tena ..let them go hatutaki kuanza kulipuliwa huku bara bure kisa muungano
 
MMKJ, acha kupotosha watu, Msome mwanasheria Pasco
Pasco? Who the bloody hell is Pasco? Jamani tuache utani na watu kama Pasco tukae nao chonjo kweli kweli, ni opportunist anaetumika tu kwa malengo anayoyajua yeye. Zanzibar wakitaka kuondoka rukhsa, kinawazuia nini! Wasianze kutuchanganya eti hawakushirikishwa, waache kabisa kutafuta visingizio visivyo na kichwa wala mguu.
 
Last edited by a moderator:
nimeisoma na haina msingi wa historia; yote anayoyasema ni kweli lakini ana assume (kwa makosa makubwa) chombo halali cha Wazanzibar wakati ule hakikuridhia Muungano. Halafu inaonekana umesoma alichoandika Pasco kana kwamba ndivyo ilivyotokea (as historical fact) wakati alichoandika ni ubunifu tu wa fikra zake.

Uhalali wa kutoka kwenye makabrasha ya CIA? tuoneshe uhalali wa kutoka Serikali ya Zanzibar na Tanganyika.

Kama hauna, kaa kimya. Unajuwa sana kuwa huu ni muungano ulioshadidiwa na Nyerere kwa sababu ya kueneza Ukatoliki Zanzibar.
 
Anayetaka kubisha abishe tu; hakuna Mzanzibari hata mmoja kwenye Revolutionary Council aliyepinga Muungano!

Asante sana Mwanakijiji kwa document hizo:

Cha kujiuliza ni kwamba yeyote anayeupinga muungano ni Muhaini maana anayapinga mapinduzi ya Zanzibar.

Kwanini wanaoupinga muungano wasiyapinge kwanza mapinduzi yaliyomuweka Karume madarakani? Maana serikali inaitwa ya mapinduzi na hata documents inasema revolutionary council wamekubali unanimously... au ni mimi sielewi maana ya neno unanimously? Ina maana wana mapinduzi walipiga kura na kukubali muungano kama documents inavyosema.

Na kila siku tunasikia kwamba SMZ kazi yake ni kuyalinda mapinduzi hayo, sasa iweje leo UAMSHO walete chokochoko na kusema tujadili muungani bila kwanza kuyajadili mapinduzi yenyewe: Inafaa kwanza wayajadali mapinduzi, na waiondoe madarakani serikali iliyoapa kuyalinda mapinduzi hayo either kwa boz la kura, mtutu au kwa njia nyingine zinazofaa.. wakimaliza hayo ndo sasa waje kujadili muungano...

Mwisho ningependa kujua tu kwanini hizo documents zilikuwa approved for rease 18.11.1997... je kulikuwa na kesi au nini kilichopelekea kutolewa
 
Acha kuwatukana wazanzibar...ina maana wao mataahira hadi wapelekwe pelekwe kiasi hiko? Nyerere aeneze ukatoliki ili iweje.. Unamfananisha Nyerere na wale wazee wenu wa uamsho? Lini ulimuona anaongelea kusambaa kwa ukatoliki ama ni nyie na imaginations zenu za kipumbavu ambazo hazi exist.. Let em go na najua wakishajitoa na kuanza kupigika wataanza kuilamu Tanganyika kumbe wamefeli wenyewe kimikakati.
 
Mwisho ningependa kujua tu kwanini hizo documents zilikuwa approved for rease 18.11.1997... je kulikuwa na kesi au nini kilichopelekea kutolewa

Nyaraka zote za intelligence na zile ambazo ziko 'classified' zinalindwa kutolewa hadharani kwa muda wa miaka mbalimbali. Kiwango cha chini ni miaka 30 na nadhani kiwango cha juu ni miaka 70 kutegemeana na nchi. Nyaraka hizo zilikuwa classified kwa miaka thelathini naamini. Sasa hivi nyaraka za Tanzania zilizokuwa zimekuwa classified kwa miaka 30 na 40 sasa hizi zinatakiwa ziwekwe wazi - kama wasomi wetu wangeng'ang'ania na waandishi wetu kupigania.
 
