Kinga ya malaria

Original Pastor

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
1,274
50
Wakuu Heshima kwanza
Napenda kuwauliza hivi Tanzania tunayo kinga ya Malaria inayotolewa na Hospital zetu kwani nauliza hivyo nimeona nchi nyingine naomba kuwauliza ili nijue inatolewa wapi???? niwaangizie Familia waende wakapate kinga. Madokta wekeni hoja
 
Kinga za malaria zipo nyingi sana zinazotolewa kwenye hospitali zetu, labda uwe 'specific' we unaongelea kinga wa aina gani na ni nchi gani umeona.

Kuna program ya kutoa vyandarua kwa kina mama wajawazito na watoto wachanga kwa 'Hati Punguzo' kujikinga na malaria, kuna dawa za SP zinatolewa kwa kina mama wajawazito hata kama hawaumwi malaria (IPTp) katika miezi 3 -4 na 6 -7 ya mimba kwa ajili ya kujikinga na malaria, kuna utafiti unaendelea Mtwara sasa juu ya huduma kama hiyo ya SP kwa kina mama wajawazito kwa watoto wachanga (IPTi), kuna tafiti zinaendelea Bagamayo juu ya chanjo ya kuzuia malaria, Kuna elimu ya afya inatolewa mahospitalini jinsi ya kujikinga na malaria etc..

We unataka/unaongelea ipi?
 
bahati mbaya huku nilipo malaria niliisoma kwenye vitabu na kuona mapicha ... but nadhani kinga ya malaria jitahidi kupigana na mbu, fukia madimbwi.. piga dawa kwenye mashimo ya vyoo once a week .. etcl!!
 
Wakuu huku niliko tumechanjwa yaani tumedungwa sundano ya kinga ya Malaria sasa nauliza hiyo kwa Tanzania yetu.
 
Njiwa...Larviciding and IRS is the way to go towards malaria elimination and then eradication. Lakini hizo intervention mbili ni 'very' expensive kwa sababu zinafanyika cycles kadhaa kwa mwaka na dawa inayotumika kwa sasa (pyrethrum products) ni expensive sana. Tanzania through NMCP kuopt LLINs, IPTp na IRS/Larviciding in selected areas ni kwa ajili hatuwezi mudu gharama za IRS kama national program, lakini si kwamba hizo intervention tunafanya ndio best.

We have been debating DDT for ages now, ni very cheap option ya pyrethrum kwa IRS/Larviciding lakini athari zake kwa mazingira ndio pingamizi kubwa...wizara za kilimo, maliasili na mazingira, maji...haziwezi kukubaliana na wizara ya afya kutimiza azma ya kutumia DDT hivi hivi tu! Lakini nchi nyingi zilizofanikiwa kueliminate/eradicate malaria ni kwa IRS through DDT, except Zanzibar wao kwa ufadhili wa waMarekani wame-eliminate malaria kwa IRS (pyrethrum) + LLINs, lakini Zanziba ni sawa na mkoa mmoja tu wa Tanzania Bara.
 
Wakuu huku niliko tumechanjwa yaani tumedungwa sundano ya kinga ya Malaria sasa nauliza hiyo kwa Tanzania yetu.

Chanjo za malaria dunia nzima ziko kwenye phases mbali mbali za majaribio...hakuna iliyothibitishwa tayari. Tena moja ya chanjo za malaria iliyoonyesha mafanikio makubwa duniani imejaribiwa Bagamoyo na taasisi ya afya ya Ifakara (IHI) na matokeo yake yatatoka kabla ya mwisho wa mwaka huu.
 
hivi hawa watu walikuwaga wapi????? UCHAGUZI UMEPITA SASA NAONA AKILI ZA WATU ZINAANZA KURUDI
MAGREAT THINKERS WANAONGEZEKA KILA KUKICHA!
THANX RIWA & CO KWA MADA ELIMISHI ZA KITABIBU
 
sasa uo uharibifu wa mazingira tanzania bara tu,ilhali zenji na nchi nyingine limewezekana?hainiingii akilini asilani
ivi ayo mazingira gani tanganyika wanataka kuyatunza?ilhali ukipima uharibifu tunaofanya ss kwa vitu vingine upo wa kumwaga??
na mazingira vs vifo vya malaria tulivonavyo je???

uwa sielewi kabisa izi akili za watu wachache wanaofanya maamuzi
 
Aza...Zanzibar walitumia pyrethrum products ambazo hazina uharibifu wowote kwa mazingira, lakini ni ghali sana, wao walipata ufadhili toka serikali ya marekani (USAID/PMI) labda kwa ajili udogo wa eneo lenyewe, kumbuka Zanzibar ni kama mkoa mmoja wa Tanzania bara, unaweza imagine cost ya mikoa 25....cost iliyotumika Zanzibar x 25!

DDT ni cheap option lakini ndio hiyo ina effects kwa mazingira.
 
Back
Top Bottom