Kingunge awashiwa moto

mkatofa

Member
May 6, 2010
38
7
Mbunge wa jimbo la Kahama James Lembeli amesema anamshangaa kada wa muda mrefu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru kuibuka sasa na kupingana na mwenendo wa baadhi ya viongozi wa chama hicho tawala kwamba hauendani na maadili tuliyoachiwa na Baba wa Taifa.Akizungumza na gazeti hili mjini Dar es salaam jana Lembeli alisema ni hivi karibuni tu kwenye bunge la mwaka jana Kingunge akiwa ni mbunge alikuwa akiwabeza na kuwashambulia wabunge waliokuwa mstari wa mbele kuwapinga mafisadi.Alisema Kingunge alionyesha dalili za wazi kwamba yupo pamoja na watuhumiwa wa ufisadi hivyo inashangaza sana kwa mzee huyo kutoa kauli kama alizotoa juzi kwenye kongamano la kumbukumbu ya mwalimu Nyerere lililofanyika chuo kikuu cha Dar es salaam.

"Sina uhakika kama ndoa ya Mafisadi na Kingunge imevunjika,au ni danganya toto na pengine mzee aliogopa kuzomewa pale chuo kikuu lakini naamini mzee huyo hana dhamira ya kweli ya kufuata na kuenzi maadili ya mwalimu Nyerere ikiwemo mapambano ya rushwa"Alisema Lembeli.Lembeli wazee kama kina Kingunge wanatakiwa kutubu dhambi za kumsaliti mwalimu kwa kushirikiana na baadhi ya watu ambao wameingia ndani ya CCM ambao sio waadilifu.Kingunge, ambaye amewahi kuwa waziri katika awamu zote za serikali tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa msemaji mkuu katika kongamano la Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM ) Jumamosi iliyopita, alisema vitendo vya viongozi wa serikali vikiwemo vya kumiliki ardhi kubwa, vimewafanya Watanzania wengi hasa wakulima wadogo kuishi maisha yaliyojaa dhiki.Katika kongamano hilo lililofanyika kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,

Mzee Kingunge alisema viongozi wengi serikalini wamepuuza maadili ya uongozi yaliyotiliwa mkazo na Mwalimu Nyerere, na hivyo kuua mipango mizuri ya muasisi ya utawala wa awamu ya kwanza ya kuinua hali ya wakulima wadogo wadogo hapa nchini.Ngombale Mwiru alishangaa kuona serikali badala ya kuinua wakulima wa Tanzania kwa kuwasaidia kuendesha kilimo cha kisasa na chenye tija, inaruhusu wawekezaji kutoka nje ya nchi ambao wanachochuma kinaenda kunufaisha mataifa ya nje.Aliongeza kuwa hakuna sababu ya kuleta wawekezaji katika sekta ya kilimo na kuwaacha maelfu ya vijana wanaohitimu elimu ya vyuo vikuu wakihangaika kutafuta kazi."Kuleta wawekezaji wa nje ni sawa na kwenda kuteka maji mbali wakati unayo karibu yako," alisema Mzee Kingunge ambaye ni kiongozi pekee anayeshikilia rekodi ya kuandika ilani ya uchaguzi ya CCM katika chaguzi kuu tatu zilizopita.Kingunge alisema ili kuondokana na hali hiyo, lazima kuwe na viongozi wa namna mpya, wenye uchungu na wananchi, sio wale wanaofaidika kupitia umaskini wa wananchi.

"Tunataka mapinduzi, mageuzi ya ndani, kujisafisha ili turudi kwenye misingi. Tunataka viongozi wa namna mpya, mko kwenye chama kutetea misingi ya chama. tunataka chombo cha kuongoza, si suala la maneno ila msimamo wa dhati na vitendo vyake," alisema.Alisema CCM inahitaji mageuzi ya dhati ndani ya chama ili kuenzi kwa dhati nia ya waasisi wa CCM.
 
An octogenarian senile.......what do you expect?.......alivuna sna pale Ubungo mpaka Pinda akamtoa mkuku...ndiye huyu leo?
 
Jaman watanzania nan katuroga sasa kibaya alichoongea kingunge nin...anachoongea c ni msaada kwa taifa letu...ndo yaleyale Lowasa anashaur taifa kwa mazur mnamjbu kwa tuhuma zake embu 2jaribu kuacha unafka then 2angalia tunaweza vp kuondoka katka hal ya umasikini! Kelele za fisadi fisadi tumechoka tuangalie tufanye nn?
 
HUYO LEMBELI NA UNAFIKI WAKE ANACHOSEKA NI NINI??MBONA WANATUCHANGANYA??ALITAKA AFANYE NINI??MZEE KALA CHUMVI ASHAPIMA UPEPO AMEGUNDUA NI NINI CHA KUFANYA NA KUSEMA EHHEeeeeee!!!!!!!!!!!
 
haya bwana watanzania tukimchukia mtu hata constructive idea zake tunatupa kapuni.Tubadilike!
 
Yaani sasa hivi hali ni tete kwa magamba, yanaoneana wivu hata kwenye kupinga Ufisadi. Akiibuka mwingine anapinga ufisadi yanakuja juu, unaona haka kazee nako kalitaka kasifiwe peke yake kwamba ndo kanapambana na ufisadi hapo ungeona hadi magego (kama bado kanayo).

Awamu hii mpaka yatoane roho pumbaf... zao
 
HUYO LEMBELI NA UNAFIKI WAKE ANACHOSEKA NI NINI??MBONA WANATUCHANGANYA??ALITAKA AFANYE NINI??MZEE KALA CHUMVI ASHAPIMA UPEPO AMEGUNDUA NI NINI CHA KUFANYA NA KUSEMA EHHEeeeeee!!!!!!!!!!!

Lembeli yuko sahihi kabisa Mzee Kingunge hajulikani msimamo kama ni mpinga mafisadi ama yuko na MAFISADI, na kwa kawaida binadamu hutakiwi kuwa vuguvugu
 
Jaman watanzania nan katuroga sasa kibaya alichoongea kingunge nin...anachoongea c ni msaada kwa taifa letu...ndo yaleyale Lowasa anashaur taifa kwa mazur mnamjbu kwa tuhuma zake embu 2jaribu kuacha unafka then 2angalia tunaweza vp kuondoka katka hal ya umasikini! Kelele za fisadi fisadi tumechoka tuangalie tufanye nn?

Ujue mtu ukifanya mazuri 100 ukijafanya baya moja linafunika mazuri yote na itachuktwa muda kurudisha hadhi yako kwahiyo sitoshangaa kwa hili ulilosema la kingunge na lowasa
 
Babu ni mnafiki angeongea hivyo wakati akiwa mbunge na waziri analiongea hilo leo ili tumwone yuko safi? Ajue ccm hakuna aliye msafi hata mmoja
 
Mwl.JK Alipata kunena kuwa ukianza kuila nyama mtu.......................malizia mwenyewe.Yanayotokea leo pale kwenye jembe na nyundo ni kama lile onyo la Mwl.JK kuwa ukianza dhambi ya ubaguzi..............malizieni wanajamvi.
 
Back
Top Bottom