Duu kazi kweli kweli,kuna kitu watanzania wengi hatukijui hapo, kama Bunge halikuwepo na baraza la mapinduzi ndio kila kitu kwa wakati ule,sasa kwa nini Muungano usiwe halali? Na pia kwa nini wasingeuratimisha baada ya kupata bunge?

Kama sheria inavyotaka?wakati umefika wananchi kwa maslahi ya nchi zote 2 waamue ila kusiwe na shinikizo la wachache kuamua juu ya wengi!hasa pesa chafu toka nje!!
 
Duu kazi kweli kweli,kuna kitu watanzania wengi hatukijui hapo,kama Bunge halikuwepo na baraza la mapinduzi ndio kila kitu kwa wakati ule,sasa kwa nini Muungano usiwe halali?na pia kwa nini wasingeuratimisha baada ya kupata bunge?kama sheria inavyotaka?wakati umefika wananchi kwa maslahi ya nchi zote 2 waamue ila kusiwe na shinikizo la wachache kuamua juu ya wengi!hasa pesa chafu toka nje!!

Hivi hujasikia Shein anaitwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi? au mnafikiria "Baraza la Mapinduzi" halipo? Ndio chombo cha juu Zanzibar - inaitwa "Revolutionary Council". Baraza la Wawakilishi bado haliaminiki kuongoza Zanzibar.
 
Anayetaka kubisha abishe tu; hakuna Mzanzibari hata mmoja kwenye Revolutionary Council aliyepinga Muungano!

Upotoshaji wako usio na mashiko waambie hao hao vilaza wenzako huko Tanganyika.
Ikiwa mwanasheria wa Z'bar (Wolfred) wakati ule hakuwa na taarifa wala kutia saini yake na hilo alikiri mwenyewe mara kadhaa sasa huo ni uhalali gani? Usikurupuke na kuandika na kutuletea chiti za zisizo na mashiko.

Kwa mujibu wa Nassor Moyo "huu muungano haukuwa na mashiko yyte isipokuwa ulikuwa wa kulazimishwa kwa njia ya vtisho kutoka kwa Nyerere (LTULLAAh) na hzo union matters zilikuwa 11 tu

Hata hivo muungano wenyewe ulikuwa wa muda tu wa miaka 10 na ilipokaribia kuisha ndio huyu adui wetu Nyerere aliopomuita Karume akakataa ndio Nyerere akamuuwa Karume"

Usipotoshe Mwanakijiji ikiwa unataka ushahidi usituletee cjui intelejensia zako nenda kwa Professor Shivji na Mwanasheria Mkuu wa Z'bar utapata kujua kuwa hata huo muelekeo wa muungano Karume aliambiwa na Nyerere kuwa ni Muungano wa Afrika mashariki na sio Tanganyika Na Z'bar.

Tena unaiscan ili ionekane kuwa ni ya kweli duh! ama ww huna tofauti na yule mwandishi wa habari wa POLISI wa Z'bar alosema kuwa "MUAMSHO wamesambaratika na Muhadhara umehudhuriwa na watu kdogo tena kwa ajili ya swala ya alghaaswir" na hali watu walijaa mpaka uwanja wa Malindi wote ukafurika na wakaibika siku ya Jumapili.
 
''wazanzibar wanaoleta fujo kwa kisingizio cha kupinga muungano wamevimbiwa amani,wamevimbiwa raha''
- Ally Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Tanzania.
 
Unaonekana huu muungano ulikuwa ni wa Tangayika tu maana kila ushahidi wa muungano uko Tanganyika!!! Basi cjui kama Tanganyika Ulijiunga na kujichukulia kila kitu cha muungano au vp?

Maana likitokea suala la ushahidi wa muungano Tanganyika ndio hujitutumua kutoa maelezo lakini kule Zenji wanakwambia ss hatuna waraka huo na wala hatuwahi kuuona na wala hatuna uhakiaka na waraka huo kw7bu hakuna maelezo kuhusiana na waraka huo.

Mfano hakuna mwanasheria hata mmoja wa Z'bar alokiri kuwepo kwa waraka wa muungano alafu leo wee Mwanakijiji watuletea siasa za kizushi kwa kuuhalalisha upuuzi huu naona kwa Wazanzibari huna cha kuwaeleza maana wako tayari kwa llte hata kifo ni bora kuliko kutawaliwa na Watanganyika na soon utasikia khabari mzito wakati hilo Tume la Katiba likijaribu kuingia kule Zenji.
 
Nyaraka zote za intelligence na zile ambazo ziko 'classified' zinalindwa kutolewa hadharani kwa muda wa miaka mbalimbali. Kiwango cha chini ni miaka 30 na nadhani kiwango cha juu ni miaka 70 kutegemeana na nchi. Nyaraka hizo zilikuwa classified kwa miaka thelathini naamini. Sasa hivi nyaraka za Tanzania zilizokuwa zimekuwa classified kwa miaka 30 na 40 sasa hizi zinatakiwa ziwekwe wazi - kama wasomi wetu wangeng'ang'ania na waandishi wetu kupigania.

And this is the moment Mzee maana hawa jamaa wanatupigia kelele tu na kutupotezea muda.
 
upotoshaji wako usio na mashiko waambie hao hao vilaza wenzako huko tanganyika. Ikiwa mwanasheria wa z'bar (wolfred) wakati ule hakuwa na taarifa wala kutia saini yake na hilo alikiri mwenyewe mara kadhaa sasa huo ni uhalali gani? Usikurupuke na kuandika na kutuletea chiti za zisizo na mashiko. Kwa mujibu wa nassor moyo "huu muungano haukuwa na mashiko yyte isipokuwa ulikuwa wa kulazimishwa kwa njia ya vtisho kutoka kwa nyerere (ltullaah) na hzo union matters zilikuwa 11 tu hata hivo muungano wenyewe ulikuwa wa muda tu wa miaka 10 na ilipokaribia kuisha ndio huyu adui wetu nyerere aliopomuita karume akakataa ndio nyerere akamuuwa karume" usipotoshe mwanakijiji ikiwa unataka ushahidi usituletee cjui intelejensia zako nenda kwa professor shivji na mwanasheria mkuu wa z'bar utapata kujua kuwa hata huo muelekeo wa muungano karume aliambiwa na nyerere kuwa ni muungano wa afrika mashariki na sio tanganyika na z'bar. Tena unaiscan ili ionekane kuwa ni ya kweli duh! Ama ww huna tofauti na yule mwandishi wa habari wa polisi wa z'bar alosema kuwa "muamsho wamesambaratika na muhadhara umehudhuriwa na watu kdogo tena kwa ajili ya swala ya alghaaswir" na hali watu walijaa mpaka uwanja wa malindi wote ukafurika na wakaibika siku ya jumapili.
sasa kipi ni kipi mkuu, muungano ulikuwa ni wa miaka 10 au haukutiwa saini kabisa? Last time namsikiliza mzee moyo katika redio moja ya kimataifa akihojiwa alisema wazi kabisa, kwamba yeye kama waziri wa sheria wa wakati huo aliuona mkataba huo!- nenda kwenye archives za mzalendo.net walishaiweka hiyo vidio, kwa hiyo usimsingizie mzee wa watu.
 
Asante sana Mwanakijiji kwa document hizo:

Cha kujiuliza ni kwamba yeyote anayeupinga muungano ni Muhaini maana anayapinga mapinduzi ya Zanzibar.

Kwanini wanaoupinga muungano wasiyapinge kwanza mapinduzi yaliyomuweka Karume madarakani? Maana serikali inaitwa ya mapinduzi na hata documents inasema revolutionary council wamekubali unanimously... au ni mimi sielewi maana ya neno unanimously? Ina maana wana mapinduzi walipiga kura na kukubali muungano kama documents inavyosema.

Na kila siku tunasikia kwamba SMZ kazi yake ni kuyalinda mapinduzi hayo, sasa iweje leo UAMSHO walete chokochoko na kusema tujadili muungani bila kwanza kuyajadili mapinduzi yenyewe: Inafaa kwanza wayajadali mapinduzi, na waiondoe madarakani serikali iliyoapa kuyalinda mapinduzi hayo either kwa boz la kura, mtutu au kwa njia nyingine zinazofaa.. wakimaliza hayo ndo sasa waje kujadili muungano...

Mwisho ningependa kujua tu kwanini hizo documents zilikuwa approved for rease 18.11.1997... je kulikuwa na kesi au nini kilichopelekea kutolewa

Dunia hii ya ajabu kweli, wengine wakipindua wanaitwa wahaini, wangine wanamapinduzi. Wate halali?
 
Back
Top Bottom