Kingunge, Makamba na Mgeja wamezidi kujikomba kwa Kikwete

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3][/h]


thumbnail.aspx

Taarifa za vyombo vya habari za hivi karibuni zilipasha kuwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja , katibu mkuu wa zamani wa CCM Yusuf Makamba na mshauri wa zamani wa rais Kingunge Ngombale Mwiru walimshambulia waziri mkuu Mizengo Pinda hadi kumtaka ajipime na kuwajibika. Sababu wanazotoa eti kama mawaziri wanne waliwajibishwa kutokana na ufujaji wa pesa za umma ulioibuliwa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa pesa za serikali (CAG) basin a waziri mkuu awajibike.
Kwani serikali ni iliyofanya madudu ni ya Pinda au Jakaya Kikwete?
Kwanini hawahoji kubaki kwa mawaziri wengine waliotuhumiwakama vile George mkuchika na Adam Malima?
Kwanini hawamuhoji Kikwete kutowawajibisha mawaziri hawa?
Je kati ya Kikwete na Pinda nani anamhitaji mwenzake?
Wamesahau kuwa Pinda aliokoa jahazi la Kikwete baada rafiki yake Edward Lowassa kuchafuka? Wanakimbilia kwenye mashina huku wakiogopa shina je huu si unafiki au wametumwa na mitandao yao kuanza kupayuka. Waziri mkuu amefanya vizuri kutowajibu maana angewapandisha chati.
Mbona hawahoji CAG kutosema ukweli kuhusiana na mahesabu ya jeshi au ofisi ya rais ambayo inajulikana kwa ufujaji kuliko hata hizo wizara nyingine ambazo mawaziri wake wamewajibishwa?
Kwanini hawahoji ukimya wa Kikwete kila unapozuka mgogoro hasa ufisadi?
Kwanini hawahoji malipo anayopata Lowassa ya ustaafu wakati hakustaafu?
Kwanini hawaelezi wazi wazi kosa la Pinda badala ya kuzungukazunguka kama siyo visa na unafiki na kujikomba kwa Kikwete? Ukweli ni kwamba hawamsaidii wala haitawasaidia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom