Kingwendu Aingizwa Mjini Tsh. Milioni 1.5 Mwanza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
2883326.jpg

Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ Saturday, August 22, 2009 7:40 AM
Komedian aliyekwenda eji Bongo, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ ameingizwa mjini na promota mmoja jijini Mwanza. Kingwendu akiongea na Showbiz mapema wiki hii alisema kwamba, promota huyo amemtia ndani kiasi cha fedha shilingi milioni 1.5 ambazo aliziingiza baada ya kupiga mzigo Kanda ya Ziwa.

Said: “ … (anataja jina la mtu aliyemliza) amenifanyia kitu kibaya sana, alinichukua vizuri Bongo akanipa advance, kula, kulala haikuwa na matatizo, kwahiyo nikamuamini lakini kumbe siyo mtu kihivyo.

“Baada ya kupiga shoo kwenye vijiji vya Zalagula, Kasaratu, Nyanango na Kanyala jijini Mwanza, nilikuwa nimekusanya shilingi milioni 1.5 kibindoni lakini juu kwa juu nilipata ‘dili’ kwahiyo nikaunganisha shoo.

“Promota wangu aliniomba nimpe pesa hizo ili akaniwekee kwenye akaunti yangu, mimi kwa sababu nilikuwa nimeshamuamini nilimpa lakini huwezi kuamini, baada ya hapo kila nikimpigia simu ni stori tu.

Hivi sasa nimemfungulia mashataka polisi kwa kosa la wizi wa kuaminiwa.” alisema Kingwendu.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2883326&&Cat=1
 
Kama hii habari ni ya ukweli (ie sio jokes), mimi nadhani ungeiweka kwenye Celebrities Forum, au walau Entertainment Forum. Ninavyojua mimi habari ikiwekwa hapa inaonekana kama ni ya kufurahisha tu na si ya kweli.
 
Back
Top Bottom