Kingine kinachomwangusha JK ni lugha!!

KAULI MBIU MPYA ZA JK na CCM:
Umasikini zaidi, Njaa zaidi, Ujinga zaidi, Maradhi zaidi, Giza zaidi, Mikoa mingi zaidi, Wilaya Nyingi zaidi, Mawaziri wengi zaidi, Wezi na Wizi zaidi - Yote haya yanapelekea "Maisha Bora kwa Wateule na Watawala na Maisha Duni kwa Watanzania wengi."

duh! You have made my day..
 
Mh. Rais kikwete katika kampeni zake za mwaka 2005 alikuja na slogan au falsafa ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" Ikibebwa Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya!!!, kwa lugha hii alioitumia alikamata hadi viongozi wa dini, na watu wa nyanja zote!!! Kwa masikini ambao kwao Neno"MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" Lilibeba sanduku la matumaini mapya, kujichomoa kwenye jalala la umasikini na kujiweka angalau katika uwezo wa kumpa maji mtu mwingine anaejiskia na kiu! KILICHOTOKEA ni tofauti na walivyotegemea...lindi la umaskini, rushwa, ufisadi viliongezeka! UCHAGUZI WA 2010 alikuja na "ARI ZAIDI, KASI ZAIDI NA NGUVU ZAIDI", Lugha hii pia iliwahadaa watu japo wengi walizinduka ilibaki kwa watu wa vijijini ambao walitoa nafasi kwa mara nyingine japo sina uhakika sana Kama alishinda tena au lah! kwa sababu Mambo yaliyojadiliwa kwenye WHITE PAPER HAYAJATIMIZWA....! Kwa sasa kila kitu kimebadilika! Watu wamechoka wameshajua kuwa "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" ILIKUWA ZUBAISHA *****.. ILIKUWA LUGHA YA UONGO! Kuweni makini 2015.

Lugha hizi alizozitumia Jakaya zisizoendana na matendo ndio zilizowapotosha Watanzania wengi kumchagua kwa vipindi vyote viwili,wacha wananchi wavune kile walichokipanda tena nnatamani sana hali iwe ngumu zaidi ya hii ili 2015 tuwe wote kwa lugha moja kuikataa ccm na mambo yake yote.
 
Nadhani kichwa kingesomeka kuwa Kinachomwangusha JK ni kauli mbiu zisizotekelezeka.Nilidhani ulimaanisha lugha ya kuongea,ambayo bado pia kwake ni tatizo.
 
Mh. Rais kikwete katika kampeni zake za mwaka 2005 alikuja na slogan au falsafa ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" Ikibebwa Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya!!!, kwa lugha hii alioitumia alikamata hadi viongozi wa dini, na watu wa nyanja zote!!! Kwa masikini ambao kwao Neno"MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" Lilibeba sanduku la matumaini mapya, kujichomoa kwenye jalala la umasikini na kujiweka angalau katika uwezo wa kumpa maji mtu mwingine anaejiskia na kiu! KILICHOTOKEA ni tofauti na walivyotegemea...lindi la umaskini, rushwa, ufisadi viliongezeka! UCHAGUZI WA 2010 alikuja na "ARI ZAIDI, KASI ZAIDI NA NGUVU ZAIDI", Lugha hii pia iliwahadaa watu japo wengi walizinduka ilibaki kwa watu wa vijijini ambao walitoa nafasi kwa mara nyingine japo sina uhakika sana Kama alishinda tena au lah! kwa sababu Mambo yaliyojadiliwa kwenye WHITE PAPER HAYAJATIMIZWA....! Kwa sasa kila kitu kimebadilika! Watu wamechoka wameshajua kuwa "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" ILIKUWA ZUBAISHA *****.. ILIKUWA LUGHA YA UONGO! Kuweni makini 2015.

Achilia mbali kuwadanganya watu kuhusu maisha bora kwa kila Mtanzania, lakini watu wengi wanadai walimchagua kwasababu ni handsome na angeonekana vizuri kwenye noti. Mibongo tunasafari ndeefu ya kuelekea mabadiriko
 
Unamaanisha Watanzania hupenda kuweka Matumaini yao kwa wanasiasa badala ya kuchapa kazi..?
Akija mwingine kutoka upande wa pili mtamtumaini?

