King'amuzi cha coconut kimekaa kitapeli zaidi

Mwambao

Member
Apr 11, 2011
22
6
Ndugu wana jamvi hivi karibuni nimenunua king'amuzi cha coconut huku zanzibar maana kwa kipindi hili nipo huku visiwani yaani kimekaa kitapeli zaidi maana hakuna lolote linaloendelea yaani tumelipia laki moja lakini hatupati channel hata moja ipo kama mtandao wa tigo unaingia na kutoka unaona robo saa inakosa kuona masaa 6 yaani tabu tupu
 
Kama satrtimes kila wakati no signal. Hwa jamaa wanakuja kuwekeze hpa wakati hawajajipanga tic vp au ndo yaleyale ufisad
 
kazi kweli kweli!!hivi ving'amuzi vinawaua wa2,kuna lodge moja nimekwenda pale mapokezi kuna ving'amuzi,utadhani ndio makao makuu ya Google!
 
Heh kuna king'amuzi cha nazi tena! Hata kama ni biashara huru bt this is too much maana makampuni mengi hayajajipanga kutoa huduma stahiki kwa jamii badala yake wanaleta kero kila kukicha.

Startimes
Zuku
Ting
Coconut
.....
Alaf wote hawajiwezi!
 
Heh kuna king'amuzi cha nazi tena! Hata kama ni biashara huru bt this is too much maana makampuni mengi hayajajipanga kutoa huduma stahiki kwa jamii badala yake wanaleta kero kila kukicha.

Startimes
Zuku
Ting
Coconut
.....
Alafwote hawajiwezi!

Ndg.mimi binafsi nimeifatilia hii biashara kwa karibu sana,hii unachokiona ni matokeo ya serikali yetu
kufanya mambo kisiasa zaidi plus conflicts of interest kwa baadhi ya watendaji wa mamlaka ya mawasiliano TCRA.
startime kupitia star media,ting kupitia AGAPE tv,na itv+star tv bado hawajaleta chakwao sokoni,hao juu ndio warushaji wa matangazo ya radio na tv kwenye digital kwa upande wa Bara,Clouds tv baada ya kukosa leseni ya biashara hiyo huku Bara ndio wamepeleka kingamuzi chao zbar.
kinachotekea ni wingi wa decoders sokoni ila matangazo au watangazaji ni walwale maana kila mmoja anamatangazo(content yake na kingamuzi chake)
 
Bado nakumbuka ya G-Tv maana hata wao walikuja kwa Kasi........ lakini mwisho wakawa
matapeli tu..... hivi TCRA vibali wanatoa kwa vigezo gani....
 
kuna king'amuzi kipya kinaingia sokoni soon kinaitwa BONGO NEWYORK
 
Nasikia hicho kung'amuzi cha coconut kinalipiwa laki moja si mchezo washatia ela ndani sasa wanatafuta mwanya wa kukimbia hawa wezi sana hawa
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom