Kinyerezi kwachafuka, Wananchi wakataa kudhulumiwa

Mutwale

Member
Oct 20, 2010
67
19
Wanajanvi moto na hasira za watanzania, juu ya wanachaita dhuluma na wizi wa mchana unaotaka kufanywa na selikari kwa kupitia halmashauri ya manispaa ya Ilala! Unawaka hapa kinyerezi, raia wanamsubiri Mkurugenzi aje kutoa ufafanuzi! Lakini UMMA unaonekana kujawa na hasira!

News nyingine baada ya jamaa kuingia.
 
Wananchi wa Kinyerezi wanaoishi katika eneo lililopimwa viwanja vipya wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara kwa kushirikiana na mwenyekiti wao wa mtaa na kuazimia kuonyesha hasira zao kuhusu Serikali kuamua kupima viwanja vyao kinyemela bila kuwashirikisha kikamilifu.

Wameagiza zoezi la kuuza viwanja hivyo wakati ni makazi yao ni ukiukaji wa haki zao. Serikali haikupima eneo la wazi bali ilipima eneo ambalo ni makazi ya watu. Wanalalamika kwamba wanasikika serikali inaanza kuuza hivyo viwanja bila hata kuwashirikisha na hawajui hatima yao

Source: Channel Ten tv
 
Hapo watu (watendaji wa wizara ya ardhi aka mission town) wanajaribu kuwaibia wananchi, kazi ipo!!
 
serikali inaposhindwa kuwaongoza watu katika njia ya haki, watu hutafuata mbadala kwa kuunda serikali yao nadni ya serikali kuu. kinyerezi ni mfano tu llkn migogoro ya viwanja imetapakaa nchi nzima!
 
Wananchi wa Kinyerezi wanaoishi katika eneo lililopimwa viwanja vipya wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara kwa kushirikiana na mwenyekiti wao wa mtaa na kuazimia kuonyesha hasira zao kuhusu Serikali kuamua kupima viwanja vyao kinyemela bila kuwashirikisha kikamilifu.

Wameagiza zoezi la kuuza viwanja hivyo wakati ni makazi yao ni ukiukaji wa haki zao. Serikali haikupima eneo la wazi bali ilipima eneo ambalo ni makazi ya watu. Wanalalamika kwamba wanasikika serikali inaanza kuuza hivyo viwanja bila hata kuwashirikisha na hawajui hatima yao

Source: Channel Ten tv

Wananchi hao kama hawana hati miliki ya viwanja hivyo ni bure, kitakachofuata hapo ni kuingiza siasa tu. Huwezi pata eneo katika Tanzania hii ambalo utaambiwa halina mwenyewe ni ndoto, watu walikuwa wanalima tangia enzi za mababu wa mababu. Cha msingi hapo ni kwamba ardhi ni mali ya Taifa na mwenye mamlaka na ardhi hiyo ni rais wa jamhuri ya muungano kwa mujibu wa katiba. Nimeona watu kibao wamenyang'anywa ardhi zao na kufidiwa mazao yao kama minazi, etc. Wananchi wa kinyerezi wawe wapole tu kwani kama viwanja hivyo vilikuwa havikupimwa basi dhahiri kuwa si mali yao kisheria. Sijawahi kuona nchi inayovunja sheria kama Tanzania na watu wanaangaliwa tu, mtu ananunua shamba anajenga bangaluu bila hata ya kibali cha ujenzi cha halmashauri husika.
 
Mfumo wa umiliki ardhi Tz ni moja ya mabomu yatayokuja kutusambaratisha.hakuna cha kubadili hilo bila katiba mpya ya wananchi wenyewe.Dr slaa anapopiga kelele za katiba wengine wanamwona kama kichaa.hilo la kinyerezi cha mtoto tunakoelekea ni kubaya zaidi!
 
Hii itakuwa ni kali ya mwaka kwa sababu kwa utaratibu wa kawaida wananchi hawa walitakiwa walipwe fidia kwa tathmini ya mali iliyopo kwenye mwashamba hayo, ndipo upimwaji ufanyike. Hivi ndivyo ilivyofanyika kwa miradi yote ya viwanja vya serikali kama vile Mbweni, Bunju, Tuangoma, Kibada na hata Buyuni na maeneo mengine. Suala hili ni la kiutekelezaji kwa sababu nina hakika sheria ndivyo inavyosema, kwa sababu wamiliki hao si wavamizi na walikuwa wanamiliki eneo hilo kwa umiliki wa kimila mpaka pale serikali ilipoamua kwamba eneo hilo lichukuliwe kwa manufaa ya umma kama hayo ya kuanzisha mradi maalum wa makazi.

Wakati kwa upande mmoja nachelea kukubali kwamba watendaji wa serikali wanaweza kupuuza matakwa ya kisheria kiasi hicho, ni vizuri serikali iakliangalia hili kusudi lisiwe chanzo cha migogoro inayoweza kuepukwa lakini yenye uwezekano wa kuleta machafuko. Hili si jambo la kisiasa na wale wanaoanza kusema kiongozi fulani wa upinzani aingilie, wanataka kuvuruga mambo ili watu hawa wacheleweshewe ufumbuzi wa suala hili.
 
Back
Top Bottom