Umeuliza swali la msingi sana hapa. Lakini ni muhimu kukubali kuwa siasa ina mchango mkubwa sana katika harakati za kuleta maendeleo ya mtu binafsi na maendeleo ya jumla. Hebu fikiria unapokuwa na nchi ambayo kipaumbele ni matumizi ya viongozi badala ya kuwekeza, madhara yake ni kudumaza shughuli mbalimbali za kukuza uchumi. Uwepo wa barabara bora, mabenki yenye nguvu, sera bora juu ya utoaji huduma muhimu kama leseni, hati ya umiliki, mgawanyo bora wa rasilimali za nchi, utawala bora (absence grand corruption) nk. Vitu hivi huchochea haraka maendeleo ya watu na nchi kwa ujumla.
 
....Ulikuwa ni usanii tu wa kuhakikisha anaingia Ikulu lakini hana hata chembe moja ya leadership quality hata ya kuwa mjumbe wa nyumba kumi kumi achilia mbali kuwa Rais wa nchi.

Vp ule mgogoro wa kifamilia, ww umeweza kuusuluhisha ? mbona ww familia inakushinda kuongoza, tusemeje sasa ?:bange:

mh. Rais kikwete katika kampeni zake za mwaka 2005 alikuja na slogan au falsafa ya "maisha bora kwa kila mtanzania" ikibebwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya!!!, kwa lugha hii alioitumia alikamata hadi viongozi wa dini, na watu wa nyanja zote!!! Kwa masikini ambao kwao neno"maisha bora kwa kila mtanzania" lilibeba sanduku la matumaini mapya, kujichomoa kwenye jalala la umasikini na kujiweka angalau katika uwezo wa kumpa maji mtu mwingine anaejiskia na kiu! Kilichotokea ni tofauti na walivyotegemea...lindi la umaskini, rushwa, ufisadi viliongezeka! Uchaguzi wa 2010 alikuja na "ari zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi", lugha hii pia iliwahadaa watu japo wengi walizinduka ilibaki kwa watu wa vijijini ambao walitoa nafasi kwa mara nyingine japo sina uhakika sana kama alishinda tena au lah! Kwa sababu mambo yaliyojadiliwa kwenye white paper hayajatimizwa....! Kwa sasa kila kitu kimebadilika! Watu wamechoka wameshajua kuwa "maisha bora kwa kila mtanzania" ilikuwa zubaisha *****.. Ilikuwa lugha ya uongo! Kuweni makini 2015.

nafikiri akija tena maneno yake yatasomeka kinyumenyume ria yapm sika yapm na vungu yapm!!!

Katika kipindi cha Kikwete kaongeza wastani wa umri wa kuishi Mtanzania kutoka miaka 48 (au 50) wakati anachukuwa madaraka mpaka kufikia miaka 55. Au huoni kuwa hapo karibu kila mmoja kafaidika kwa maisha bora? Na hiyo ni kwa miaka 6 aliyopo madarakani, haijawahi chart ya wastani wa umri wa Mtanzania kupanda kama kipindi hiki cha Kikwete ni rekodi ambayo anaishikilia.
 
Ni kweli wa Tanzania tulipenda boom na sasa limetulipukia! Tujifunze kutokana na makosa!.
 
Katika kipindi cha Kikwete kaongeza wastani wa umri wa kuishi Mtanzania kutoka miaka 48 (au 50) wakati anachukuwa madaraka mpaka kufikia miaka 55. Au huoni kuwa hapo karibu kila mmoja kafaidika kwa maisha bora? Na hiyo ni kwa miaka 6 aliyopo madarakani, haijawahi chart ya wastani wa umri wa Mtanzania kupanda kama kipindi hiki cha Kikwete ni rekodi ambayo anaishikilia.

Hahahaha hizo takwimu alikupa daktari Jakaya au?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom